Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Jukwaa mbona tunalipata jamani.Mwendo wa VPN tu.
nimecheka kwamba kumbe viongozi huwa wanatupia vpn kimya kimya kama sisi
 

Attachments

  • Screenshot_20250906_115008_Lite.jpg
    Screenshot_20250906_115008_Lite.jpg
    647.6 KB · Views: 25
Kwani Picha nani kuvujisha? Hakukuwepo waliopatikana ikulu wakati wa ule mkumbatio hatukuwepo kwanini tuhukumiwe kwa kupata hizo taarifa?

Dah! Sasa Polepole tutapata wapi taarifa zake?
 
Lilifungiwa 2018 wiki 3 hana usafi wowote huyo mtu.

He was the hallmark of all these gimmicks.
Nini kinawazuia kuyasahihisha ikiwa sasa hayupo na ndio yamezidi mara dufu? usafi anao, angalau alitetea rasilimali zisichukuliwe kijinga na kizembe!
 
Hii nchi bwana, sasa kwanini wao hawaja jitokeza na kuthibitisha hizo tuhuma alizo toa pole pole kuwa sio za kweli ni uzushi tu.
Lengo lao naona wanataka vyombo vyote vya habari waogope kurusha habari za Polepole na habari zote zinazoweka wazi uozo uliopo ndani ya serikali. Wanawatisha wajiwekee self censorship.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
Tupo na vpn tunatamba duniani
 
Naunga mkono hoja, haiwezekani jukwaa litumike Kwa maslahi ya vikundi au watu badala ya Umma.

Pole sana ila sheria zifuatwe.

Nawashauri TCRA wangefungia jukwaa la siasa na mengine ambayo yanaandika siasa ,then Yale mengine yasalie na wamiliki wadhibiti maudhui y Kisiasa kwenye majukwaa yasiyo ya siasa.
Acha uchoko wewe pimbi hamtaki msemwe mbwa nyie
 
Nadhani ni zile picha za mama Abdul akikumbatiana na yule raia fisadi wa Zimbabwe,nilijua hapa lazima kiumane,

Hatuna amani tena
Kwani zile picha si zimepigwa na watu wa ikulu wenyewe jamani au ? Huku Jf zimekuja kujadiliwa tu 😂😂
Source ya hizo picha ni web ipi mkuu yan wa mwanzo kuzipublish ?
 
Back
Top Bottom