Maoni: Ifanyike tathmini ya Uchaguzi wa 2019/2020 kabla ya kufanyika uchaguzi 2024/2025

I once again confirm to you without fear of contradiction, uchaguzi unafanyika 2025 bila Katiba mpya na kwa Amani na utulivu haijapata kutokea katika historia ya Tanzania...
Nikwambie yafuatayo,

Mchezo wa siasa ni mchezo huru,

Polisi na virungu, Risasi vikae pembeni,

Tutakusanyika wenye kutaka Tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya 2025.

Pia wewe na chama chako kusanyikeni Kwa wakati wenu mnaotaka tuingie uchaguzi bila Tume huru na Katiba mpya.

Itapigwa kura ya WAZI na tutapata mshindi.

Na maoni hayo yaheshimiwe.

CCM hamna uhalali wa HOJA mnazosumamia Kutoka Kwa wananchi. Ikiwa mnao wanaowasupport nyuma yenu watoke hadharani.

Kujificha nyuma ya mgongo wa Polisi na Jeshi haitawasaidia.

Siasa ni mchezo huru.

Njooni Kwa battle ,polisi wasimamie Amani basi.
 
Haya ni mambo ya kawaida kutofautina katika demokrasi ya vyama vingi. Mimi nasema tume ni huru wewe unasema siyo huru. Wewe unataka serkali 3 mimi nataka 2. Kwa nini yasiingizwe kwenye Ilani watu wachague?
 
Haya ni mambo ya kawaida kutofautina katika demokrasi ya vyama vingi. Mimi nasema tume ni huru wewe unasema siyo huru. Wewe unataka serkali 3 mimi nataka 2. Kwa nini yasiingizwe kwenye Ilani watu wachague?
Yaingizwe kwenye Ilani ipi Ili tuchague?
 
Ww utakuwa ni mzee lazima, wazee ndio huwa na vitisho hivi vya kishamba.
 
Wengine tulishavuka viwango wa kutishwa.

Ikiwa ninachosimamia ni Kweli na HAKI Wala siogopi.

Halafu ujue, kuandamana imeruhusiwa kikatiba, Si kosa la jinai kuandamana.

Juzi mlivyoandamana kumpokea Makonda nani aliwangoa meno?

Changia basi kama mtu timamu!!
 
Haya ni mambo ya kawaida kutofautina katika demokrasi ya vyama vingi. Mimi nasema tume ni huru wewe unasema siyo huru. Wewe unataka serkali 3 mimi nataka 2. Kwa nini yasiingizwe kwenye Ilani watu wachague?
Unamaanisha iitishwe kura ya maoni juu ya wanaotaka Uchaguzi BILA Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA VS Wanaotaka Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya KABLA ya Uchaguzi mkuu?

Nakubaliana nawe ktk hili.πŸ™
 

Mkuu ni muhimu sana kutambua CCM hawataki iwepo katiba mpya wala tume huru kwa malengo yaliyo wazi.

Kumtegemea CCM anaweza akatufanyia wepesi au huruma yoyote achilia mbali haki, ni muhimu mno kujua hilo halipo.

Hivyo kama hatutasimama wenyewe imara kupambana kwa nguvu zetu wenyewe, basi na tusahau kupatikana kwa katiba tunayoihitaji, na hata milele.

Ni lazima tuuvae ujasili Sasa tupambane. Haipo namna nyingine:

1. "Lissu: Watanzania si waoga, ila wenye kutunyooshea kidole"

2. "Lissu: Tukubali kukosolewa, tuukatae u CCM

3. "Lissu: Hakuna Katiba Mpya, hakuna uchaguzi

Ni kuwa, kwa bahati mbaya mno kuna tetesi zenye ka harufu ka kukwamishana na hata kutaka kuenguana ikiwezekana ndani ya CDM.

Huyu mwamba wanamwona kizingiti kwa maslahi fulani binafsi japo wakijua ni asset kwenye mapambano na kwa wananchi.

Mzani unalalia kwenye maslahi binafsi:

Mchongo ni huu:

Ajabu ni kuwa, kuna wanaomchukia mno Kila wauonapo mchango wa mwamba kwenye ukombozi usiopingika, ukitambulika kokote na hasa inapokuwa dhahiri anastahili kupewa maua yake.

Humo wamo kutokea CCM, CHADEMA na hata wasomi (wenziwe).

CCM - Hawa wanajua huyu anawapalilia kiama chao kwa dhahiri iliyo karibu mno.

CHADEMA - Hawa ni wale wa Baniani mbaya ila kiatu chake dawa.

Wasomi - husuda za kisomi na chuki za mafanikio mtambuka.


Ni lazima tupige kelele.

Katiba mpya ilikuwapo sasa kwa kuunganisha nguvu zetu tu hapo 9/11.

Hivi kweli, ni kwa sababu ya ubinafsi tu?

Kuililia CCM kufanya lolote la haki kwa maneno matupu ni dua la kuku.

Hatima yote tuko nayo mikononi mwetu. Ni kusuka au kunyoa.
 
Ndio lengo Hasa.

Wananchi wenzetu waone umuhimu wa Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote 2024&2025.

Baada ya hapo, tuandamane na MASHUJAA wetu, Mwabukusi, Slaa, Mdude, Madeleka , Lissu,Mwamakula nk nk.

Hiyo ndo njia pekee ya kuamsha umma kupinga Hila za kufanya uchaguzi wa maigizo.

Pamoja sana ndugu Brazaj.πŸ™
 

Tutoke kwenye maneno, wanatuita vyama vya taarifa.

Hilo jina wanapaswa kulifuta wao siyo sisi.
 
Tutoke kwenye maneno, wanatuita vyama vya taarifa.

Hilo jina wanapaswa kulifuta wao siyo sisi.
Uko sawa,

Na Ukombozi wa Nchi huhitaji watu Wachache wenye kuongoza njia, wengine watafuata.

Aluta continua.
 
Acha kuchekesha...
ccm inaishi kwa sababu ya hizo kasoro sasa wewe unataka waziondoe??πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚
 
Kuwaza kuwa tutapata mabadiliko kupitia uchaguzi, hilo ni kosa kubwa. Hakuna mabadiliko yatakayopatikana kupitia sanduku la kura.

Watawala wanawaza kujiongezea posho na mishahara. Jana wamepitisha muswada wenza wa viongozi nao wawe wanalipwa mishahara pasipo kufanya kazi na pia wawe wanalipwa mafao baada ya kustaafu. Hayo ni mabilioni aisee

Kwa kuwa hatuna mbadala wa CCM, na hatuwezi kuupata kupitia vyama vya siasa na siasa kwa ujumla, serikali ipeleke fedha kwenye miradi tu
 
Ikiwa hayo ndo mawazo Yako,

Ungana na Wazalendo Tarehe 9 Nov, kupinga uchaguzi usifanyike ikiwa hapatakuwa na Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya.
 
Acha kuchekesha...
ccm inaishi kwa sababu ya hizo kasoro sasa wewe unataka waziondoe??πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚
zitaondolewa traaratriiiibuu sio kama wanavyotaka wengine bali wanavitraakaa ccm wenyewe
 
Afaddhalli hata wewe mwenye mawazo ya kipekee na tofauti kabisa na hata CCM wenyewe unaweza jiamulia cha kufanya mwenye kwa bidii na ukatoboa vilivyo....

sawa zingine mabishano haya ya kisiasa, ukiyategemea sana yana tuchelewesha kufika mapema mahali tunapostahili kufika kimaendeleo...
 
zitaondolewa traaratriiiibuu sio kama wanavyotaka wengine bali wanavitraakaa ccm wenyewe
ccm ina elite capture syndromes... Kuna familia zinakaa na kuamua nini kifanyike na nini kisifanyike!
Wengine wote ni machawa wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…