Mambo ya Nje: Vita ya Ukraine isituingize mkenge

Hali si hali. Hata kibaraka wa marekani kwa miaka mingi saudia this time kamgomea.

Nasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi Ufaransa trh 24. Le pen kaweka wazi, akishinda hakuna vikwazo kwa russia kwenye mafuta na gesi.
Bahati mbaya sana chance ya kushinda kwake ni kidogo.
 
Analogy ya baba na mwana na jambazi ni mahala pake kabisa.
Na kama huelewi holo basi na kuelewa kwa nini Urusi inampiga Ukraine itakuwa vigumu sana kwako kuelewa.
WWIII karibia itokee 1962 katika Cuban Missile Crisis, wakati Urusi ilitaka kufanya kile kile ambacho Wamarekani walitaka kufanya Uraine.

Cuba kwa uhuru wake na sovereighnity, iliomba na kukubaliwa na Urusi kuweka makombora mazito kilometa 90 toka Marekani.
Marekani ikapinga “jirani” na ndugu yake( kama Ukraine) kupokea makombora hayo na ikapiga mtiti wa nguvu kuipiga mabomu Cuba na hata Urusi kama wameendelea na mpango huo.
Urusi ikakubali yaishe na kurudisha makombora yake.

Pengine ninyi wengine mlikiwa hamjazaliwa

Leo kinatokea kile kile in reverse, hamuyaoni wala hamuelewi.
Kueni muyaone.
 
Tafadhali ujelimishe angalau kidogo kabla ya kuendelea.
1. Urusi ilipeleka makombora Kuba, hakuna aliyepeleka makombora Ukraine
2. Urusi ilileta wanajeshi Kuba, hakuna wanajeshi wa NATO Ukraine. (Kinyume Ukraine ilikabidhi silaha zake kalio kwa Urusi kwa hiari yake!)
3. Marekani ilidai Warusi waondoke, waliondoka, hakuna aliyevamia Kuba baadaye.
4. Urusi alivamia Ukraine wakati hakuna kombora ya NATO wala mwanajeshi wa NATO nchini.-
5. Marekani ilichukia lakini ilivumilia ushirikiano wa Kuba na Urusi baadaye
6. Urusi inadai eti ina haki ya kuamulia Ukraine ishirikiane na nani...

Kusoma Propaganda mno kunaathiri uwezo wa kutumia akili, naona. Sivyo?
 
1. NATO ilikuwa na mpango wa kupeleka silaha Ukraine, ikijiunga tu na NATO
2. Nchi za NATO zimepeleka “washauri” wengi tu Ukraine. Inategemea wewe unaelewa nini by washauri.
3. Urusi imeshauri Ukrane asijiingize NATO, amekaidi
4. Refer2 above
5. Hata hueleweki, ushirikiano na Venezuela vipi?
6. Kina Ortega, Allende walikula joto ya jiwe, na nchi nyingi za South America peleka mishale yako na umwone Uncle Sam.

Its shocking vijana wa leo mko empty headed in international issues.
 
Mbona unaleta madai matupu, ilahali huna cha kuonyesha.
1. Hapakuwa na mpango wowote kupeleka silaha za kishambulizi Ukraine. NATO imekataa ombi la Ukraine kujiunga tangu 2008. Ukisai kinyume, lete ushahidi. -
2. hadi sasa hata hakuna silaha za mashambulizi zilizopelekwa katika nchi nyingine za NATO katika Ulaya mashariki (zulizokuwa nusukoloni za Urusi hadi 1991)
3. Idadi ndogo wa washauri na walimu waliwahi kufika UKraine, wote waliondoka kabla ya uvamizi. Hakuna vikosi vya NATO UKRAINE.
4. Ulileta KUBA, nilikujibu, unashindwa kuleta chochote sana unaanza stori za Venezuela au mapinduzi ya kijeshi (si uvamizi wa Marekani) huko Chile.

Hapakuwa na silaha yoyote ya kishambulizi ya NATO UKraine, hapakuwa na mpango wa kuleta, Urusi inavamia kwa sababu inataka kurudisha ukoloni wake.
Na wewe ilhali huna cha kujibu, unaanza matusi. Hongera sana!
 
Mkuu ukishalishwa peremende za Washington, si rahisi kuona upande mwingine.
Tutabishana mpaka asubuhi na hatutafikia muafaka.
Ndio maana nilisema huko nyuma we should mind our own business and the West should mind theirs.
Nimeweka clip ya India ili ikugutue akili, wengine wanaivyoiona dunia.
 
kweli huna cha kuonyesha, tuache.
 
Nilitahadharisha wiki iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani kutinga Dar karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…