Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Man United: Kipigo, Matumaini Yanayoyeyuka, na Mvumo wa Mashaka
Usiku wa Desemba 30, 2024, Old Trafford, uwanja uliojaa kumbukumbu za ushindi wa kihistoria ukageuka kuwa kaburi la matumaini ya mashabiki wa Manchester United.
Sauti za shangwe zilizokuwa zinaashiria imani ya mashabiki zilidhoofika, na kuzimwa kabisa baada ya kipenga cha mwisho.
Newcastle United walitembea kwa ushindi wa mabao 2-0, wakiacha wingu zito kwa Man United.
United, Mabingwa wa enzi, sasa wanaingia mwaka mpya wakiwa kwenye nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Wakiwa na alama 19 baada ya mechi 17, tofauti ya alama 7 tu inawatenganisha na timu zilizo hatarini kushuka daraja.
Hakuna tena miujiza kubadili matokeo ya "Fergie Time." Hakuna tena wachezaji kama Cantona, Ronaldo au Rooney kuokoa timu.
Timu inaenda kwa kasi kwenye hadhi za timu ndogo za EPL. Ni habari mbaya. Jitihada nyingi zimefanyika ili kunusuru timu, lakini bado inazama.
Ni msimu wa giza, msimu ambao historia inapigwa kikumbo na hali halisi isiyosameheka.
Ova