Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nakuunga mkono, akiweza kweli kukaa mbali na wafanya biashara na ki ukweli biashara ikiwa ya haki au ya ushindani wa haki hakuna neno.

Na hilo la kodi, na incentive liwe la watu wote foreigners na locals
 
Ushauri Mzuri Aifunge aisikie Dunia
 
Labda umeme tuu lakini miradi mingine ni liabilities kwa nchi
 
Pongezi nyingi kwa Mhe. Rais kwa Hotuba safi iliyo jaa ukomavu, hekima na busara.

sisi wananchi tumemuelewa na kwa upande wetu tutahakikisha tunampa ushirikiano kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

lkn pia tuna muomba kamwe asiwavumilie watendaji ambao watashindwa kujituma na kutatua kero za wananchi.

tutawafichua wale wote watakao mkwaza au kuhujumu jitahada za Mhe. Rais.
 
Kwa taarifa yako mitandaoni ni mtaani katika digital approach. Usidhani ukiingia mtandaoni basi unahama mtaani. Kwa kukusaidia tu, mtandaoni ni mtaa mkubwa.
Fanya kwanza kauchunguzi utakuja kukubaliana na mimi.
 
Hujajua kwamba CCM iko makundi mawili? Hujaona huko bungeni wabunge wa CCM wakiparuana kuonyeshana upendo kwa JPM na wengine kwa SSH hadi mama akaingilia kati kwamba hao wawili ni "kitu kimoja" ??
Akipitishwa na CCM kugombea tena 2025 upo tayari kumchagua?
 
Fanya kwanza kauchunguzi utakuja kukubaliana na mimi.
Nifanye utafiti wa jambo ninalolijua? Huko mtaani kama watu wako kimya ni kwakuwa watu wako kwenye majukumu yao, na kipindi cha Magufuli watu walijazwa hofu, wakawa wako salama kusifia na sio kukosoa. Inawezekana unatembea na hiyo picha ya hofu, kisha unaleta hapa jukwaani kwamba ndio uhalisia. Toka nje ya box.
 
Achana na mambo ya Magufuli mkuu ndio maana nikakwambia ufanye uchunguzi upate picha halisi huko mitaani, kwahiyo mkuu unataka kusema inawezekana wale waliyokuwa wanatandika kanga kwenye msafara wa kumuaga Magufuli miongoni mwao ni member wa JF ambao walifanya vile vya hofu?
 

Hao wa kutandika kanga mbona walikuwa wachache, ilitakiwa hata wavue nguo ili kuonyesha mapenzi yao kwake, lakini ukweli uko wazi. Na ungetaka kuujua ukweli waliokuwa wanashangilia kifo chake wangeachwa ndio ungepata mrejesho sahihi.
 
Boksi uliloingia sio.. kuna moshi humo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hao wa kutandika kanga mbona walikuwa wachache, ilitakiwa hata wavue nguo ili kuonyesha mapenzi yao kwake, lakini ukweli uko wazi. Na ungetaka kuujua ukweli waliokuwa wanashangilia kifo chake wangeachwa ndio ungepata mrejesho sahihi.
Ishu iko hivi ni kwamba kwa mtazamo wa mitandaoni tusingetegemea kuwa huko mitaani kuna watu wa kufanya, sasa kufikiri kuwa waliyofurahia kifo chake ni zaidi ya ule umati tuliyokuwa tunauona kwenye kuaga sijui umetizama nini hadi uone kuna uwezekano huo? maana ni sawa na ile issue ya maandamano ya Lissu ambayo huku mitandaoni inaonesha watu wamechoka liwalo na liwe lazima waandamane ila siku ya tukio mtaani palikuwa hakuna dalili kabisa ya watu kuwa walikusudia kuandamana wako bize na mambo yao.
 
I cannot say more!
 

Akili ya Kawaida kabisa ingeweza kung'amua walioenda kuhudhuria msiba wa Magufuli, hawakuwa kwenye kitisho chochote cha kuuwawa na vyombo vya dola. Lakini waliotakiwa na Lisu kuandamana dhidi ya ushenzi kwenye uchaguzi ule, dhalimu alishaagiza vyombo vya dola viwaue, kwani hata kwenye huo uchaguzi bado aliagiza wengi kuuwawa, na waliuwawa kweli. Kwahiyo hapa unataka ulinganisho wa waliojitokeza kwa wingi wakiwa salama v/s ambao wangetoka kuandamana tayari kukiwa na amri ya kuuwawa.

Hivyo unatumia kipimo cha mazingira mawili tofauti kuonyesha kukubalika kwa dhalimu, wakati sio kipimo sahihi. Ni kweli waliofurahia kifo cha dhalimu wasingeweza kuwa wengi hadharani maana sio kitendo cha kawaida, na hakukuwa na kiwanja maalum cha wote waliofuhi kukutania ili uone wingi wao. Uwezekano wa waliofurahia kifo cha dhalimu na waliohuzunika ungeweza kuwa sawa, iwapo mazingira yote ya kuonyesha hisia za wahusika yangeachiwa. Huu ndio ukweli, hutaki meza sumu ufe.
 
Ndio nimekuuliza ni kipi kinachokufanya ufikiri kuwa kulikuwa na watu wengi waliyofurahia kifo cha Jiwe sawa na wale tuliyowaona wakimuaga Jiwe au zaidi ya wale? usikimbilie kwenye kificho cha kudai et walikatazwa kana kwamba unajua kwamba hao walikuwepo kweli kwa kiwango sawa na kile ila tatizo ni kukatazwa. Ndio maana nikatoa mfano wa maandamano ya Lissu ambayo kwa kutizama mitandaoni mlikuwa mnaonesha kabisa mpo teyari kwa lolote hamuogopi kitu wengine tukawa tunasubiri tuone hizo fujo zitakuaje kati yenu na jeshi la polisi ila kumbe mtaani hali iko tofauti kabisa na mitandaoni na ndio kile kilichotokea siku ya tukio mtaani watu wako bize na shughuli zao hawakuwa na mawazo ya kufanya maandamano hakukuwa kabisa na dalili za kwamba hawa watu walikuwa wamepanga kufanya maandamano.

Sasa naona unaleta story hizo hizo za et walizuiliwa na ndio ishakuwa sababu ya kujifichia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…