Mange Kimambi na Kauli ya 'No Reforms, No Election': Je Vijana wa Instagram Wanaamka Kisiasa?

Mange Kimambi na Kauli ya 'No Reforms, No Election': Je Vijana wa Instagram Wanaamka Kisiasa?

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,910
Reaction score
4,711
Katika hali ya kushangaza, kauli mbiu ya "No Reforms, No Election" inachipuka kwa kasi kubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, jukwaa ambalo lilizoea kudharauliwa na wachambuzi wa kisiasa kama sehemu ya "wajinga", wasiojali siasa wala mustakabali wa taifa. Instagram, mtandao wa picha, hadithi za maisha ya watu mashuhuri, umbea na burudani, sasa unageuka kuwa uwanja wa mijadala mikali ya kimageuzi (No reforms No election).

Moja ya sababu ya kilichoibua hali hii ni uamuzi wa ghafla wa Mange Kimambi, mwanaharakati na mwanachama wa zamani wa CCM, kuacha maudhui ya burudani na kuingia rasmi kwenye kampeni ya kisiasa kupitia kauli mbiu hiyo maarufu. Mange, ambaye kwa muda mrefu amekuwa na ushawishi mkubwa kwenye Instagram, hasa kwa vijana na wanawake, ametumia nguvu ya jukwaa lake kuhamasisha Watanzania kuhoji mchakato wa uchaguzi unaokuja, akisisitiza kwamba uchaguzi usifanyike bila mabadiliko ya msingi ya kisiasa na kisheria.

Mabadiliko haya ya ghafla yanachambuliwa vema kupitia lenzi ya 'sayansi ya jamii' na 'usanifu wa kijamii' (social engineering). Mange hakubadilisha sura yake wala namna yake ya kuwasiliana, ameendelea kutumia lugha rahisi ya mtaa, video za moja kwa moja, na posti zenye ujumbe mkali lakini unaoeleweka kirahisi kwa mamilioni ya wafuasi wake. Hili ndilo linafanya ujumbe wake uwe na athari kubwa kuliko hata wanasiasa wa kawaida.

Zaidi ya hapo, Mange amegusa mahali ambapo watawala wengi hawakutegemea, kundi la watu waliodhaniwa kuwa “hawajui lolote”. Kwa miaka mingi, kundi hili liliaminika kuwa ni mtaji wa watawala, watu wanaofuatilia maisha ya wasanii, mitindo, mahusiano na burudani , lakini sasa ndilo linaanza kuuliza maswali mazito kuhusu Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi, na haki ya kupiga kura kwa usawa.

Nguvu ya ushawishi wa kijamii kupitia mitandao haipaswi kupuuzwa. Katika dunia ya leo, si lazima mtu awe msomi au mwanasiasa ili kuongoza harakati, anachohitaji ni ushawishi, lugha sahihi, na jukwaa lenye ufuasi mkubwa. Mange ana kila kigezo hicho.

Kauli mbiu ya "No Reforms, No Election" sasa inazidi kuenea kama moto wa nyika, na inaweza kuwa mwiba halisi kwa watawala, hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba. Ikiwa kundi lililodhaniwa kuwa “wajinga” linaanza kuamka, basi kuna kila sababu ya kuamini kuwa mfumo wa siasa umeanza kutikiswa kutoka chini.

Mabadiliko haya si ya kawaida. Ni ishara kuwa harakati za kisiasa haziko tena kwenye majukwaa ya mikutano ya hadhara pekee, bali zimehamia kwenye viganja vya watu kupitia simu zao. Kama harakati hizi zitadumu na kupata uungwaji mkono mkubwa, basi historia ya Tanzania ya kisiasa huenda ikaandikwa upya na chanzo chake kikiwa ni jukwaa lililowahi kubezwa kama "mtandao wa wajinga.
 
FB_IMG_1749139137988.jpg
 
Tunakoelekeaa n kuzurii kuliko tulipotokaa na hii safari kwa watz n yetu sote c ya mtu mmoja mmojaa....

Tukazeee...
Hii ni ya watanzania wote na si Chadema tu.
 
Back
Top Bottom