Ni wazo zuri sana!
Najua kufa kunaogopesha, lakini ukweli ni kwamba bila watu kujitoa mhanga, mabadiliko ya kweli hayatapatikana.
Watu wamepigana vita ili wawe huru.
Anzia kwenye vita vya mapinduzi vya Marekani kujitoa kwenye ufalme wa Uingereza.
Njoo kwenye vita vya May Mau hapo Kenya.
Zunguka Afrika nzima kwenye harakati za ukombozi.
Hapo Afrika Kusini walikufa watu wengi ili watu weusi wapate haki zao.
Chris Hani aliuliwa mbele ya binti yake kisa alikuwa mstari wa mbele kupigania haki na uhuru ambao watu wote wanao huko Afrika Kusini leo.
Medgar Evers, Martin Luther King Jr., na wengineo huko Marekani waliuliwa kisa walikuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za watu wote.
Evers na Dr. King walikuwa ni wasomi ambao wangeweza kuachana na harakati zao za kudai haki kwa wote na kuishi maisha yao bila bugudha lakini hawakufanya hivyo.
Historia imeshaonyesha kwamba haki kwa wote huwa hazitolewi kwa hiari na waliopo madarakani. Ni lazima zidaiwe kwa njia na namna zozote zile zilizo za lazima.
Bila ya sisi kubadili fikra zetu na kuachana na uoga, kamwe hatutapata mabadiliko tunayoyataka.