Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Case CLosed.

Kariakoo na Kivukoni zipo wilaya gani?
😀😀😀 zipo wilaya ya Ilala mkuu. Kuna mwana alidadavua kwamba wilaya ya Ilala ipo vizuri kibiashara ndio maana watu wanatoka maeneo mbali mbali ya mji kuja kufanya biashara katika wilaya hiyo huko kariakoo, posta, feri kivukoni, karume, buguruni nk.

Ila akasema kwa kuishi sehemu nzuri yenye sifa nyingi tajwa hapo juu ni Kinondoni. Ndo maana utakuta wafanya biashara wengi wenye mapesa yao wamejenga mabangaloo ya maana sana katika wilaya hiyo ya Kinondoni kuliko wilaya yoyote ile ya Dar es salaam. Hapa hajazungumzia viongozi wa serikali na wale wastaafu ambao wengi wamejichimbia Kinondoni, mabalozi wa nchi mbali mbali, wabunge nk.
 
Acha kufananisha kinondoni na vitu vya ajabu ajabu!!
Najivunia kuzaliwa kinondoni
 
Unazungumzia majengo ya PSSSF Taasisi ambayo ina michango ya watanzania wote hata walioko Katavi.

Hiyo TPA nayo ni Mali ya Umma.

Nadhani tungeweka vigezo. Kama ni residential areas, pesa kuzunguka , huduma za maji, afya , sewage system n.k.

Hizi akili zako za kuvukia barabara unadhani majengo mazuri ndio welfare Bora ya raia wakati unashi uswekeni. Lete Vigezo vinavyokugusa wewe raia kama housing, Ulinzi na usalama, accessibility ya maeneo kama yakitokea majanga ya Moto n.k. hivyo vigezo ndio vitumike kulinganisha maeneo.

Kwa unayoandika ndio akili za kiafrica unafurahia kwenda kupiga bicha Posta halafu unarudi kwako uswekeni kwenye nyumba iliyojengwa kwenye kiwanja cha

kwa vigezo ulivyotaja nimeviorodhesha hapo chini.
"1. residential areas
2. mzunguko wa pesa
3.huduma za maji,afya,sewage
4. Ulinzi na usalama."

Hivyo vyote ulivyovitaja juu Ilala inaongoza kwa kuwa navyo vyote tena vizuri kulipo wilaya yeyote hapa Tanzania
 
[emoji3][emoji3][emoji3] zipo wilaya ya Ilala mkuu. Kuna mwana alidadavua kwamba wilaya ya Ilala ipo vizuri kibiashara ndio maana watu wanatoka maeneo mbali mbali ya mji kuja kufanya biashara katika wilaya hiyo huko kariakoo, posta, feri kivukoni, karume, buguruni nk.

Ila akasema kwa kuishi sehemu nzuri yenye sifa nyingi tajwa hapo juu ni Kinondoni. Ndo maana utakuta wafanya biashara wengi wenye mapesa yao wamejenga mabangaloo ya maana sana katika wilaya hiyo ya Kinondoni kuliko wilaya yoyote ile ya Dar es salaam. Hapa hajazungumzia viongozi wa serikali na wale wastaafu ambao wengi wamejichimbia Kinondoni, mabalozi wa nchi mbali mbali, wabunge nk.
Umeongea kitaalamu sana, Ilala ndio jiji,makazi safi Kinondoni game imeisha
 
😀😀😀 zipo wilaya ya Ilala mkuu. Kuna mwana alidadavua kwamba wilaya ya Ilala ipo vizuri kibiashara ndio maana watu wanatoka maeneo mbali mbali ya mji kuja kufanya biashara katika wilaya hiyo huko kariakoo, posta, feri kivukoni, karume, buguruni nk.

Ila akasema kwa kuishi sehemu nzuri yenye sifa nyingi tajwa hapo juu ni Kinondoni. Ndo maana utakuta wafanya biashara wengi wenye mapesa yao wamejenga mabangaloo ya maana sana katika wilaya hiyo ya Kinondoni kuliko wilaya yoyote ile ya Dar es salaam. Hapa hajazungumzia viongozi wa serikali na wale wastaafu ambao wengi wamejichimbia Kinondoni, mabalozi wa nchi mbali mbali, wabunge nk.

Ni kweli mkuu Mapedejhee wengi wamejenga Kino - Mbweni JKT.
 
Ukisoma huo mwandiko wangu vizuri nme assume, mbezi beach nmekaa napafahamu vizuri na ninauzoefu na ishu za ujenzi ndio maana nmeweka kama standard...na nyumba nyingi za mbezi zilijengwa muda kidogo wakati vitu bei zilikua hazijapaa sana
Ok sawa mkuu
 
Bandari ipo Ilala
No japokuwa temeke wengi tumeitenga humu, lkn kwa hili tuwe wakweli. Bandari ya Dar ipo katika wilaya ya Temeke mkuu. Hila kila mtu analijua.

Kivukoni, Station na pale kwa kupandia boat za kwenda Zanzibar ndio Ilala.
 
Umeongea kitaalamu sana, Ilala ndio jiji,makazi safi Kinondoni game imeisha
Hakika mkuu. Mimi ni wa Kinondoni ila nakubali kwamba Ilala ipo vizuri kibiashara na kimzunguko wa pesa hasa kwa maeneo ya town kama vile k'koo, mnazi mmoja, posta zote mbili mpya+zamani, kivukoni feri, shule ya uhuru, karume, ilala yenyewe, buguruni nk.

Kwa upande wa Kinondoni yetu huku ni sehem ya kuja kupumzisha kichwa na mwili baada ya pilika pilika za kutwa nzima katika kutafuta ugali na mkate wa watoto.

Mchumia juani hulia kimvulini.
Yani ilala ni 'kuchumia juani mchana' na kinondoni ni 'kulia kimvulini usiku'.
 
No japokuwa temeke wengi tumeitenga humu, lkn kwa hili tuwe wakweli. Bandari ya Dar ipo katika wilaya ya Temeke mkuu. Hila kila mtu analijua.

Kivukoni, Station na pale kwa kupandia boat za kwenda Zanzibar ndio Ilala.
Labda kama unamaanisha chuo cha bandari kule mwembe yanga mkuu, Ila bandari ipo wilaya ya ilala tena (CBD) . Tena makao makuu ya bandari yapo pale jirani kabisa na ofisi za hamashauri ya jiji la Ilala
Nimekuwekea kiambatisho embu jifunze inaelekea huielewi jografia ya hilo eneo.
 
Attachments

Acha kufananisha kinondoni na vitu vya ajabu ajabu!!
Najivunia kuzaliwa kinondoni
Kifupi Kinondoni ndio inaongoza katika mtenenge huu, huku tukifuatiwa na Ilala ambao kiasili ni watani zetu wa kimaendeleo.

Ubungo, Kigamboni na Temeke wao chali wamekosa watetezi. Hata yule jamaa wa Goba leo kaingia mitini.
 
Hiyo ubungo bado ni kinondoni wapuuzi WAnasiasa uchwara waliimega wapate sehemu pa kula

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
wilaya ya Ubungo ipo nyuma sana, nadhani hakuna viongozi weledi na wabunifu.
Mkurugenzi na idara zake wote wamelala ofisini!!!

Kuanzia ilipo Ofisi ya Halmashauri maeneo ya Luguruni hadi Kituo kikuu cha Polisi maeneo ya gogoni Kikuvya bado hakujapangika kabisaaa,
ilitakiwa maeneo hayo yawe na miundombinu safi, mpqngilio safi lakini wapi ovyo kabisa.

maafisa mipango miji wa wilaya ya ubungo wmelala fofofooo
 
Labda kama unamaanisha chuo cha bandari kule mwembe yanga mkuu, Ila bandari ipo wilaya ya ilala tena (CBD) . Tena makao makuu ya bandari yapo pale jirani kabisa na ofisi za hamashauri ya jiji la Ilala
Nimekuwekea kiambatisho embu jifunze inaelekea huielewi jografia ya hilo eneo.
Mkuu bandari ya Dar es salaam ipo katika kata ya Kurasini, na kata ya Kurasini ipo katika wilaya ya Temeke.

Kwahiyo mpaka hapo utakuwa umepata jibu kuwa bandari yetu imeegemea zaidi Temeke kuliko Ilala.

Kwa makao makuu nakubaliana na wewe kuwa yapo Ilala ila bandari ni Temeke.
 
wilaya ya Ubungo ipo nyuma sana, nadhani hakuna viongozi weledi na wabunifu.
Mkurugenzi na idara zake wote wamelala ofisini!!!

Kuanzia ilipo Ofisi ya Halmashauri maeneo ya Luguruni hadi Kituo kikuu cha Polisi maeneo ya gogoni Kikuvya bado hakujapangika kabisaaa,
ilitakiwa maeneo hayo yawe na miundombinu safi, mpqngilio safi lakini wapi ovyo kabisa.

maafisa mipango miji wa wilaya ya ubungo wmelala fofofooo
Ubungo ipo nyuma kuliko wilaya zote yan hata Kigamboni imeiacha ubungo kwa mbali. Inasikitisha sana.
 
Hahahaha mwana analinganisha majengo ya ofisi za serikali na nyumba za kuishi watu, badala ya kulinganisha mitaa kwa mitaa ambayo inaishi watu wa kawaida.

Na mara nyingi watu wa Ilala hukimbilia kujisifu kupitia ofisi za serikali bank za serikali na mashirika mbali mbali ya umma ambavyo hata mimi na wewe pia tunahusika na ofisi hizo.
Mwenye mada, anataka kujua wilaya iliyoendelea, siyo nyumba za makazi.

Hivyo akijivunia majengo makubwa ya serikali yuko sawa tu kwa mujibu wa mada iliopo, Mzee kwani hayo nyumba binafsi, ambazo wewe unajivunia unazimiliki wewe.

Dar ni mji mmoja, unaweza kuishi kinondoni, ila pia ukaziishi tabu na raha za ilala, au unaweza kuishi ilala ukaziishi tabu raha za kinondoni.
Kuna watu mchana kutwa wako ilala, kulala kinondoni, na wapo wengine mchana kutwa yupo kinondoni kulala ilala.

Hii kwa Dar mzima na pwani, hivyo tujivunie maendeleo ya jumla.
 
Back
Top Bottom