Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Mambo ya Msingi Sana katika maisha

ANOTHER ONE: Msaidie mtu mwenye shida kwa maana binadamu tumeumbwa kusaidiana, lakini yeye kuja kukusaidia hapo baadae ukishikwa na tatizo, sio guarantee/sio lazima. Unaweza ukamsaidia ila baadae akishafanikiwa, anaanza kukukwepa.

WAHENGA WALISEMA, TENDA WEMA NENDA ZAKO.
 
ANOTHER ONE: Ndugu/rafiki yako unayeshibana naye, akihama kutoka makazi A kwenda makazi B, Tenga siku moja uende ukapajue anapokaa. (Walau mara moja kwa mwaka)

Usisubirie mpaka siku akipata tatizo (ajali au msiba) ndio uanze kuuliza, hivi Alex anakaa Kibamba sehemu gani?? Sio poa..
 
ANOTHER ONE: Ukienda ugenini kusalimia, sasa ya kuondoka kama una coins shilingi mia mbili mbili au mia Tano, wape watoto wadogo uliowakuta pale, waambie kuwa "Hii uncle anakupa, utaenda kununua pili, sawa rafiki yangu ehh??"
 
ANOTHER ONE: Ukitumiwa Kadi ya mchango wa sherehe, na kama haupo vizuri financially, basi watumie 20,000/= tu kisha waambie kuwa "Hii pesa mtawekea mafuta katika gari la maharusi. Ninawatakia kila la kheri katika shughuli yenu"
 
Back
Top Bottom