Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Kabila na ukabila vilikuwepo vipo na vitakuwepo mpaka dahali wakuviondoa bado hajazaliwa na akizaliwa atakufa na ataviacha viendelee kushamiri.
Kwani ili mtu akusaidie kwenye msiba ni lazima awe wa kabila lako tu? Hoja dhaifu hii.


Mlikotoka kuna kabila moja tu? Hoja mufilisi hii.

Mnyeti shikilia hapo hapo baba. Majitu haya yanaleta ukabila nchini.
 
Kwani ili mtu akusaidie kwenye msiba ni lazima awe wa kabila lako tu? Hoja dhaifu hii.


Mlikotoka kuna kabila moja tu? Hoja mufilisi hii.

Mnyeti shikilia hapo hapo baba. Majitu haya yanaleta ukabila nchini.
Mkuu wewe kabila lako ni lipi? Je,una kabila au huna?
 
Wachaga ni wakabila sana! Ukitaka kila siku humu za kujisifu. Sifa za ukabila na ukanda!

Amefanya la maana sana. Kazi kuwasema wapinzani wenu nshomile kumbe nyie ndo wakabila wa kwanza
 
Mnyeti asichojua ni kuwa kwa kufanya hivyo ndio amewaunganisha zaidi wachaga.
Hawa jamaa wako kama Waisrael, jinsi wanavyotengwa ndivyo wanavyo pendana zaidi na kutumia akili ya ziada kujilinda.
Usishangae ukienda Babati ukakuta wana mfuko wa maafa una mamilioni na hawaibiani zaidi ya kukomboana kwenye madhila.
 
Mbona nawewe kama huna tofauti na Mnyeti? Wivu wa kike? Huo nao ni ubaguzi tu
Sijasema mimi ni tofauti,nimeshangaa tu....Msemo ni uthibitisho kwamba identities ni sehemu ya jamii....
 
Nadhani mngemjibu kwa hoja ingependeza zaidi!
ni vizuri na yafaa kujibu hoja kwa hoja. sio kila mawazo ya mtu ni hoja. sexless ana hoja gani? kwamba vikundi kama hivyo walivianzisha udsm, mukandala kavifutilia mbali; ni hoja? wengi hapa hatujui maana ya ukabila. ukiulizwa kabila gani unang'aka kuwa muulizaji analeta ukabila! Mungu anaumba makabila. haumbi mataifa. ni taifa moja tu analojua mipaka yake. mataifa mengine wanajua wanadamu.
 
Majuzi niliona video clip ikitembea kwenye social media ikimnukuu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Komred Alexander Mnyeti akitoa tamko la kusitisha shughuli ya Umoja wa Watu wa Kilimanjaro katika mkoa wa Manyara.

Baada ya video hiyo kusambaa nikaona jamii ya Wachaga na wafuasi wao wa vyama vya Upinzani na hata ndani ya Chama cha Mapinduzi wakipiga kelele kuwa wachaga wameonewa.

Wapambe hao wa jamii ya wachaga wakaenda mbali na kudai ndugu Mnyeti analea ukabila katika mkoa wake.

Nimejitahidi sana kurudia kutizama video Ile sijaona mahala ambapo Mkuu wa Mkoa amewataja wachaga bali wametajwa watu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Je, mkoa wa Kilimanjaro wanaishi kabila la Wachaga tu?

Mimi niajuavyo mkoa wa Kilimanjaro kuna makabila kadhaa kama ifuatayo:

Wachaga ambao wamegawanyika katika koo kadhaa ambao ni Wamachame, Wamarangu, Warombo, Wahuru, Wakibosho, nk.

Makabila mengine ni Wapare, Wamasai, Wasiha na Wataita. Wamarangu, Wakibosho, Wahuru, wanaishi Wilaya ya Moshi. Wasiha na Wamasai wanaishi Wilaya wa Siha Warombo na Wataita wanaishi Wilaya ya Rombo.

Wilaya ya Hai wanaishi Wamachame, Wamasai na Wasiha. Wapare Wanaishi Wilaya ya Same na Mwanga.

Makabila yote haya ni jamii wanaoishi mkoa wa Kilimanjaro kwanini wachaga ndiyo wapige kelele? Kuna agenda gani iliyojificha katika Umoja wa Watu wa Kilimanjaro huko Manyara?

Hii dhana ya jamii ya wachaga kupiga kelele kuwa wanaonewa na serikali ya Awamu ya tano haijaanza sasa kwa Mnyeti.

Mtakumbuka Mara baada ya Mh Rais wa Tanzania kuunda baraza la mawaziri walianza kupiga kelele kuwa mkoa wao umetengwa wakati katika baraza la kwanza la Mhe Magufuli walikuwepo Mawaziri wawili na Naibu waziri kutoka mkoa wa Kilimanjaro.

Mawaziri kutoka Mkoa wa Kilimanjaro waliokuwepo kwenye baraza la kwanza la Mhe Magufuli ni professor Maghembe Jumanne na Angel Mkwizu Kairuki lakini kwasababu hao sio Wachaga ilionekana Kilimanjaro wametengwa.

Jamii ya Wachaga hapa nchini wanakadiriwa kufika watu kama milioni mbili na laki mbili hivi sawa na 2.0% ya Watanzania wote.

Hawa ndugu zetu wanaishi katika Wilaya tatu tu zinazozunguka Mlima Kilimanjaro hapa nchini lakini wamekuwa watu wabinafsi ambao kila kitu wanataka wahodhi wao.

Hivi kwanini Mh Alexander Mnyeti alipopiga marufuku umoja wa watu wa Mara kule Mererani mkoani Manyara mbona hatukuona kelele hizi za utetezi kama tunavyoona sasa?

Hivi waandishi hawakuona ili la watu wa Mara au watu wa Mara sio Watanzania?
Mbona Umoja wa Wanamara walipopigwa marufuku hawa watetezi wa sasa wa wachaga hatukuwaona? Au nchi hii kuna makabila ambayo ni daraja la kwanza na wengine ni madaraja ya chini?

Hawa watetezi wa kabila la daraja la juu hapa nchini ( Wachaga) wanadai Umoja wao unawasaidia katika misiba hivi bila Umoja misiba haisafirishwi?

Hii tabia ya wachaga kujiona kuwa wao ni Kabila la daraja la juu hapa nchini ni la kupingwa kwa nguvu zote hata sehemu za kazi wasipoajiriwa utawaona wanalalamika kuwa wanaonewa imefika hatua hata Mh Rais akifanya Uteuzi wanaanza kutizama kama kuna mchaga kama hajateuliwa mchaga utasikia wanalalamika Rais anateua ndugu zake kutoka Chato.

Tunafahamu Mkakati wa jamii hii kupitia vyama vya siasa hata kuelekea mwaka 2015 aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mheshimiwa Joshua Nassari alijikuta akitoa siri ambayo ndiyo Mkakati wa muda mrefu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kupitia Jumuiya ya nchi za Ulaya Magharibi.

Mengine ngoja ninyamaze.

Itoshe tu kusema hakuna kabila la daraja la kwanza hapa Tanzania kama watu wa Mkoa Mara walipigwa marufuku mkoani Manyara na hatukupiga kelele hata sasa tuendelee kunyamaza wakati watu wa Mkoa wa Kilimanjaro nao wakipigwa marufuku.

Naandika kutokea hapa Uwanjani wa CCM Kirumba Jijini Mwanza muda huu saa 8.03 alfajiri tayari kwa sherehe ya Uhuru.

#Happy58IndependenceDay
 
Wachaga Hoyee3eeee. Kabila Maarufu Tanzania. Kila mtu analifahamu. Hoyeeeee Kwa kuwattoa Povu wenye Husda na Vijiba vya Roho juu ya Ustawi wenu🤪🤪👍💪👏👏👏👍💪. Hata mfanyeje hawa Watu watazidi kushikamana. Social Cohesion Yao ndio Utambulisho wao. Mchaga hajawahi sahau Kwao hata kama ni muuza Kongoro Supu alipo, kurudi kwao Lazima. Mtashindana nao Mtawapa Sifa zote Mbaya lakini Hamtashinda. Msahau Kwaoo Mtumwa. Viva Wachaga Hatimaye Mme Prove kuwa Mlipo ni Mojawapo ya Matatizo ya Wasio na Kwao.
 
Mkuu, ktk jambo ambalo mtu makini hapaswi kufanya ni kuhamisha ama kupiteza mantinki ya mjadala. Katika hilo "generalisation" ya mambo haiwezi kutumika kuhalalisha mapungufu ya kiongozi mwenye dhamana ktk ofisi ya umma.

Kama watu wa Mara wametendewa yasiyopaswa kufanywa na wakaamua kukaa kimya, haiwezi kuwa sababu ya watu wa mkoa wa Kilimanjaro pia waige huu ukondoo. Haki za msingi za kiraia ndicho kitu cha msingi kuzingatia, naona si viongozi wenye dhamana ambao wanaona fahari kumomonyoa misingi ya utaifa bali hata wapambe wengi ambao wapo humu ktk "social media'

Hivi tunapo wazungumzia Wachagga na kile kinachopigiwa kelele na wale wote wenye "perception error" juu yao kuwa ni wabaguzi, hivi tumzungumzia Mchagga yupi hasa? Je! Ni hawa waadhiri na walimu ambao wapo ktk vyuo na shule nyingi hapa nchini? Ni madaktari, mainjinia na wabobezi wengi ambao wametawanyika ktk fani nyingi hapa nchini?

Je! Ni hawa wakina mangi wenye kumiliki biashara ndogo, za kati na hata kubwa zilizotapakaa kote nchini? Ni hawa makasisi, wachungaji na hata maaskofu na viongozi wa dini ambao wametapakaa kite nchini? Je! Ni wale wakulima na vibarua maskini ambao wamekosa pa kwenda na kujikuta wakiishi ktk ardhi ya babu zao na kupigika kama Watanzania wengine?

Mimi, nashauri tuepuke sana "perception errors" na kuhalalisha ubaguzi juu ya kabila hili, ni ukweli uliokuwa wazi babu zao waliziona fursa mapema, wakafunguka macho na hata kuyakubali maendeleo zaidi ya makabila mengine hapa nchini. Kwenye kila "cluster out of sampling" inapoonekana wamehodhi nafasi nyingi za kitaaluma, hii inatokana na uwekezaji mkubwa waliokwisha kuufanya ktk sekta ya elimu toka ngazi ya familia kwa muda mrefu sasa.

Tuwatendee haki kwa kujifunza na kuiga mazuri kutoka kwao. Chuki yoyote dhidi yao haindoi sifa wala weledi waliouwekeza ktk vijana wao, umahiri wao ktk kuendesha biashara na hata ustaarabu wa kutukuka wa kabila lao.
 
Kuimba ni kupokezana wanasema wenye lugha yao adhimu ya kiswahili.

Wasukuma wanakashifiwa sana awamu hii, lakini kinachosahaulika ni ukweli kwamba hili ni kabila lenye mikoa mitano, Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Tabora, hili ndilo kabila kubwa kuliko yote juu ya ardhi ya Tanzania.

Lakini ni watu fulani wakimya wasio na makuu ambao siku zote kunyenyekea kwao ni jambo la kawaida tu.
 
Mnyeti hataki wachaga tu , lakini ameruhusu makabila ya Manyara kuanzisha vikundi na ameenda mbali zaidi kwa kuwaambia wachaga kwmba kama wanataka vikundi hivyo wakaanzishie kwao .
Usibishane na huyo anajitoa ufahamu maksudi !!
 
Sexless,
Umeisikiliza clip vizuri? Ametakataza wachaga ila hao wa huko wairaq, wafyome, nk waanzishe vikundi vyao ila wachaga wakaanzishie Moshi! Usijitoe ufahamu!!

Kuhusu Mukandara anajua sababu zake mwenyewe, suala haswaa kulikuwa based kwenye ukabila huohuo. Yeye alivikuta vikundi hivyo hata wakati anasoma alikuwemo kwenye vikundi!

Suala ni vikundi vikaanza kutafuta madaraka kwa kupambana, kundi lake halikuwa na nguvu, kwa hamnazo yeyote atampongeza without knowing his motive behind, motive haikuwa nzuri!!
 
👍💪💪💪👏👏👏👏👋👋👋
Mkuu umechambua vizuri sana. Ila ukweli ni kwamba hawabaguliwina pia haiwezekani kuwabagua watu wenye nguvu ya uchumi na Elimu Kama Wachagga. Kilichokatazwa na mnyeti ni umoja wa vikundi vya kikabila. Tulipata viongozi wa kutuambia hapa sio sawa, hata Kama inakugusa wewe moja kwa moja, tukubali na kujisahihisha. Ila ninyi Wachagga mnapendeleana Sana katika maeneo ya kazi za umma. Katika kupendeleana kwenu, mnajikuta mmetubagua na sisi Warangi na Wapare.
 
Bora tu kuanzisha Rift Valley Republic ambayo itakuwa na mji mkuu wake hapo Arusha.
Manyara Kilimanjaro na Arusha kwa maana uonevu umetalamaki
Muwe mnapima comment zenu kabla ya kubandika hapa....
 
Mkuu umechambua vizuri sana. Ila ukweli ni kwamba hawabaguliwina pia haiwezekani kuwabagua watu wenye nguvu ya uchumi na Elimu Kama Wachagga. Kilichokatazwa na mnyeti ni umoja wa vikundi vya kikabila. Tulipata viongozi wa kutuambia hapa sio sawa, hata Kama inakugusa wewe moja kwa moja, tukubali na kujisahihisha. Ila ninyi Wachagga mnapendeleana Sana katika maeneo ya kazi za umma. Katika kupendeleana kwenu, mnajikuta mmetubagua na sisi Warangi na Wapare.
Ofisi za Umma zipo? Toa mfano na sifa zao.
 
Hivi jirani yako ni nani? Mpaka kusaidiana kuwe ni kutokana na mlikotoka, basi hate biashara na vitu vingine tuungane mkono kutokana na tunakotoka? ?
 
Tuwasikilizw viongozi wetu. Kuna mengi hatuyajui, na naamini anayo nia njema kwa nchii hii.
 
Back
Top Bottom