Kweli sikatai ila mleta uzi ana hali mbaya bora waalimuTuongee ukweli, hauwezi kutoboa kupitia ualimu
Na hakuna mtu ambaye ana maisha mazuri kisha akaitamani kazi hii
ila watu huwa wanafanya kama njia, anafanya mambo yake mengine yakitick anang'oka
Ajabu kasomea ualimu. Ana utukana sababu kakosa ajira kila akiombaKuna wakati alifungiwa naona karudi
Yeye kama ualimi haupendi aachie wengine wanaopenda hata vyakula kuna mwingine anapenda hiki kile hapendi
Lakini huyu mwenzetu mleta mada anahitaji tiba ya akili ana dalili za ukichaa.Kitu.kama hukipendi huwezi kuwa kutwa unaongelea hicho tu ni dalili.ya ugonjwa wa akili awahi hospital sio siri na naongea kwa dhati.Hasora ya muda mrefu kwenye kitu.kile kile huzalisha ukichaa
Muda si mrefu atatupa nguo.na kutembea uchi barabarani walio karibu naye wamshauri
Hali jui hilom waalimu wamejiongeza kupitia mikopo wana biashara nzuri zinawapa goodlife. Kenge ambae hata akiambiwa hapo alipo atoe 5M hana na hata dhamana ya kukopa hana.Anajua waalim wa leo ndio wa enzi zile za ualimu wito!!. Siku hizi ualimu kazi.
Sawa wapo choka mbaya kama walivyojaa kwenye kila kada nyingine.
Waoneeni huruma basi hao walimu mnaowadharau na kuwasimanga humu kila siku. Utadhani hamna ndugu zenu ambao kula na kuvaa kwao kunategemea huo huo ualimu na ikitokea umekwenda kumtembelea hicho kinywaji au chakula atakachokuandalia kitakuwa kimetokana na kazi hiyo ya ualimu.Hizi ndio akili za kimaskini hasa Walimu. Utaskia Bora Mimi Nina hata hiyo laki mbili.
Basi ndugu sio vita TUISHI.
Hawa watu kama walilogwa vileMpaka sasa ubao unasoma
Mpwayungu 3 - 0 walimu zero
[emoji16][emoji16][emoji16]
Dah mkuu wasamehe tu watu waishi maisha yao kama ambavyo unaishi yako
Na hapo bado mkurugenzi,wadhibiti ubora,walezi wa kata,afisa taaluma wilaya,afisa utumishi n.kChildish, silly and illogical.
Wewe endelea kubanduliwa mwanaume , acha walioamua kutafuta vipato kwa njia halali wale kwa jasho lao wafurahie kidogo chao wanachopata.
Wewe ndio mpekwe ukishabanduliwa huko unabaki kuwa guilty dume zima hovyo kabisa
Ualimu ni kazi fulani hivi ya hovyo kichizi yaani, ukiwa mwalimu kila mtu ni bosi wako mwanakijiji, mwenyekiti wa kamati ya shule, mwenyekiti wa Kijiji, diwani, mwenyekiti wa ccm, wajumbe wa kamati ya shule, mwalimu mkuu, mwalimu wa taaluma, mwenyekiti wa kitongoji, afisa elimu kata, mtendaji wa Kijiji, mtendaji wa kata, diwani, wachungaji na masheikh, afisa elimu wilaya...n.k
Tena usiombe uwe mwalimu wa vijijini ndo balaa kubwa
Kibaya zaidi hadi wanafunzi wanapewa ukubwa wasiostahili,
Angalia lile tangazo la haki elimu, wanafunzi wanapewa airtime eti washiriki kwenye vikao vya bodi
Sasa mtu amesoma hadi university halafu akae na mtoto wa form one au four kwenye kikao cha bodi si upumbavu huo
Maana yake walimu pamoja na kusoma hawaaminiki
Mbona vikao vya madaktari hawakai na wagonjwa?
Polisi mbona hawakai na wafungwa?
Sisi Waalimu tunajivunia kazi yetu na tunaipendaHii kazi ni ya kipweke sana, unakuwa mnyonge popote ulipo maana huna nguvu ya pesa kwahiyo huwezi kufanya chochote kwenye watu wengi. Hii kazi inahitaji moyo wa chuma
Haina allowance yoyote ileeee, hata kuhama tu ni bure ukibahatika kupewa pesa basi ni laki tano au million moja. Walimu wanaishi ili wasife tu ila hawana future yoyote ileeee
Poleni sana walimu
Am not a teacher.Punguza makasiriko mwalimu wa upe.
Sawa. Uko sahihi kwa mtazamo wako, mimi ni nani nipingane na opinion zako kamanda?Kama ni ajira basi zile za kikoloni. Ila Ualimu ni kibarua tu cha kubangaiza ili ujitafute.
Ualimu sio ajira ni kazi ya wito kwa watoto wa kimaskini.
Mbona walimu wanaheshimika sana kitaaa? Wewe unayewadharau ndo kinyaa! Wana kipato halali hawajaja kwako kukopa! Wanatufundishia watoto wetu! Mungu awabariki sana walimu wetu! Nyerere alikuwa mwalimu! Magufuli alikuwa mwalimu! Zaidi ya 50% ya viongozi wetu (mawaziri na wabunge) walipitia ualimu!
Sio uvumilivu boss ni kukosa namna tu na umaskini.
Kuna jamaa zangu waliamishwaa baadae wakaambiwa hakuna hela za uamisho warudi kwenye vituo vyao vya kwanza, kwa usumbufu huu unadhani madaktari au mwanasheria anaweza ambiwa!?
Mnacomplicate maisha sana!!Nakumbuka miaka ile wanaweka vigezo vya kupata mikopo ya chuo, course niliyochaguliwa sikupata sifa ya kupewa mkopo.
Nikapewa option nibadili course kwenda ualimu ili nipate mkopo, nikakataa.
Nikalazimika kukaa nyumbani mwaka mzima nikijipanga, mwaka uliofuata nikapata chuo course ile ile niliyochaguliwa mwaka jana. Kwa sababu ndio course nilikua napenda.
Najiuliza, hivi kwa principle zangu hizi, ningekua mwalimu si ningekua nishafukuzwa kazi ama kuacha kazi?
Ualimu bongo ni kazi inayotaka uwe na wito na uwe na moyo.