Mambo ya Nje: Vita ya Ukraine isituingize mkenge

Mambo ya Nje: Vita ya Ukraine isituingize mkenge

Wewe inaelekea hujui kabisa hata chanzo cha vita hivyo.
Na hujui kuwa Ukraine na Warusi ni ndugu wenye asili moja.
Na hujui kuwa kati ya ndugu hawa wawili, Ukraine wamerubuniwa wajiunge NATO ili wampige ndugu yake Ukraine, Mrusi.
Na hujui kwamba Urusi anampiga mdogo wake Ukraine ili kumkomoa tu na kuikomoa NATO.

SASA mtoa posti wewe ndugu yako mweupe hapo nani?
Kaka Ukraine na Urusi walikuwa na asili ya pamoja miaka 1000 iliyopita. Tangu siku zile lugha na utamaduni zimekuwa tofauti. Hii ni kawaida kote duniani na kila taifa lina haki kuamua, au la?
Ukraine wana maarifa mabaya kuhusu Urusi hivyo waliamua uhuru na Urusi ilikubali ikafanya mkataba nao wakiahidi kuheshimu mipaka na uhuru wa Ukraine. Ahadi hiyo sasa imevunjika.
 
Kwenda Marekani hakuna maana ya ku compromise msimamo wa kutoingilia vita hii.
Na zaidi ya hspo Tanzania imeshasema mazungumzo ndio njia pekee ya kutatua mzozo huo.

"Tanzania imesema msimamo wake katika mgogoro kati ya Urusi na Ukraine ni pande zote kutafuta suluhu kwenye meza ya mazungumzo."

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema hayo akifanya mahojiano na chombo cha habari kutoka China.
Nyutro Kati kulia na Kati kushoto zote zetu ndo Mana tunakosa maendeleo unafiki kila eneo
 
Kaka Ukraine na Urusi walikuwa na asili ya pamoja miaka 1000 iliyopita. Tangu siku zile lugha na utamaduni zimekuwa tofauti. Hii ni kawaida kote duniani na kila taifa lina haki kuamua, au la?
Ukraine wana maarifa mabaya kuhusu Urusi hivyo waliamua uhuru na Urusi ilikubali ikafanya mkataba nao wakiahidi kuheshimu mipaka na uhuru wa Ukraine. Ahadi hiyo sasa imevunjika.
Naona huelewi ubabe hapo uliopo.
Ukraine inapigwa makonzi maana inataka kujiunga na adui wa Urusi, NATO.
Hivyo Urusi imeamua kumkong'ota Ukraine kabisa ili ijue moja.

Hawa watu hawangombanii mpaka wala mali, ni misimamo ya uadui.

Sasa wewe uko upande gani wa NATO maadui wa Urusi au Urusi yenyewe?

Ndio maana heri kuwa mbali na ugomvi huu.
 
Vita ya Ukraine na Urusi haituhusu waafrika, ni vita ya kwao Ulaya
Kiukweli tunawahurumia watu wa Ukraine kwa kuingizwa mkenge na nchi za magharibi.
Kwa hiyo mnatutaka tuunge mkono mauaji ya warusi wanayofanya kwa watu wa Ukraine?
Hivi Taifa moja kulivamia lingine na kusababisha uharibifu ule ni ubinadamu kweli?
Kisa eti walitusaidia kupigania uhuru? Hapana penye ukweli tuuseme jamani!
 
Mkuu sana sana ni kuwahurumia Ukraine, lakini huna la kufanya.
 
Waafrika Wengi Hatujitambui maana Tunawategemea Wao Vitu Vingi mpka Bajeti za Nchi zetu. Hapa Ni mpaka Muwe na Vyenu ndio Mtajitamba
 
Ushaambiwa urusi alitusaidia wakati wa ukombozi, kama sio urusi bibi yako angeendelea kuchapwa bakora na wakoloni/mabeberu.
Urusi haijawahi kusaidia nchi yetu kupata uhuru rudi shule akasome tena
 
Mrusi anatusaidia nini kwenye sekta za Afya, Elimu, Kilimo, Ustawi wa jamii au hata Technologia?

We go with someone who cares about Africa..at least.
.
Hakuna shirika la misaada la Urusi!!! AFRICA nzima

Mrusi kazi yake kuuza mabomu tu na mabunduki hatoi misaada ya elimu,afya nk
 
Naona huelewi ubabe hapo uliopo.
Ukraine inapigwa makonzi maana inataka kujiunga na adui wa Urusi, NATO.
Hivyo Urusi imeamua kumkong'ota Ukraine kabisa ili ijue moja.

Hawa watu hawangombanii mpaka wala mali, ni misimamo ya uadui.

Sasa wewe uko upande gani wa NATO maadui wa Urusi au Urusi yenyewe?

Ndio maana heri kuwa mbali na ugomvi huu.
Nilishangaa tu, ukijisikia uko mbalio na unataka kuwa mbali na mgogoro huo, kwa nini unarudia propaganda ya Kirusi neno kwa neno?
Sawa, ukae mbali, lakini usifiche kwamba ni jaribio la kurudisha ukoloni kwa nchi iliyoamua kwa kura huru (miaka baada ya 2014) kuendelea kama taifa huru na kujitegemea...
 
Msimamo wa Urusi unaeleweka vizuri.
Mtoto wako akiamua kuungana na jambazi , unamshughulikia mtoto kwanza, jambazi baadaye.
 
Msimamo wa Urusi unaeleweka vizuri.
Mtoto wako akiamua kuungana na jambazi , unamshughulikia mtoto kwanza, jambazi baadaye.
Mzee, kwanza Ukraine si mtoto wa Urusi, labda usome historia yako tena.
Lugha hii ya baba na mtoto ni bure kati ya mataifa.
Unaonaje kama Mjerumani au Mwingereza anakuja kuchapa mtoto wake Tanzania? (maanake mipaka iliyopo iliamuliwa 100% na hao, Nyerere aliunganisha vipande viwili tu vilivyoamuliwa awali).

Tena NATO si mjambazi, ni ushirikiano uliooundwa si kwa shabaha ya kuvamia Urusi, bali wa kuteteana dhidi ya vamizi wa Urusi jinsi zilivyotokea kuanzia 1945 mwaka kwa mwaka.
Kwa nini unadhani watu wa Finland wanaamua ghafla kujiunga nayo NATO? Kwa sababu wanaona kiongozi wa Urusi hajali mapatano wala mikatab a, anatafuta ukoloni mpya tu bila kujali mapatano yoyote.
 
Tayari mama anaenda America marekani ushauri wako umechelewa
Akiwa huko lazima ashinikizwe kuilaani Urusi!! Atakuwa na wakati mgumu sana kujieleza kwa nini Tanzania ili-abstain kwenye kura ya kuitoa Urusi kwenye time ya haki za binafsmu ya umoja wa mataifa!
 
Back
Top Bottom