Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Honger kwa utabiri w Yanga Yetu mpya..! Pia niongeze jambo ukiwa ugenini usikae kama bubu., Tambua wenyeji wako wanapenda kipi cha kuzungumza... NB: usivuke mipaka ,kuw mtu wa fact
 
Nachukia mgeni anakuja kwako anawasha computer sa 1 mpaka anaitwa mezani chakula Cha usiku, akimaliza kula anarudikwenye computer mpaka mnaenda kulala mnamuacha sebuleni.

F@(n bastard, mpaka watoto wanaogopa kumuambia wanataka kufanya kazizao kwenye computer, jitu limepinda mgongo linamaliza umemetu.
 
USIWEKE MIGUU KWENYE MAKOCHI AU MEZA. .

Kuna watu wanaweka miguu katoka kupuyanga nje huko anatuliza kwenye coffee table au masofa wakati anajua hayafuliwi. .
duh, sasa atajuaje na hana exposure?
 
Nachukia mgeni anakuja kwako anawasha computer sa 1 mpaka anaitwa mezani chakula Cha usiku, akimaliza kula anarudikwenye computer mpaka mnaenda kulala mnamuacha sebuleni.

F@(n bastard, mpaka watoto wanaogopa kumuambia wanataka kufanya kazizao kwenye computer, jitu limepinda mgongo linamaliza umemetu.
Mgeni anagombania rimoti na watoto....😁
 
Mie nisivyo penda kukaa kwa watu, iwe ndugu au jamaa na marafiki, naish kwangu, nikichokaaa ni home kwa wazaziii.

Hawa wenginee hapana wanisamehe tyuuh, kwan had wanani mic wenyewe niende makwao. Lol.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa namna nilivyo na mambo yangu..kukaa kwa watu kutanishinda.
 
Kwakweli hiki kipengele cha ugeni kwangu huwa ni changamoto kiasi naonekana nna roho mbaya....

Hivi serious mgeni unakaa kwangu miezi 3+ halafu bado unataka nikutreat kama mgeni nikuandalie sijui maji nikuletee msosi chumba kwako nikusafishie chumbani??? Hapana sina huu muda treatment za hivo utazipata within a week kama tofauti na hapo nna roho mbaya basi sawa.
Miezi mitatu bado anajiita mgeni?
 
.......na ikitokea chakula kimetengwa kwenye hotpots na ukapewa nafasi ya kwanza kujisevia basi consider kwamba mko wengi .......jikadirie kidogo sio unachota nyama zote hadi watoto wa mwenyeji wanakosa wanaanza kumegana......mkimaliza kula basi anza hata kuwanawisha mikono wenyeji waliomaliza kula, yaani usijikute we ndo mgeeeeeeni, kila kitu ufanyiwe.....hawatakumiss ukiondoka......
Watu mnajua kujipendekeza; yaanimuwanawishe mikono😂
 
Hiyo namba 3 ilinikuta. Nilipata mgeni ndugu yangu tena mpaka mume wangu akawa uncomfortable nyumbani kwake. Kitoto kinakaa miguu juu sebuleni kimeshikilia remote. Mr anaishia kukaa dining. Mnaenda kulala bado busy na tv na usipomfuata akalale atakesha. Kwakweli kuna baadhi ya wageni wanakera na wengine unatamani wasiondoke.
Hicho kitoto kilikuwa Cha kike😂😂
 
1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGODOGO
Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya meno, taulo na mahitaji yako mengine madogomadogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...kwa wenyeji sio vizuri.

2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI
Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.

3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

5. USIINGILIE MAZUNGUMZO
Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.

6. USITEMBELEE MAJIRANI
Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.

7. KULA VYAKULA VILIVYOPO
Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.

8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI
Usianze kutumia vifaa vya wenyeji bila ruhusa mfano unaanza kuwasha computer au vifaa vya mazoezi . Usianze kuzunguka nyumba na kuingia kila mahali labda mwenyeji wako akuoneshe sio kukagua nyumba nzima na kuingia vyumba ambavyo hujaambiwa.

9. SAIDIA KAZI
Tandika kitanda chako na safisha chumba ulichopewa kulala. Saidia kazi za hapo nyumbani ulipofikia labda wakukataze wenyeji. Sambamba na hilo utakapoondoka acha chumba katika hali ya usafi kama ulivyokikuta.

10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.

Tukutane Taifa Yanga anapiga mtu 2 bili
KWANI KOSA LA MLETA MADA NI LIPI HAPO MAANA KAWEKA NA USHAHIDI WA PICHA?
 
3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

248893095_109945061486324_4066502796358241732_n.jpg
 

Attachments

  • 248893095_109945061486324_4066502796358241732_n.jpg
    248893095_109945061486324_4066502796358241732_n.jpg
    42.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom