#COVID19 Maneno ya Askofu Gwajima yamepata nguvu, kitaa wanaamini wakubwa wamehongwa


Huo ndio ukweli mkuu achana na hawa wapiga kelele ambao wapo mtandaoni porojo nyingi chanjo chanjo na hawaendi kuchanjwa

Nenda mtaani fanya research watu hawataki chanjo na hawatachanja.
 
Mkuu sio 90% ni zaidi ya 98%, mpaka Sasa sijaona mtu aliye tayari kuchanjwa nikihoji mtaani. Wote unawakuta huku mitandaoni walio tayari kuchanjwa. Mtaani watu wengi wanapingana na chanjo vibaya sana.
 
Hiyo chanjo yenyewe wengi hawana vigezo vya kuipata. Kelele nyingi wakati hamna vigezo vya kuipata
 
Mkuu sio 90% ni zaidi ya 98%, mpaka Sasa sijaona mtu aliye tayari kuchanjwa nikihoji mtaani. Wote unawakuta huku mitandaoni walio tayari kuchanjwa. Mtaani watu wengi wanapingana na chanjo vibaya sana.

Kabisa mkuu hakuna aliyeko tayari watu wanajifariji tu mitandaoni ila mtaani hali ni tofauti sana
 
Tangu huu ugonjwa umeingia kuna phase 1 mpaka 3 je Watanzania wamekufa kwa malaki kama USA? Kama tupo na tunadunda kkoo tutaendelea kuishi na legacy tuliyoachiwa
Huyo aliye kuachia ligasi amekufa kwa ugonjwa gani tena? Sio huo nasemea ule wenyewe ule!!
 
Mkuu sio 90% ni zaidi ya 98%, mpaka Sasa sijaona mtu aliye tayari kuchanjwa nikihoji mtaani. Wote unawakuta huku mitandaoni walio tayari kuchanjwa. Mtaani watu wengi wanapingana na chanjo vibaya sana.
Hata wakitaka kuchanjwa hawatachanjwa. Chanjo si za kila mtu
 
Mkuu tafiti zipo, tumia Google kupata taarifa hizo.
Sasa Kama wasomi wenyewe ndo nyinyi ambao mnategemea Google ndo iwafanyie tafiti ,nynyi mkopi vya Google ndo mje mjimwambafai kwa Wana nchi kwamba kaangalieni Google tafiti zipo.shain zenu.basi hata Chimpanzee ana akili nyingi kuliko wasomi hawa ,maana wao hawaamini mpaka wajiridhishe wenyewe !! Watu wanauliza maswali ya msingi mnakosa majibu !! shain kabisa!!!,
 
Waambie comedy ya kwenye TV haitawaokoa,watajuta Kula vya beberu.
 
Shain ndo nini mkuu? Bora utumie Kiswahili tu. Nimekujibu utumie google sababu mtu unayejua kutumia internet na kuingia jamii forum hushindwi kupata takwimu hizo unazoziulizia hapo juu kutoka kwenye vyanzo vinavoaminika ndani ya google search. Zaidi ya hapo unataka kubishana tu.
 
Kuna watanzania hawajitambui kabisa. Huyu Gwajima(askofu) amekwisha toa kauli tata kibao. Ahadi kibao ambazo hajatekeleza...lakini bado kuna watu wanamwamini. Sijui tumelogwa? How comes,we behave this way?
Wewe mwenye kujitambua hebu tuambie long term na short term side effects za hiyo chanjo.

Na tuambie kwanini chanjo zingine Kama pepo punda,tetanus, surua nk,huwa hatujazi consent form?
 
Viongozi wajitokeze wapangue kuanzia hoja za Magufuli maana ndo walimwamini zaidi,na alidai chanjo Zina madhara.
Halafu wajibu za Gwajima kuliko kurukia conclusion tu eti anapotosha.
Kinachoshangaza hawa wote walikuwepo wakati wa Magufuli alipokuwa anazungumzia mapapai, chanjo na sikumsikia yeyote kudai anawavuruga wananchi, hizi mbinu zinanikumbusha kisa cha aliyekuwa mkurugenzi wa NIMR alipodai kuna ugonjwa sijui Ziggy(nimesahau jina) wakati huo ugonjwa haupo na lengo lake alambe pesa ya mabeberu, mwendazake akamtimua, na hatukuusikia tena au kuona madhara ya huo ugonjwa hapa nchini, pia akaja binti mwingine nae akaanza janja akatolewa. Kifupi hizi pesa za ufadhili za mabeberu zitatumaliza, UVIKO 19 ni tofauti na UKIMWI kwa hiyo tujihadhari na hizi chanjo, kila mtu aamue kivyake na si viongozi wa serikali au wa dini ndio watuamulie, hizi nguvu nyingi zinazotumika kubishana zina haribu malengo yetu, miluzi mingi hupoteza timing ya dog anapokuwa mawindoni.
 
Acha wavune walichopanda, mamba wamemlea wenyewe sasa ameanza kuwatafuna,ameanza na mkuu kwa kuvuta mguu
 
Pesa za mateso yaani mtu anajitoa ufahamu kuwafurahisha mabeberu,huku nafsi zikiwasuta.
 
Mamlaka tayari zimeonesha hali ya kushindwa kueleza umuhinu na usalama wa chanjo, kuwarudisha wanainchi kwenye mstari itachukua muda. Jambo la kijiuliza kama kuna maelezo toshelevu na yenye ukweli kwanini wanainchi wayafuate maelezo batili?

Tunalo jambo la kujifunza hapa aidha kuna mahali hatuko sawa sawa.
 

Tatizo ni U-Turn iliyopigwa mkuu, miezi michache ilyopita tuliambiwa hakuna korona Tanzania na tumeshaishinda, tukaambiwa ni propaganda za mabeberu kutumaliza mbali zaidi na barakoa zikadhihakiwa tukaambiwa nj kama vifuniko vya matiti (sidiria), tukakatazwa kuzivaa, tukaambiwa tupige nyungu.

Kiongozi mkuu wa nchi na serikali alituaminisha yote hayo, waziri wa afya alitumbuliwa kusimamia Sayansi juu ya korona, Waziri mpya akaja ambaye yupo mpaka sasa na ambaye ni daktari kitaaluma akaacha taaluma akatwambia tuongee nyungu, tusali na tuachane nanpropaganda za mabeberu. Mawaziri, wabunge CCM na wataalamu wote wakwatwambia tumeishinda korona wanaanchi tukaamini tukapuuzia na tukaendelea na maisha.

Tukaamini yote tuliombiwa na viongozi na tukawa na imani tumeshinda sasa walewale wanakuja kutuambia tofauti hapa ndio tatizo.

Sasa watumie nguvu na ushawishi ule ule kutuaminisha hatujaishinda korona, inatumaliza na tunahitaji kufanya wanayosema sasa hivi.
 
Ulikuwa ni msimamo wa hayati JPM....


#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#KaziIendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…