Muathirika wa mafundisho potofu huyu hapa.
Hata biblia hujui mnabugizwa matango pori tu.
Kuna tofauti kubwa ya mtu kuitwa nabii na unabii.
1. Unaweza kutoa unabii na usiwe nabii.
Rejea Sauli alipotoka kupakwa mafuta na Samweli, alipofika njiani, alikutana na wana wa manabii...akatabiri lakini hakuwa nabii.
2. Kibiblia ili uitwe nabii sio mafundisho, sio kutabiri wala sio kuponya bali ni suala la muda...utabiri mambo na yatokee..
MALISA WAKO ametabiri nini kimkoa, kitaifa au kijamii kikatukia?
3. Kuna kitu kinaitwa neno la maarifa, kinaweza kufanana na unabii lkn sio.
Hii ikoje?
Inatokea unapokuwa unahubiri au kuombea...utahisi hali ya mtu mwenye tatizo...mfano kuumwa kichwa sana upande mmoja.
Ndio maana kanisanisani utasikia mchungaji anasema...kuna mtu anaumwa na kichwa upande wa kushoto na kweli anatokea.
Huu sio unabii bali neno la maarifa.
Huwezi kunielewa ewe kipofu wa rohoni.
Mtatumikishwa na manabii fake hadi mchakae.
Note: utajiri haupatikani kwa maombi wala unabii...ingekuwa hivyo tungekuwa na mabilionea Tanzania.
binti kiziwi