Ufike wakati watu tuwe na fikra huru.
Mimi aina team, Kiba ni msanii mzuri lakini hana amsha amsha zinazoendana na tukio kama lile la jana ambalo lilihitaji hamasa kubwa kuashiria kufana kwa ufunguzi.
Kosa la kwanza ulilolifanya ni kudhani fikra zangu hazipo huru. ( ondoa hii nadharia afu tutaelewana vizuri tu).
Kati ya Simba day za Hovyo kuwahi kutokea ni ambayo Diamond aliperform.
Hizo unazoziita amsha amsha ndio zilifanya performance iwe mbaya......
Uwanja ule ni mkubwa huwezi kuutawala kwa Mavurugu, ukiuendea kwa pupa utakutia aibu.
Diamond aliishia kukimbia kwenye running track kama Mwehu badala ya kuperform.
Wakati unanitaka mimi niwe na fikra huru, umesahau kuwa wewe ndio uko biased.
1.Kiba ana maringo, so maringo yake ( kama anayo) yanawahusu nini watu walioenda uwanjani?
2. Umeshindwa kuonyesha ni namna gani Ali kiba ameliangusha tamasha la jana ( Tamasha bora la mpira kuwahi kufanyika Tanzania ).
Kingine wakati, unasema Kiba ana maringo ni vyema mkamkumbusha mondi kuchunga mdomo wake, na kuelewa nafasi yake kwenye jamii.
Asidhani alivyo na "zombie " fans kwenye muziki basi ana hiyo influence kwenye Mpira.
Wakati diamond na Familia yake wanashirikiana na Manara kutaka kumfitinisha Mo na mashabiki wa Simba alitakiwa aelewe kuna Kesho, na huyo Manara hana uwezo wa kumfikisha Popote.