Maoni: Dkt. Batilda Buriani ameshushwa mno kuteuliwa kuwa Katibu Tawala

Maoni: Dkt. Batilda Buriani ameshushwa mno kuteuliwa kuwa Katibu Tawala

Nimeona Ndugu mmoja aliyekuwa na cheo cha Waziri, Balozi na hatimaye kuja kuteuliwa kuwa Katibu Tawala. Kwa ushauri wangu huyu sasa angepaswa kupumzika na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi fulani. Kweli mtu alikuwa Mhe. Waziri leo anakuwa Katibu Tawala?.
Njaa hatari,amefanya lobbying apate japo chakula,unaweza kukuta hata Ada ya kusomeshea hana,
 
Alikuwa mchepuko wa Lowasa,kipindi anagombea ubunge Arusha mjini,2010,hana jipya,anakitu gani Cha upekee!?hapo ashukuru tu,maana lazima Kikwete amemuombea apatiwe Ka nafasi asije kufa njaa,huyu hakutakiwa kurudi kabisa,mtu alikuwa Mbunge 2010!amekuwa Balozi,miaka 11 baadae,anapewa nafasi Tena kwenye utumishi wa umma,tujiulize miaka yote hiyo alikuwa anafanya nini?ana biashara,alikuwa anasoma,
Mh Raisi hizi teuzi zake hazina tija kwa Taifa,Urafiki umejaa sana.Utumishi wa umma sio sehemu ya kwenda kuzeekea,ni sehemu ya kujenga nchi,sasa hivi vizee anavyoteua vya Kazi gani?
Ndio maana hatuendelei
 
acheni mambo yenu, Malecela aliwahi kuwa waziri akapelekwa iringa kuwa Mkuu wa Mkoa halafu akaja kuwa waziri Mkuu, Marehe Samuel Sita alikua Waziri akaja kuwa Mkuu wa Mkoa akarudi kua spika hayo mambo yapo toka enzi ya Mwalimu na wapo wengi tu
 
Mradi roho yake ina amani mwacheni tu achape kazi...
 
Kwenye maisha hakuna aibu, unapaswa kuishi kulingana na kipato/uwezo wako sio ku-fake au kulazimisha ukubwa au ufahari au kulazimisha heshima utajikuta unaadhirika x3, unapaswa kubadilika na hali yako ipasavyo ndio HEKIMA NA BUSARA
 
watanzania tuna ujuaji Sana.
Kuna watu hata ujumbe WA nyumba 10 hawajawahi kupewa
 
Bora wangempa hata ubunge wa Magogoni. Mama Samia sijui anakwama wapi?
 
Dk. Batilda Buriani Alikuwa Balozi Kenya na Japan, Leo kateuliwa kuwa Katibu Tawala mkoa? Ni kudhalilishwa mno, ni MAWAZO yangu. Angepewa hata ukuu wa Mkoa
Mme Wa Batilda Ndio Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar, Yule Jamaa Wa Act-W
 
..mbona Rashidi Kawawa alishuka toka Waziri Mkuu mpaka kuwa Waziri asiye na wizara maalum.

..baada ya uhuru Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu na Mzee Kawawa akashika usukani wa nchi.

..Mzee Kawawa alishuka toka kuwa kiongozi mwenye walinzi na msafara, mpaka kuwa kiongozi wa kawaida ambaye gari yake inabidi isukumwe kwanza ndio iwake.

..Pia yupo Mzee Msuya ambaye alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Raisi baadae akashuka akawa Katibu wa Uchumi CCM wilaya ya Mwanga.
Vijana hawawezi jua haya JokaKuu
 
Dkt. Batilda Buriani alikuwa Balozi Kenya na Japan, Leo kateuliwa kuwa Katibu Tawala mkoa!! Ni kudhalilishwa mno, ni mawazo yangu.

Angepewa hata ukuu wa Mkoa.
Labda katumwa kufanya kazi maalumu,Kama ya Kihamia.
 
..mbona Rashidi Kawawa alishuka toka Waziri Mkuu mpaka kuwa Waziri asiye na wizara maalum.

..baada ya uhuru Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu na Mzee Kawawa akashika usukani wa nchi.

..Mzee Kawawa alishuka toka kuwa kiongozi mwenye walinzi na msafara, mpaka kuwa kiongozi wa kawaida ambaye gari yake inabidi isukumwe kwanza ndio iwake.

..Pia yupo Mzee Msuya ambaye alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Raisi baadae akashuka akawa Katibu wa Uchumi CCM wilaya ya Mwanga.
Hiyo ya mwisho ni balaa.
 
Back
Top Bottom