SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,338
- 4,676
Inasemekana kuwa barua ya maombi ya kujiunga na CCM ya mbunge wa kiibamba JJ Mnyika wa chadema imekwamishwa na Wanene wa CCM. Sababu kuu ni kauli ya dharau na kuudhi aliyoitoa Mnyika katika bunge la Makinda iliyomlenga Rais wa awamu ya 4 aliyekuwa pia Mwenyekiti wa CCM taifa. Inadaiwa ama Mnyika amuombe JK msamaha hadharani au amwandikie KM wa CCM barua nyingine ya kuomba radhi na copy aipeleke kwa mstaafu JK. Nimejulishwa na mwana Ufipa mmoja juu ya kadhia hii, binafsi naomba niishie hapo!
1. Tunakaa tunawalaumu sana mataifa ya Magharibi na Marekani, na sasa China,kwamba wao ndio wanatuhujumu kiuchumi, lakini tatizo kubwa na pekee ni sisi wenyewe waafrika. Kwa thinking kama hii ya kwako, ya kuamini kwamba Mnyika akija CCM ndio CCM ita-balance au itaweza kuwaletea wananchi maendeleo ndio maana tumeshindwa kusonga mbele pasi na kufahamu tatizo ni nini hasa?
2. Hivi kweli fikra kama hizi za mtu Wa Level yako kuamua kushughulisha akili yako kuandika vitu vya kutunga sio ishara na kielelezo tosha cha jinsi tunavyochezea rasilimali muda?
3. Hivi watanzania na hasa tunaojiita wasomi kuamua kukaza akili zetu katika kushawishi watu wahamie katika vyama vyetu ndio matunda ya kukaa kwetu madarasani kwa zaidi ya miaka 16?
4.Je,fikra kama hizi za kuacha kuandika mambo chanya na kuamua kutunga mambo ambayo kwa hakika unafahamu hayana Kichwa wala miguu,inatosha kusadikisha kwamba Taifa hili kweli watu wake wanajitambua?