Hao wanawake wa kwenye mabar na clubs ndio hao hao ambao angeweza kukutana nao hata makanisani na masokoni, hivyo basi bado sampling yake iko accurate kufanya interpretation na conclusion sahihi..Mkisoma maelezo yangu vizuri mtaelewa maana yangu, kwanza ni kitendo cha kuwajumuisha wanawake wote wa KITANZANIA wakati yeye amekutana na WADANGAJI wa DAR na ZNZ,
Hayo yote aliyoyaongelea ni aina ya wanawake alokutana nao barabarani na kwenye bars na clubs alipaswa aainishe hayo kwenye maelezo yake badala ya kujumuisha wote,
Yangesemwa na mtanzania hasa mwanaume isingekuwa habari ndio kwa sababu huyo mwanaume angeishia tu kukejeriwa na kuambiwa atafute pesa tena na hao hao wadangaji.. maneno hayo kusemwa na mzungu ni jambo zuri sana maana yana uzito na pengine madada wa kibongo watashikwa na aibu na hatimae wataondokana na mindset ya kidangaji na kugundua kwamba mahusiano sio njia ya kuikimbia umskini, bali umaskini unakimbiwa kwa juhudi na maarifa katika kazi.Pili hayo maneno akiyasema mtanzania kwenda kwa mtanzania mwenzake sio habari ila kuyasema mzungu kwenda kwa Watanzania ndio habari ilipo
Kwa hiyo angesema hayo kama tabia za wanawake wa kiafrika kwa ujumla ndio usingeumia ila umeumia alivyoitaja tanzania specifically sio? Watu kama wewe hata shuleni mkifeli darasa zima unaona ni sherehe ila ukifeli peke yako ndio kilio, such an obnoxious loser's mindset.Tatu yooooote aliyoyasema yapo kwenye nchi zote za Kiafrica na nchi zingine maskini kwanini iwe TANZANIA tu?
Anawaogopesha kivipi? Kwa kuwasanua wazungu wenzake kuhusu kasumba za wanawake wa kitanzania au? Na kwa taarifa yako alichokifanya huyu mzungu kwenye hii video ndio amewasaidia sasa.. maana mzungu yeyote ambaye ana mpango wa kuja kutafuta mwanamke hapa Tanzania, baada ya kuangalia video hiyo atakuja huku amejiandaa kisaikolojia kabisa kwamba anakutana na wanawake wa aina gani, hivyo atakuja anajua kabisa itabidi awe tayari kusaidia ndugu wa mwanamke atakayeingia nae kwenye mahusiano, atakuwa tayari kubeba bills zote yeye peke yake maana pesa yake itakuwa ni ya wote na pesa ya mwanamke ni ya kwake peke yake.. na zaidi ya yote atakuwa tayari kuishi na mwanamke ambaye hana cha kuoffer kingine zaidi ya uchi alionao.Nne hamuoni kama anawaogopesha wageni wenye matarajio ya kupata wenza wa maisha Tanzania kwa huo mjumuisho wake wa hao wanawake wadangaji na wanaume machawa anaokutana nao?
Kwa ufupi tu hii video imewasaidia sio tu wazungu wenzake bali hata madada wa kibongo kwenye suala zima la hook up/dating tofauti na unavyofikiri.