MangeKimambi, kinara wa maandamano ya Oktoba 29 huyu hapa

MangeKimambi, kinara wa maandamano ya Oktoba 29 huyu hapa

Kwani huyo mange anaathirika vipi na maisha mabovu ya bongo?
Kodi zinazoliwa, makato holela.. laini ya spika wa bunge haina makato yako ww ukimtumia mama yako sitimbi inakatwa.

Unadhani hali ingekuwa imenyooka kuna watu wangemsikiliza huyo mange na kifupi mange sio anasikilizwa, ila anapata nguvu sababu wengi hawana pakusemea, mange umekuwa kama spika ya wengi, hivyo watu wanapambana spika isiishe chaji.

Ila kifupi bongo yanayoendelea ni uozo mtupu, kungekuwa na free of speech huyo mange saa hizi angekuwa anatamba na skendo za kina mondi tu...

We uko bongo jichanganye kusema ukweli, kuna ufisadi huu na huu, uone kitakachokusibu
Lazima asafe consequences
 
Anatengeneza taharuki ili apate kuchangamsha App yake ya udaku, atengeneze pesa. Hata akitoka Samia akaja Tundu Lissu naye atamuandika hivyo hivyo ili apate hela
Kama ana andika ukweli hakuna shida aendelee kuwaanika wabadhirifu wote bila kuangalia chama, dini, au kabila.
 
View attachment 3488359

Tanzania haina wajinga na watu wenye fikra fupi na wala hawatakaa wawepo. Kama kuna mtu anadhani anaweza kukaa ughaibuni huko na kuposti mtandaoni eti wenzake waingie mtaani siku na saa fulani kuandamana kisha yeye atumiwe klipu kuposti huku akiwa anapunga upepo na kunywa sharubati basi anajidanganya. Endelea kufurahia matumizi ya bando.
“Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people"
Najua umejiona ulipo kati ya Great, average au small, Mungu akusaidie ili wazazi na uzao wako wasijute kuwa na mtu wa aina yako!
 
Huyo Kinara wa maandamano ukiwasha feni karibu yake upepo unampeperusha
 
Labda wewe siyo mtu wa mitandao ya Jamii. Kwa taarifa yako hii tarehe 29/ 10 imechaguliwa na Mange naye ndiyo mtu wa kwanza kui broadcast. Wanamutandao wengine wamesikia kwake.

Yeye ndiye organiser lakini yuko California
Bora serikali isingekua inawatisha watu.

Swali langu ni je, askari watajuaje huyu anaenda kupiga kura na huyu ameandamana?

Kwa jibu lolote lile ili mimi na familia yangu tuwe salama, siku hiyo tutajifungia.

Kama serikali ingetuhakikishia kuwa ingewalinda wapiga kura pamoja na waandamanaji, ingekua poa sana maana hata mimi mpiga kura nisingekua na wasiwasi.

Sijui kama umeelewa hoja yangu
 
Wewe sio bure utakuwa ni mnufaika na huu mfumo wa wizi na unyonyaji unaoendeleq nchini kwetu
Unadhani ikitoka CCM na ikaja CHADEMA itakubadilishia maisha? Forget about that fella!! Kama mpaka leo hii huwezi kujishughulisha na fursa zilizopo jihesabu tu kuwa unasubiri siku yako ya kufa tu
 
Kama ana andika ukweli hakuna shida aendelee kuwaanika wabadhirifu wote bila kuangalia chama, dini, au kabila.
Kukaa nje ya nchi ma kuandika habari zisizo na uhakika na kuzua taharuki zisizo na msingi kwa watu
 
Daah, Mange ni mzuri hivi kumbe
Sasa uzuri uko wapi ? Au siku hizi neno uzuri limebadilika maana?
Screenshot_20250916_171641_Google.jpg
 
“Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people"
Najua umejiona ulipo kati ya Great, average au small, Mungu akusaidie ili wazazi na uzao wako wasijute kuwa na mtu wa aina yako!
Tayari hata wewe kuingia kwenye huu mjadala umeingia kwenye category ya those who "discuss people".
 
Back
Top Bottom