Mamlaka husika zimzuie Rais Samia: Nchi yetu inaelekea wapi?

Mamlaka husika zimzuie Rais Samia: Nchi yetu inaelekea wapi?

Ndugu zangu Watanganyika mliopo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na wale mnaomshauri rais Samia hebu msaidieni asidanganywe na walaghai wenye nia ovu.

Baada ya hapo fanyeni haraka kurudisha umiliki wa eneo la Ngorongoro, KIA na bandari zetu. Pia mchakato wa kuchimba madini kwenye hifadhi na maeneo nyeti usitishwe kwanza.

Ndugu zangu watanganyika kuna leo na Kesho, hakikisheni hamfanyi mambo yatakayofanya vizazi vijavyo vitulaumu.

Nyie ni mashahidi kuwa chifu Mangungo wa Msovero anatukanwa na kudharauliwa mpaka leo kwa kutokuwa makini na kusaini mikataba ya hovyo.

Hili lisijirudie jamani.

Asanteni, nawatakia utekelezaji mwema.
Mchawi wa kutokea kwa madhila yote haya ni Katiba Mbovu tuliyonayo.
Wananchi wa Tz kamwe hawataweza kupata utulivu wa mwili na akili hadi hapo wao wenyewe kwa wingi wao watakapoamua kujitungia Katiba yao itakayotokana na fikra na mawazo yao wao wenyewe.
 
1. Nyerere alijua anatuachia katiba mbovu lakini bado akakubali tu kuiacha wakati alikuwa na uwezo wa kusababisha ibadilishwe.

2. Wakati vyama vingi vinaanzishwa Nyerere alijua ccm wamejimilikisha maeneo ya umma na majengo yaliyojengwa na Watz wote bila kujali vyama lakini bado aliona sawa na kuwaacha ccm kupora mali za umma bila kuchukuliwa hatua

3. Muungano tulionao niwa kwake Nyerere na Karume. Haukuwahi kuridhiwa na wananchi. Nyerere pamoja na kujua kuwa Tanganyika imepoteza kila kitu aliacha tu huu muungano uendelee kuwepo ili malengo yake ya kisiasa yatimie

Nyerere hawezi kukwepa hizi lawama ndiyo maana Lissu anamlaumu

1. Nyerere hakujua wahuni hawakuwa watu wazuri.

2. Mama Mgaya alikuwa kaishi miaka 100+ pamoja na suluba zote za maisha alizopitia.

3. Kumbuka alisema angemwona hadi rais wetu wa 5 labda agongwe na lori.

4. Akidhani angekuwapo, hivyo hakuna asingeweza kutommudu.

5. Akiwapo haipo shaka si msoga, jiwe au chura kiziwi wangetia timu magogoni.

6. Ama kweli wahuni si watu wazuri!
 
Ndugu zangu Watanganyika mliopo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na wale mnaomshauri rais Samia hebu msaidieni asidanganywe na walaghai wenye nia ovu.

Baada ya hapo fanyeni haraka kurudisha umiliki wa eneo la Ngorongoro, KIA na bandari zetu. Pia mchakato wa kuchimba madini kwenye hifadhi na maeneo nyeti usitishwe kwanza.

Ndugu zangu watanganyika kuna leo na Kesho, hakikisheni hamfanyi mambo yatakayofanya vizazi vijavyo vitulaumu.

Nyie ni mashahidi kuwa chifu Mangungo wa Msovero anatukanwa na kudharauliwa mpaka leo kwa kutokuwa makini na kusaini mikataba ya hovyo.

Hili lisijirudie jamani.

Asanteni, nawatakia utekelezaji mwema.

Hakuna mamlaka ya kumzuia zaidi yetu sisi wenyewe.

Tatizo ni kuwa tunapenda mno kuvuna tusipopanda, hivyo tungependa wawepo wa kutukombolea nchi.
 
Back
Top Bottom