LGE2024 Manyoni: Jeshi la Polisi linamshikilia Askari aliyesababisha kifo cha mgombea wa CHADEMA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wameshasema CHADEMA walikuja "kufanya vurugu"... sasa uchunguzi wa nini tena?
 
4R
 
Nchi hii uongo limekuwa jambo la kawaida sana kuanzia ikulu mpaka mitaani
 
Kapewa maelekezo anatimiza..
Anakamatwa ila kazi imeisha.
Mnazugwa.
Anarudi mzigoni.
Ndiyo lazima arudi kazini kama alipiga risasi juu kuonya na akaendelea kupigwa na mawe kweli maana Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sect 21 (2)( 1) cap 20 R.E 2022 inamruhusu askari kutumia silaha ikiwezekana kuua kwaajili ya kutetea uhai wake au uhai wa watu wengine

Kwahiyo ukivunja sheria ujue kuna mipaka ukifikia unaweza kuuwawa
 
It's okay mkuu, Je askari huyo hana Jina?.
 
Kwa hiyo huyu anatuhumiwa tu? Hatajwi hata jina? Na kwanini wamshikilie ikiwa ameua akiwa anafanya kazi yake na Sheri na Marekebisho ya Katiba yanamlinda?
Kwa hiyo uchunguzi umefanyika na umekamilika? Na ndiyo maanap hapa hakuna anayethumia? Kwanini wamshikilie huyo askari wa Magereza na kwanini waendelee kumtuhumu?
Utaratibu wa askari wa Maereza kuomdoka kituoni na kwenda kukabiliana na civil unrest upoje?
Aidha, Katika purukushani hizo, risasi moja ilimjeruhi George Juma, (41), ambaye alikuwa mgombea wa kitongoji cha Stendi kupitia CHADEMA. Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kufanikisha kuwakamata wale wote waliosababisha vurugu hizo.
Ni uchunguzi gani unaoendelea hapo wakiti hapo juu wametumia kauli za kuhukumu?
Jeshi la Polisi Singida linatoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na
Mbona wananchi wanatuhumiwa kuchukia sheria mkononi wakati askari ambao waliingilia jukumu lisilowahusu hatuoni rai yoyote ikielekezwa kwao?
Pia Jeshi la Polisi Singida linatoa onyo kwa mtu yeyote atakayevuruga zoezi la uchaguzi kwani halitasita kumchukulia hatua za kisheria.
Wangese wanatoa onyo kwa mtu yeyote asiye wa Chama Cha Mapinduzi atakayejaribu kuvuruga uchaguzi, binafsi ningewaheshimu na kuwaamini sana. Kinyume cha ni upuuzi na ulongo
 
inakuwaje risasi imfuate mgombea tu ....kwanini isingempiga mwingine yeyote.
duh!!
 
Nijuavyo ni kuwa gereza liko Manyoni mjini,Kijichi cha mkwese kipo umbali wa KM 14 kutoka Manyoni mjini, inawezekanaje askari magereza kwenda kutuliza fujo umbali wa 14km?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…