LGE2024 Manyoni: Jeshi la Polisi linamshikilia Askari aliyesababisha kifo cha mgombea wa CHADEMA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia Askari mmoja wa Jeshi la Magereza kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwananchi mmoja tukio ambalo lilitokea Novemba 26,2024 majira ya saa 5:00 usiku huko katika Kitongoji cha Stendi, kata ya Mkwese Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida.

Chanzo cha tukio hilo ni kwamba katika eneo hilo kuna wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM walikuwa katika nyumba moja wakiwa na kikao chao cha ndani. Wakati kikao hicho kikiendelea walivamiwa na kundi la wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vurugu kubwa kutokea ambapo askari magereza ambao wapo katika gereza ambalo lipo karibu na eneo hilo walipigiwa simu kujulishwa juu ya vurugu hizo ikabidi watoke kwenda kuona hali ilivyo huku wakiwasiliana na polisi, walipofika eneo la tukio walianza kushambuliwa kwa mawe jambo lililowalazimu kupiga risasi hewani kuwatahadharisha na kuwazuia watu waliokuwa wakiwashambulia kwa mawe.

Aidha, Katika purukushani hizo, risasi moja ilimjeruhi George Juma, (41), ambaye alikuwa mgombea wa kitongoji cha Stendi kupitia CHADEMA. Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kufanikisha kuwakamata wale wote waliosababisha vurugu hizo.

Jeshi la Polisi Singida linatoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuendelea na shughuli za upigaji kura kuwachagua viongozi wao kwa amani na utulivu kwani Jeshi la Polisi liko imara katika ulinzi kipindi hiki cha kupiga kura na kutangaza matokeo kwa viongozi watakaochaguliwa.

Pia Jeshi la Polisi Singida linatoa onyo kwa mtu yeyote atakayevuruga zoezi la uchaguzi kwani halitasita kumchukulia hatua za kisheria.

Imetolewa na Amon Daudi Kakwale - SACP
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.

Kuhusu kifo cha kada wa CHADEMA, soma LGE2024 - TANZIA - Manyoni: George Juma Mohamed, Mgombea wa CHADEMA auawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia tar 27, 11, 2024

4R
 
Nchi hii uongo limekuwa jambo la kawaida sana kuanzia ikulu mpaka mitaani
 
Kapewa maelekezo anatimiza..
Anakamatwa ila kazi imeisha.
Mnazugwa.
Anarudi mzigoni.
Ndiyo lazima arudi kazini kama alipiga risasi juu kuonya na akaendelea kupigwa na mawe kweli maana Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sect 21 (2)( 1) cap 20 R.E 2022 inamruhusu askari kutumia silaha ikiwezekana kuua kwaajili ya kutetea uhai wake au uhai wa watu wengine

Kwahiyo ukivunja sheria ujue kuna mipaka ukifikia unaweza kuuwawa
 
Ndiyo lazima arudi kazini kama alipiga risasi juu kuonya na akaendelea kupigwa na mawe kweli maana Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sect 21 (2)( i) cap 20 R.E 2022 inamruhusu askari kutumia silaha ikiwezekana kuua kwaajili ya kutetea uhai wake au uhai wa watu wengine

Kwahiyo ukivunja sheria ujue kuna mipaka ukifikia unaweza kuuwawa
It's okay mkuu, Je askari huyo hana Jina?.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia Askari mmoja wa Jeshi la Magereza kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwananchi mmoja tukio ambalo lilitokea Novemba 26,2024 majira ya saa 5:00 usiku huko katika Kitongoji cha Stendi, kata ya Mkwese Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida.
Kwa hiyo huyu anatuhumiwa tu? Hatajwi hata jina? Na kwanini wamshikilie ikiwa ameua akiwa anafanya kazi yake na Sheri na Marekebisho ya Katiba yanamlinda?
Chanzo cha tukio hilo ni kwamba katika eneo hilo kuna wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM walikuwa katika nyumba moja wakiwa na kikao chao cha ndani. Wakati kikao hicho kikiendelea walivamiwa na kundi la wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kwa hiyo uchunguzi umefanyika na umekamilika? Na ndiyo maanap hapa hakuna anayethumia? Kwanini wamshikilie huyo askari wa Magereza na kwanini waendelee kumtuhumu?
na vurugu kubwa kutokea ambapo askari magereza ambao wapo katika gereza ambalo lipo karibu na eneo hilo walipigiwa simu kujulishwa juu ya vurugu hizo
ikabidi watoke kwenda kuona hali ilivyo huku wakiwasiliana na polisi, walipofika eneo la tukio walianza kushambuliwa kwa mawe jambo lililowalazimu kupiga risasi hewani kuwatahadharisha na kuwazuia watu waliokuwa wakiwashambulia kwa mawe.
Utaratibu wa askari wa Maereza kuomdoka kituoni na kwenda kukabiliana na civil unrest upoje?
Aidha, Katika purukushani hizo, risasi moja ilimjeruhi George Juma, (41), ambaye alikuwa mgombea wa kitongoji cha Stendi kupitia CHADEMA. Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kufanikisha kuwakamata wale wote waliosababisha vurugu hizo.
Ni uchunguzi gani unaoendelea hapo wakiti hapo juu wametumia kauli za kuhukumu?
Jeshi la Polisi Singida linatoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na
Mbona wananchi wanatuhumiwa kuchukia sheria mkononi wakati askari ambao waliingilia jukumu lisilowahusu hatuoni rai yoyote ikielekezwa kwao?
Pia Jeshi la Polisi Singida linatoa onyo kwa mtu yeyote atakayevuruga zoezi la uchaguzi kwani halitasita kumchukulia hatua za kisheria.
Wangese wanatoa onyo kwa mtu yeyote asiye wa Chama Cha Mapinduzi atakayejaribu kuvuruga uchaguzi, binafsi ningewaheshimu na kuwaamini sana. Kinyume cha ni upuuzi na ulongo
 
download.jpeg
 
inakuwaje risasi imfuate mgombea tu ....kwanini isingempiga mwingine yeyote.
duh!!
 
Nijuavyo ni kuwa gereza liko Manyoni mjini,Kijichi cha mkwese kipo umbali wa KM 14 kutoka Manyoni mjini, inawezekanaje askari magereza kwenda kutuliza fujo umbali wa 14km?
 
Back
Top Bottom