Asante kwa taarifa, sio kila data wanayomfidi kidada ni kweli, hivyo msiamini kila anachosema!, tumieni a common sense logic to determine the facts.
- Ni muda mrefu nchi yetu haijachapisha new bank notes, nq noti zinachakaa, sasa ni wakati muafaka kuchapisha noti mpya za saint ya Mwigulu.
- Siku zote note mpya zikiletwa, zinaletwa kwenye ma container na makontena clearing inafanyika usiku, kunakuwa na ulinzi wa ajabu toka bandarini mpaka BOT.
- Uchapishaji is a long process and takes time, sii kweli kuwa noti mpya zimechapishwa kwa ajili ya uchaguzi.
- Kwa vile mimi ni mwandishi, nitawawekee ni links za mchakato wa noti mpya, ni kiasi gani, ni kampuni gani zimechapisha, kutoka nchi gani, pia najua ni container ngapi, zinaletwa na meli gani na lini lakini vingine sisemi kiusalama na kiuzalendo
- P
Haha Mayalla bhana, sijui unaongea haya kwa maslai ya nani, anyway ngoja nkujibu:
Unacho zungumza ww na mada iliyopo ni tofauti, wewe unazungumzia utaratibu wa kuchapisha, kuingiza hizo fedha nchini kutoka kwa waliogewa tenda yakuchapisha nje nchi. Taarifa haimaanishi anaye print ni BOT, Nchi nyingi afrika zimewapa wakandarasi nje kufanya hivyo, ila utasikia wanasema nchi fulani imechapisha pesa na kuingiza kwa mzunguko hata kama zinachapishwa nje.
Hao wanaogewa tenda hiyo, kazi yao ni kuchapisha na usafirishaji tu na sio kuangalia au kujua uchumi wenu ukoje ndo wachapishe, wao wanafuata order iliyotoka kwa mteja kama mtu anavyonunua bidhaa viwandani.
Kinachozungumzwa ni uchapishaj na kuingizwa pesa kwenye mzunguko bila kuzingatia dynamics za uchumi (monetary policy decisions).
uliowapa hyo tenda kazi yao ni uchapishaji kulingana na order uliyowapa, ila anayecontrol hizo pesa ili kubalance dynamics za uchumi (price stability na economic balance) ndani ya nchi ni BOT ili kulinda uchumi wa ndani na kuzuia mfumuko wa bei, kama umechapisha makontena na makontena, zikafika Tanzania, na ukaziruhusu pesa nyingi ziingie mtaani bila kuangalia uhalisia wa uchumi (inflation rate, GDP growth, Interest rates, foreign exchange reserves etc) inaenda kusababisha mfumuko wa bei mtaani (inflation rate skyrocketing).
Kwahyo kinachozungumzwa ni kuchapisha pesa, na wanaziingiza kwenye mzunguko bila kuzingatia hayo niliyosema. Na BOT uwa wanakuwa na notes mpya zimekaa kwenye vault, pale factors za uchumi zikiruhusu wanaingiza pesa mtaani kwa kadri inavyotakiwa na sio kuzimwaga tu.
Pia sio pesa inahitajika mtaani ndo wanatoa order ya kuprint hapana, zinakuwa tayari zipo kwenye vault, hvyo inawezekana zilikuwa zishachapishwa hata kabla ya uchaguzi maana zinaingizwa kwa batch na kuhifadhiwa kwenye vault, na kutolewa kidogo kidogo Labda kubadilisha zilizochoka au kuchangamsha uchumi (economic stimulus) n.k
Tatizo: Ni kuingiza hizo pesa kwenye mzunguko kupitia matumizi ya serikali ikiwemo uchaguzi bila kufuata utaratibu ni hatari mno, hutoona ndani ya mwezi mmoja au miwili, ila chuma kitaitika, I guarantee you kama hii ni kweli. Numbers never lie.