Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Jaman mbavu sina mimi, yaani watu wameshakata tamaa ya maisha hivi unakubali uponyaji kwa mizizi huku mkiwa mmesubiliana hadi watu mamia! si angeamuru wapone kwa Neno tu sasa hadi wanakufa!
Upupu mwingine bana!:hand::hand::hand:

Mkuu Mazunguse, Biblia inaonyesha Bwana Yesu amewahi kuponya kipofu kwa kutemea mate udongo na kutengeneza tope kisha akampaka machoni (leo hii ingekuwa wewe pengine ungepigana). Nadhani unapokuwa na shida hasa maradhi makali unachotaka ni kupona tu, na mara nyingi upupu ndio unaoponyesha. Japo matapeli nao huingia humo humo.

Biblia kwenye 1Kor 1:18 inasema neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi(upupu) na kwa sisi tunaookolewa( tunaopona) ni nguvu ya Mungu.
 
Msishangae jamani. Yeye anaamini akikesha kanisani akiomba chakula kitajileta chenyewe! Mbona hujaganda huko tuone? Potelea mbali, ni vitu vingapi unatumia wewe vimetokana na hiyo miti shamba? Unajua aliyegundua nani alimwezesha?
 
huyu ndo kat ya wale wasabato masalia waliokuwa wanakesha uwanja wa ndge wakiamin watatokezea ulaya!
 
Hivi Musa alipofika kwenye yale maji yasiyonyweka aliambiwa afanye nini na Mungu?

Ngoja tukueleze ulelewe, MTI Ndio uhai na ukombozi wa mwanadamu, Zambi ya Kwanza ilianzia kwenye mti na ukombozi wa kweli unapatikana kwenye Mti,
Musa aliwaokoa watu wa Islaeli kutoka Misri kwa neema za Mungu huku akitumia Fimbo (Mti)
Nuhu aliwaokoa watu wake kwa kutengeneza safina iliyotengenezwa kwa miti,
Lutu alipokosa uzao watoto wake walimlewesha kutokana na divai, iliyotengenezwa kwa dhabibu (Mti)

NA ILI UKOMBOZI WA KWELI UPATIKANE MWANA WA ADAMU ILIMBIDI AANGIKWE MTINI (mSALABANI) AFE KIFO CHA LAANA, KAMA UKOMBOZI ULIKUWA NI LAZIMA YESU AFE KWA NINI HAKUFA KIFO KINGINE CHOCHOTE MPAKA AFE MTINI?

HUYO BABU ANGEKUWA ANAKWAMBIA NJOO NA KUKU MWEUSI UMWAGE DAMU HAPO NDIPO TUNGEKUWA NA WASIWASI, LAKINI KUNYWA MAJI YALIYOCHANGANYIKA NA MITI YUPO SAHIHI SANA

kwa kumalizia soma kitabu cha timoteo, "NA KWA MATATIZO YAKO YA TUMBO, USINYWE MAJI PEKEYAKE UNYWE NA MVINYO KIDOGO"
 
Ukiwa na imani utapona kama ambavyo wengi wametoa ushuhuda wao bali ambao imani yao ipo kama yako sio rahisi kupona maana kila kitu ni Imani ( Soma Math 8:5-13)
 
hivi musa alipofika kwenye yale maji yasiyonyweka aliambiwa afanye nini na mungu?

Ngoja tukueleze ulelewe, mti ndio uhai na ukombozi wa mwanadamu, zambi ya kwanza ilianzia kwenye mti na ukombozi wa kweli unapatikana kwenye mti,
musa aliwaokoa watu wa islaeli kutoka misri kwa neema za mungu huku akitumia fimbo (mti)
nuhu aliwaokoa watu wake kwa kutengeneza safina iliyotengenezwa kwa miti,
lutu alipokosa uzao watoto wake walimlewesha kutokana na divai, iliyotengenezwa kwa dhabibu (mti)

na ili ukombozi wa kweli upatikane mwana wa adamu ilimbidi aangikwe mtini (msalabani) afe kifo cha laana, kama ukombozi ulikuwa ni lazima yesu afe kwa nini hakufa kifo kingine chochote mpaka afe mtini?

Huyo babu angekuwa anakwambia njoo na kuku mweusi umwage damu hapo ndipo tungekuwa na wasiwasi, lakini kunywa maji yaliyochanganyika na miti yupo sahihi sana

kwa kumalizia soma kitabu cha timoteo, "na kwa matatizo yako ya tumbo, usinywe maji pekeyake unywe na mvinyo kidogo"

kumbuka mfalme naamani alinawishwa tope ..akapona..kulikuwa na majai angewezaomba anawe lakini kwa nini aambiwe tope,,same to mti babu kaonyeshwa mti..
 
Jina Jipya la Mungu wangu ni Yesu; aliyejulikana zamani kwa majina mengi kama Yehova Yire (Mungu mponyaji), Yehove Nisi (Mungu ndiye bendera ya ushindi wangu) Jehova Shalom (Mungu wa Amani) Alfa na Omega (Yeye ni mwanzo na pia Mwisho), alionekana kwa Musa kama Yuko ambaye Yuko na kwa Wana wa Israel kama Mungu wa baba yao Ibrahimu Isac na Yakobo....So ukiniuliza kuhusu huyo Babu alioteshwa na nani na kama ni mganga au mchungaji; I cant say much he knows better than I do for he is the owner of the dream/vision....Sijawahi kumwona kumsikia yeye kama individual anadai nini hivyo nadhani I have no right to rule out who he is and kwa jina gani anafanya hayo anayofanya...

Kwakukusaidia mimi sina dini na wala siamini katika yeyote I am a christian by faith na ukristo tafsiri yake ni Outward working of Divinity in Humanbeings...The power that worketh is that of Holly spirit of God/Jesus hayo mengine ya dini niwaachie wanazozimiliki am out!

Hahahaha, lugha uliyoongea i can bet a lot of people will not understand, ukisema huna dini watu wanatamani kuruka wasijue kuwa Mungu the creator of this world is not into dini.

The natural man will not understand the spiritual mysteries, they are perceived by the spirit.
 
hivi nikichukua hiki kikombe cha babu wa loliondo halafu nikamwagia kwenye nyumba yangu si umeme unaweza usikatike tena niishiwe na tatizo la mgao wa umeme?
 
Huwezi kumuwekea mipaka Mwenyezi Mungu katika utendaji wake kwani njia zake si njia zetu.
 
Huwezi kumuwekea mipaka Mwenyezi Mungu katika utendaji wake kwani njia zake si njia zetu.

na mawazo yake si mawazo yetu....hatufiki hata chembe ya ufahamu wake....binadamu tunapenda kujitia ujuaji sana....ndio maana tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Biblia unaijua vizuri wewe? Naaman hakupewa shart ili apone? Beba kitanda chako.. Si shart, amri za mungu si masharti ya mungu?, nenda zako...na usimwambie mtu habari ya kuponywa macho yako{ baada ya kupakwa tope la mate kwenye macho} si sharti? Singizia jingine lkn si biblia.
 
Habari Za wandugu wa JF,
Nimeamini kuwa kilichosemwa na BIBLIA hakitabadilika hata kama ni kwanini.

1.WATU HAWA WANAMACHO LAKINI HAWAONI, WANAMASIKIO LAKINI HAWASIKII.
2. WENGI WATAKUJA KWA JINA LA MUNGU.

Tusibabaishwe na mganga wa Loliondo ukweli hakuna Mungu wa namna hiyo yeye angetumia tu jina la Mganga wa kienyeji sio Mungu unajua ni kwanini?
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake swali: Watumishi wa Mungu Loliondo ni yeye peke yake? kama wengine wapo kwanini wasisaidiane? si kumpa tu mtu maji anakunywa??
b. Kwanini mti huo kama umefunuliwa na Mungu ukitumiwa na wengine usiponye?? Maana yake Mungu ameanza lini kutufundisha ubinafsi na uchoyo?

Nikomee hapa nitarudi! View attachment 24640

Radio Producer: Umesema Biblia, kama ukifuatilia vizuri mafundisho ya Yesu na uponyaji wake utaona kuna sehemu alikuwa anatumia vitu kama hata maji katika uponyaji. Mfano kipofu aliyeponywa. Imani ya mtu huwezi ihamishia kwa mtu mwingine. Mussa alipo waongoza wana waisraeli kutoka misri alifanya mengi ambayo sijaona mahari kwenye Biblia yakiludiwa na nabii yeyote yule. Kumbuka pia Eliya na manabii wa Baali. Mungu hufanya kazi kwa kutumia mkono wa mtu aliyemchagua. Kwa hiyo siri ya Babu wa Loliondo ni yeye na Mungu wake aliyempa hiyo kazi. Na kama unaamini siyo mkono wa Mungu huwezi kuthibitisha hapa kuwa na nguvu za giza.. Pia kumbuka madawa asilimia kubwa hapa duniani yanapatikana na miti shamba. Kwa hiyo kunywa dawa inayotokana na mti siyo vibaya labda umeipata kwa ramli. Croloquine inatokana na mti wa mquinine, na mengine mengi kaka. Acha Mungu amhukumu kutokana na matendo yake kwa naye ana nafsi kama mtu mwingine yeyote yule.
 
Wana Jf nivumilieni tu nimuulize huyu aliyepost kuhusu mganga wa loliondo kuweka masharti ya kutoa dawa mwenyewe, swali moja

NAAMANI JEMADARI WA JESHI LA WASHAMI ALIPOAMBIWA NA MTUMISHI WA MUNGU ELISHA KUWA AKAOGE MARA SABA MTO YORDAN HAPAKUWA NA MITO KWAO? HATA ELISHA ALIKUWA MGANGA WA KIENYEJI KUMPANGIA MASHARTI? (lazima aoge mara 7, mto Yordan?)

Wakina Tomaso wapo wengi..cjui ni wivu ama ni ubishi wa asili...achana nao
 
huyu nae anataka kukatisha watu tamaa,angekuwa na ngoma au kisukari mda huu angekuwa huko na asingeandika huu upuzi.kama watu wanapona acha atibu mbona kawapa wachungaji wengine hiyo dawa wamsaidie kuwapa watu kupunguza msongamano?
 
hivi nikichukua hiki kikombe cha babu wa loliondo halafu nikamwagia kwenye nyumba yangu si umeme unaweza usikatike tena niishiwe na tatizo la mgao wa umeme?

Kweli wewe ni sijui kitu...hukukosea kuchagua ID hiyo na you have proven that
 
1. Hakuna undani wowote... huo ni ukweli wa Tanzania... Ukweli usio na undani wowote uko wazi hadharani kabisa.

2 ...Undani wa watanzania ni waoga...hawawezi kuwakabili ..viongozi wazembe walioko madarakani... Watekeleze mambo yote wanayoahidi kwenye kampeni za uchaguzi...ie Afya nk
 
maana nina matatizo yangu nataka niyatatue na kuna wabaya wangu sinto jali kama wakawa vipofu.

Infact niko tayari kuwa meneja wake na inabidi dau lipande to laki moja haya mambo ya jero hatufiki

TRA sijui wako wapi...na serikali ikitaka kuingilia shughuli za huyu babu watachemsha ile mbaya kwani kila mtu kesha pagawa na the least liberty we enjoy ni hii ya babu


any ideas?


Ikishindikana conventional methods basi tukamhamishe atutibie mpaka tupone ndio tunamrudisha

I'm open for ideas maana sina interest ya kukaa kwenye ile foleni hata kidogo
 
Huyu ni wale ambao ukimwambia hii ni sumu hatoamini mpaka aionje
 
Back
Top Bottom