A
Anonymous
Guest
Kero yangu ni walichotufanyia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (Tanzania Airports Authority – TAA) vijana 40 kutoka JKT 2024 OP Mabeyo, walituchukua tukiwa vikosini wakatupeleka kama Maafisa Usalama wa Viwanja vya Ndege, Airport Security Officer (AVSEC) bila kuomba nafasi hiyo, wakatushawishi kuwa tusahau kuhusu fursa za majeshi na kwa sasa tutafanya kazi TAA kwa muda na baadaye watatuajiri kabisa.
Nanukuu "Tuna shortage ya security officer zaidi ya 600" kwa hiyo baada ya mkataba huu wa mwaka mmoja tutawaajiri kwa kuwa ni sekta ya serikali na ni nyeti, hatukuhoji na isitoshe tumepelekwa na jeshi na malezi na maelekezo hatukuwa na haja ya kuleta sinto fahamu.
Tulitumikia mamlaka kwa mwaka mmoja na miezi sita yaani 2024 January hadi Mei 2025. Baada ya hapo walitutumia barua katika vituo vyeti vya kazi Airports, kwa kusema kuwa mamlaka haina nia ya kutuajiri kwa kuwa tuna elimu za juu zaidi yaani degree, yaani waliobakizwa ni wenye diploma.
Tulijaribu kwenda sehemu mbalimbal kuomba msaada hatujapata hadi leo.
Tumepishana na fursa nyingi baada ya kuaminishwa tumeshaajiriwa na kwa kuwa mamlaka zilizo kuwa zikitusimamia ni nyeti kwa hiyo hatukuwa na shaka juu ya ahadi zao hata kama zilikuwa ni za mdomo.
Mwaka mmoja na miezi sita kama watumishi wa mamlaka imesabanisha kupoteza fursa nyingi za ajira hasa katika majeshi tukiamini tumefika pia vigezo viliendelea kututupa mkono kwa umri pia ukizingatia elimu zetu ni za juu.
Tunahitaji taarifa ifike kwa number moja au mkuu wa wizara ya uchukuzi ili tuweze pata haki yetu yakurudishwa kazini na kupewa kipaumbele cha ajira.
Tumeitumikia nchi kwa uzalendo, kuanzia JKT kwa kujitolea napaka huko mamlaka, tunajihisi kutelekezwa mtaani na kiukweli wame tupa msongo wa mawazo sana.