Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Jitaidi ukiwa unakula au unatafuna kitu mdomoni ufunge mdomo ili kuzuia sauti ya kukera kwa wengine unaokula nao utafunapo huku unafungua mdomo.
Hahaaaa. Yupo bosi wetu miaka hiyo yaani ikitokea ukakaa naye karibu kantini utachokaaaaa. tena msomi hasa. Hata sasa nikimuona kwenye TV katika matukio kadhaa nawaza kwenye hizo hafla inakuwaje na wakuu wenzake.
 
Hahaaaa. Yupo bosi wetu miaka hiyo yaani ikitokea ukakaa naye karibu kantini utachokaaaaa. tena msomi hasa. Hata sasa nikimuona kwenye TV katika matukio kadhaa nawaza kwenye hizo hafla inakuwaje na wakuu wenzake.
Kama hajabadilika basi itakuwa ni aibu kubwa sana kwake..
 
ANOTHER ONE: Jitahidi sana usiwe na mwanamke wa ziada katika mtaa mmoja unapoishi na familia yako (mke na watoto). Kama utaamua kuwa na mwanamke wa ziada basi awe mbali na hapo mtaani kwako.

Respect your wife and children.
Kumbuka kwamba unamficha mkeo,lkn haumfichi mungu, ndugu acha kabisa zinaa ni mbaya,pia waweza ficha kwa watu lkn maradhi hayafichiki,kuna siku utayaleta ndani kwa mkeo???!
 
Namba nane hapo umenikumbusha tukio moja enzi hizo,jamaa fulani walimwona shemeji yao akiingia gesti na njemba,wakaamua kwenda kumwambia mwenye mali,eti waende nae gesti wafumanie na wakamwambia jamaa wao wataiadhibu njemba,lkn ye mwenye mke amfukuze kabisa uyo mkewe,kwakuwa kamtia haibu kubwa na kamdhalilisha,basi kufika guest wale jamaa wakatimiza Kwa upande wao dhidi ya ile njemba,
Lkn walishangaa mwenye mke wala akuchukua hatua alokua kahaidi,badala akamshika mkono mkewe na kumwambia hebu twende nyumbani shenzi sana,na baadae akawajibu wenzake awezi kulichoma shamba kwasababu yanguruwe mmoja,badala yake amemfukuza nguruwe full stop!!!,jamaa walimwona ovyo sana na kawahaibisha.
 
Kama rafiki yako amesafiri, usiende nyumbani kwake peke yako. Ukitaka kwenda, chukua watu wengine wawili wakusindikize.
 
1: Ukikuta mtu/watu wamekaa. Anayetakiwa kuanza kusalimia ni wewe uliyesimama

2: Ukienda sehemu. Anayetakiwa kuanza kusalimia ni wewe mgeni

3: Wakati wa mazungumzo ya kawaida. Msubiri mwenziyo amalize, na wewe ndiyo uongee. Wanaokatishana kauli ni wanaogambana

4: Mnapotembea kwenye njia nyembamba. Anayetakiwa kutangulia mbele ni mdogo kiumri.

5: Ni bora kuwa muuliza maswali kuliko kujifanya unajua kumbe hujui

6: Mazingira mengi ya kugombana na majirani zako ni mtego. Tumia busara nyakati za purukushani
 
Back
Top Bottom