MAMA SAMIA; UNAPOTEZA MUDA WAKO KAMA HUTOFANYIA KAZI HILI,
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Miaka mitatu iliyopita niliandika makala yenye ujumbe wa namna hii nikimtonya aliyekuwa Rais wa wakati huo, Hayatti John Magufuli. Nilimwambia JPM kuwa anapoteza muda wake tuu, na nilizifananisha mbio zake kama mbio za sakafuni ambazo hufika ukingoni kwa upesi.
Mhe. Rais, Samia Hassan Suluhu, usijesema ninadharau uyafanyao isipokuwa nakutonya siri ambayo itakurahisishia kazi ya kulifanya taifa hili kuwa taifa tajiri.
Watu wengi walinipinga, na huenda hata leo wakanipinga, sikatai kupingwa lakini kabla sijapingwa naomba utulivu wa fikra zenu katika jambo hili. Kwa yeyote anayetaka kuongoza taifa hili basi aniazime utulivu wa fikra zake kisha badaye tutajadili kwa kina.
Andiko hili halitamhusu Mama Samia Hassan pekeake bali litawahusu viongozi wote ambao wapo kwenye nafasi kubwa za kufanya maamuzi, pia wale wote wenye ndoto za kuongoza nchi hii.
Mama Samia Suluhu ambaye kwa sasa ni Rais wa taifa letu atahesabika kama kiwakilishi cha viongozi wote wakuu mliopo na mtakaokuja kuongoza nchi hii. Aidha mawazo haya kuchukuliwa ama kutokuchukuliwa haitanifanya nilete chuki kwa washauriwa isipokuwa itakuwa ni wajibu wangu kuyasema yale ninayoona ni nafuu kwa taifa.
Mhe. Rais, ninapenda kukupongeza kwa jitihada kadhaa ulizochukua katika kuleta unafuu katika nchi yetu kama vile ulivyonavyo, hata hivyo natambua yakuwa haupo pekeako, kwani Urais ni Taasisi.
Hatuwezi endelea katika nchi yetu pasipo KUFANYA UVAMIZI NA KUNYONYA WENGINE, hili nitalisema kila siku iendayo kwa Mungu dunia ingalipo mimi nikiwepo. Bila UVAMIZI hakuna maendeleo. Binafsi naamini Maendeleo ni Uvamizi wa maeneo mengine duniani na kuyanyonya.
Hatuwezi endelea kwa kutumia Rasilimali zetu pekeake, hatuwezi endelea kwa kutegemea raia wetu pekee. Huo ni uongo wa mchana kweupe. Siku nchi yetu itakapojua kuwa ili tuendelee tunapaswa kuvamia wengine na kuwanyonya vilivyo ndio siku hiyo hiyo tutaweza kuendelea.
Hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kwa kutumia wananchi wake pekee na rasilimali zake pekee, nchi zote duniani ziliendelea kwa kuvamia mataifa mengine na kuiba kama sio kunyonya mali za nchi zingine.
Taifa la Misri liliendelea kwa biashara ya utumwa ambapo lilichukua watumwa mahali mahali na kuwaleta nchini Misri kufanya kazi za vibarua ambazo Kuwatumikisha wamisri wenzao ingekuwa jau. Hata Waisrael walishawahi kuonja joto la jiwe huko Misri.
WAMEDI, WAAJEMI, WAASHURU, WAGIRIKI, WARUMI wote waliendeleza maeneo yao kwa kuenda kuvamia mataifa mengine na kuiba mali kama madini, mifugo, na watu wenye nguvu kama watumwa.
Wafaransa, waingereza, Wareno, Wajerumani, Wahispania, Waitaliano miongoni mwa wengine walivamia mataifa mengine na kuyageuza makoloni yao, walichuma mali na kunyonya nguvu za makoloni yao mna kujenga nchi zao.
Mataifa kama Japan, Marekani, Uchina, Urusi yamevamia mataifa mengine kwa mtindo wa Uwekezaji na ukoloni mamboleo, teknolojia miongoni mwa mambo mengine.
Mifano hiyo michache inadhihirsha kuwa huwezi endeleza nchi yako kwa level za juu kimataifa pasipo kuvamia wengine na kuwanyonya iwe kwa mabavu au kwa hiyari yao wenyewe.
Taifa letu lazima ifikie hatua tuweke mikakati ya kusaidia watu wetu wapate unafuu na sapoti ya kuweza kuvamia mataifa mengine na kuyanyonya.
Unajua kuchukua kodi kwa raia mwenzako ni noma tofauti na kuchukua kodi kwa raia wa nchi zingine. Kumtumikisha ndugu yako ni kazi zaidi kuliko kumtumikisha mtu baki.
Kanuni inasema, usipovamia unavamiwa, usipokula wenzako basi utaliwa na wenzako. Hiyo ndio kanuni inayoongoza dunia. Usiponyonya utanyonywa. Hakuna nchi iliyoendelea hapa duniani bila kunyonya mataifa mengine, hakuna nchi masikini duniani bila kunyonywa na mataifa mengine. Hakuna.
Nchi yetu imevamiwa kila upande, imezingirwa kila pembe, tumevamiwa kiutamaduni, dini tulizonazo zote ni uvamizi wa kipekee unaozalisha mamilioni kwa mamilioni ya pesa kwenda nchi za dunia ya kwanza. Madhehebu yote makubwa hapa nchini makao yake makuu yapo nchi zilizoendelea. Na sehemu ya kipato cha sadaka huenda huko.
Zile sisi tunaziita Sadaka lakini zile ni pesa na ni mradi ambao ungeweza kuiletea nchi faida. Mapato ya vitabu, vijarida, huduma za kijamii, dhana za muziki nk, hupandisha uchumi wa mataifa hayo.
Ingefaa nchi yetu iwe na dini yake, naamini wapo watu werevu wa kutunga sheria za kimila, desturi, miiko, sala, dua, mavazi, vyakula, ujenzi, kilimo, miuujiza nk ambazo zitaingizwa katika kitabu cha muongoz ndani ya dini yetu. Ili tuwe huru. Nafahamu ni kazi kuanzisha mambo haya lakini hata hizi dini za uvamizi tulizonazo hazikuanzishwa kirahisi, zilianzishwa kwa ugumu tena kwa damu na machozi.
Tayari baadhi ya Watanzania wenzetu washaenda KUVAMIA kwenye mataifa mengine, hawa huitwa walowezi kama sio Diaspora. Serikali inapaswa iwatambua, iwachukulia kama raia wenzetu. Wazalishe huko na kuleta utajiri huku, wakatwe kodi. Mbona wale Ma-explorer, Wamishenari na wafanyabiashara walikuwa wanarejesha mali kwao, kwa nini hawa wetu wasiwekewe utaratibu.
Serikali ipunguze mlolongo katika kuchukua Hati ya kusafiria, iweke utaratibu mzuri wa vijana kuchukua hati hizo na kutafuta pembe za kwenda kusaka maisha. Serikali isiogope ku-take Risk kama kuna vijana wanaotaka kujitoa mhanga. Mbona Kenya, Nigeria wameweza, huu ni muda wa kuvamiana sio kuvamiwa.
Tumeshaona kila uchwao Wachina, Wahindi, mataifa jirani wanavyovamia nchi yetu kung'ang'ania Mali. Serikali isiogope.
Kila siku tunawaona kwenye vyombo vya habari Mamia ya Waethiopia na wasomali wakipita nchi yetu kwenda kuvamia South Africa na maeneo mengine, viongozi wetu hiyo muichukue kama changamoto, changamsheni vijana wetu wawe na hiyo spirit ya kuvamia pasipo woga, unapozima spirit za hivyo ni kuzima maendeleo ya nchi pasipo kujua.
Inafahamika wazi kuwa ni rahisi kufanikiwa ukiwa mbali na nyumbani ukilinganisha na ukiwa nyumbani.
Haya vamia Congo huko, hao vijana wanaojifanya wanapenda upanya road, ujambazi, kusanya wote, peleka jeshini, fundisha mapambano, chukua wote peleka msituni Congo, chukua madini. Imeisha hiyo.
Kila fursa itumiwe ipaswavyo, sio unakamata jambazi unaua, au unafunga unajipa kazi ya kulilinda na kulipa chakula, peleka msituni huko likalete pesa kwa utaratibu maalumu.
Mataifa makubwa yanajua kucheza na mambo ya uvamizi, kuunda vikundi vya waasi au Magaidi makusudically kwa ajili ya kuzalisha uchumi hiyo kwao ni fursa nono wasiotaka iwapite.
Mataifa makubwa hayapotayari kuona fursa yoyote inawapita, mataifa makubwa yanajua ni ngumu kuzuia uovu na mauaji kutoweka duniani hivyo wanaona watumia hao wapenda uovu kujizalishia utajiri.
Mataifa makubwa yanajua kuzuia umalaya ni jambo ambalo lilishashindikana, kama ni hivyo basi wakaona hiyo waigeuze fursa na kuiwekea utaratibu, wakapitisha ikawa ni biashara kama biashara zingine, watu wanalipa kodi, watu wanacheza pono wanauza kwenye mataifa mengine, wanapata pesa.
Sasa lazima tuwe na akili kama ulimwengu huu, ni kweli tunamaadili ila tujue sio wote wenye hayo maadili, na kuyazuia hatuwezi, ndio maana kila mara picha za uchi zinavuja, ingefaa watu wapendao huo mchezo, wachukuliwe wawekewe utaratibu, warekodiwe, ziuzwe nchi zingine watu wajipatie kipato nchi iendelee.
Pengine nikaonekana nimechanganyikiwa lakini ikiwa jambo lolote unalichukia na hulipendi lakini huwezi kulitowesha basi litumie kama fursa kukuzalishia na kukuingizia kipato. Huo huitwa Uvamizi wa kitu usichokipenda.
Wazungu tangu zamani hawatupendi, kutuua wote hawawezi, hivyo kwa sasa wanatutumia kama fursa kwao, na wanajipatia utajiri kupitia sisi wasiotupenda, hiyo ni akili.
Sio kila kitu usichokipenda ukiondoe na kukiangamiza, vingine vitumie kama fursa. Hiyo ndio Akili
Kwa mfano Pombe kidini sio nzuri lakini kuiondoa pombe duniani ni Uongo, yaani haiwezekani kwa sababu wapo wanaoipenda, hivyo serikali zenye akili zikaona kuzuia pombe tumeshindwa sasa tuifanye kuwa fursa, hiyo ni akili
Naweza andika mambo mengi, andiko likawa refu jambo ambalo watu wengi hawapendi,
Lakini lengo langu ni kuwatonya viongozi kuwa nchi hii hatuwezi endelea kwa kutegemea wananchi wa ndani, huko ni kuumizana tuu na kufanya watu wasiwe wazalendo.
Ziundwe kamati zenye watu wenye akili, wanamikakati, wanausalama, wenye roho ngumu, wanataaluma waunde mipango ya kuvamia mataifa mengine.
Kumbuka; Tusipovamia tutavamiwa. Hata hivyo tusipovamia sasa bado itatupasa tuvamie baadaye. Kuvamia hakuepukiki. Tusiwe na aibu ya macho.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300