Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Mimi mara nyingi nilikua sili ..nikirud nawaambia nishakula naenda tu kulala
😂😂😂😂🤓🤓🤓Mkuu wee ndo komoa sasa..
Hapo sasa na wewe itabidi umtengenezee mazingira mazuri mgeni wako ata akija kwako awe huru yaani mweke mazingira ambayo asione kila analo fanya anakosea

Kipindi hicho Niliwahi zinguliwa na mfanyakazi wa pale kwa ndugu yangu
Nikaona bora niwe cool maana naweza kuzinguana nae. Nikamwalibia
ukizingatia yeye pale kaja kutafuta ila akaona sisi ndugu kama wote tupo chini yake
 
4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.
10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.
Hizo mbili kwangu muhimu sana kuzingatia mtu anapokuja kwangu, mengine nishazowea kuna jamaa yangu yeye baada ya salamu moja kwa moja kwenye Friji. Akiona juice,soda,chocolate,keki,vileja au mayai lazima apite navyo.🤣🤣
 
Mfumo wa maisha kwa dunia ya sasa unebadilika watu hawapendani umfumo wa ubepari ndio unatawala ukileta itikadi za kijaamaa unatafuta lawama na watu .Ili uheshimiwe usipende kupokea bali uwe mtoaji .
Yah kweli man ....
Ukiwa na kitu ww toa ila usipokeee
NA ukitoa usingoje shukrani sepa haraka haswaa
 
Maisha ya zamani yalikua mazuri sana mnatembeleana hadi raha..ile.jioni mnawasha moto mnakaa nje mnapiga stori za maaana za maisha
Ila siku hizi hamna hayo unaenda kusalimia ndugu kila mtu yupo busy na simu
 
Maisha ya zamani yalikua mazuri sana mnatembeleana hadi raha..ile.jioni mnawasha moto mnakaa nje mnapiga stori za maaana za maisha
Ila siku hizi hamna hayo unaenda kusalimia ndugu kila mtu yupo busy na simu
Mfumo wa maisha umebadilika kwanza wanakuona kero labda uwe na hela ila umechoka unamchongo utakubali.
 
1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGODOGO
Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya mswaki, taulo na mahitaji yako mengine madogomadogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...kwa wenyeji sio vizuri.

2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI
Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.

3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

5. USIINGILIE MAZUNGUMZO
Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.

6. USITEMBELEE MAJIRANI
Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.

7. KULA VYAKULA VILIVYOPO
Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.

8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI
Usianze kutumia vifaa vya wenyeji bila ruhusa mfano unaanza kuwasha computer au vifaa vya mazoezi . Usianze kuzunguka nyumba na kuingia kila mahali labda mwenyeji wako akuoneshe sio kukagua nyumba nzima na kuingia vyumba ambavyo hujaambiwa.

9.SAIDIA KAZI
Tandika kitanda chako na safisha chumba ulichopewa kulala. Saidia kazi za hapo nyumbani ulipofikia labda wakukataze wenyeji. Sambamba na hilo utakapoondoka acha chumba katika hali ya usafi kama ulivyokikuta.

10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.

Tukutane Taifa Yanga anapiga mtu 2 bili
"USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe", kama bado siku tano mshahara utoke itabidi nisubiri ili niondoke siku ya mshahara.
 
Kwa jinsi nilikuwa naona wageni wanavosemwa vby nyumbani kwetu.niliamua siendi KWA ndugu zaidi ya kusalimia au kuwa naenda na kuondoka.naweza kula msosi ila kulala na kuamkia hapo NEHIII.of coz hata mi sipendi wageni wasumbufu ambae akija ht donesheni hatoi.hata kusaidia usafi hakuna.utakuwa unapeleka makosa
 
Back
Top Bottom