Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mh rais Samia suluhu Hassan ccm ni chama kinachoelekea kufa ndio maana kina hulka za kibabe na pia tabia za magufuli kutumia nguvu zisiweke kivuli kwenye haiba yako. Tumia busara kuliko nguvu. Mwisho wa siku utapimwa wewe Kama wewe.
Unaandika ukiwa bar ipi?.unataka mwanaccm awasikilize chadema hivi unaakili timamu kweli


USSR
 
Chama ni kikubwa kuliko mtu bila CCM Samia si kitu CCM ipo pale na itakuwa pale ni sawa na Chadema leo umwambie Mbowe afanye mambo nje ya idiology ya Chadema haitowezekana
Utaongea mpaka utakaposoma Katiba ya zamani inavyompa nguvu za kifalme za kufanya lolote alipendalo
 
Mh rais Samia suluhu Hassan ccm ni chama kinachoelekea kufa ndio maana kina hulka za kibabe na pia tabia za magufuli kutumia nguvu zisiweke kivuli kwenye haiba yako. Tumia busara kuliko nguvu. Mwisho wa siku utapimwa wewe Kama wewe.

Ajitenge na CCM wakati CCM ndo imemuweka madarakani. Hilo haliwezi tokea! Tanzania ni nchi ngumu sana kuongoza kwa sasa kwa sababu ya kizazi cha sasa ambacho kimekaa kiuharakati.
 
Nianze na salama...Shikamoo Mama Samia ambae ni Mh.Rais wa JMT.

Siku nyingi nimeandika apa kwenye jamvi tangu mama uchukue usukani wa Taifa letu zuri la Tanzania. Siku ya leo nimetafakari sana utawala wako tangu umeingia Ikulu. Ukweli ni kuwa Mama unafanya vizuri sana.

Ushauri na ombi langu ni zuri na bila shaka linaweza kuchukuliwa na kufanyiwa kazi maana nalipenda Taifa ili nawe pia unalipenda.
Kwa mamlaka ulionayo ni dhairi unaweza kufuta vyama vyote na katiba ili tubaki kufuata utaratibu na fikra zako. Alifanya hivyo Museveni baada ya kuingia Ikulu na Hayati Mzee Karume na walifanikiwa sana.

Nikuombe Mama Samia Rais wetu futeni vyama vya Siasa na Katiba yetu ili tuweze kupiga hatua.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Ushauri mzuri na mfupi
Kweli tutasonga haraka kuliko hiki kiini macho cha katiba na vyama.
 
Rais wangu, Mama Samia Hassan Suluhu wewe ni Rais wangu. Ninajua unazungukwa na wengi ambao ni mapro JPM. Umeshindwa kufanya mambo mengi kwa sababu ya kutaka kubeba yale amabyo pengine yanaonekana yalikuwa mazuri ya JPM. Kuna mengi!

Ulianza na kurudisha Baraza la Mawaziri kwa asilimia kubwa wale wale wa JPM. Kosa kubwa ulifanya hapa. Katika uteuzi wako kwa Makamu wa Rais ulipiga bingo asilimia 100. Waziri Mkuu sitaki kusema lakini mawaziri wengi hukupatia. Awamu yako inatakiwa kuwa na Mawaziri kama yule wa Utumishi - Mchengerewa, Ndugulile, Simbachawene angalau, Ummy angalau, Kitila Mkumbo nafuu, Mkenda bingo kubwa, lakini wengine waliobaki kwa kweli uwongo mbaya hao ni bendera fuata upepo tu. Hawa siku zote wanapoongea sentensi moja inatamka majina ya Rais mara mbili. Hawa ni wabaya watu hawa!

Nilishawahi kumsikiliza Jenister, Mwigulu, Biteko, Ndalichako na hata Gwajima kwa kiasi hawa maneno 50 wanayotamka lazima jina la Rais litajwe! Hawa watu hawafai Mheshimiwa wangu.

Hawa watu walikuwa wanafaa regime iliyopita na hata mambo waliyoyabeba yalikuwa ni regime hiyo. Mhagama ni failure kabisa - kipindi hicho hakufanikiwa kuongeza mishahara ya watumishi na sasa amekuja kukushawishi na wewe usiongeze mishahara ya watumishi wakati nafsi ya moyo wako unakusuta kuwa pengine ungeongeza.

Haki ya Mungu haitakuja kutokea ukaongeza mishahara kwa namna inavyoahidiwa kipindi cha JPM eti alikuwa akisema ni Zaidi ya asilimia 50. Hii haiwezekani na haitakuja itokee. Maneno uliyowapa watumishi yalikuwa ni mazuri na yalitoka moyoni mwako kuhusu kuangalia madai na malimbikizo mengine. Nyongeza ya asilimia moja ya JPM mwaka jana wewe umeifanya vibaya zaidi. Imeongezwa shilingi 2,700/- - hivi kweli hiyo ni nyongeza Rais wangu!?

Hawa watu wanakudanganya - kodi za miamala zimezidi nyongeza ya mishahara, mafuta yaani petrol ya dada Neema imepanda ghafla ili tu eti uendeleze miradi ya JPM. Hilo haliwezekani Rais wangu.

Usitake ku-apply ubabe wa JPM kwenye suala la demokrasia - achana na kuwakamata akina Mbowe! Wewe huna roho ya hivyo - pls usifanye hivyo. Mwendazake alikuwa anaongelea kufa kufa kila wakati akijua nini kilikuwepo mwilini mwake. Wewe haupo hivyo Rais wangu.

Acha demokrasi itamalaki ikusaidie wewe kuongoza vizuri na bila pressure. Nchi hii ni yetu wote hata wapinzani pia. Mie siumii mwanangu kuwa CDM na mimi kubaki na UCCM wangu - je ninakosea? Acha kudeal na hawa watu kwa kuiga roho mbaya ya Mwendazake. Wewe sio wa kukubali watu kupotezwa, wewe sio wa kukubali wastu kupigwa risasi. Usiyabebe hayo kwa ajili ya kuzuia mijadala ya kidemokrasia. Acha watu waongelee Katiba! Kwani kuna ubaya gani? Unapozuia sana hata nafsi yako itaumia siku za usoni.
Rais wangu mpendwa achana na ya Mwendazake chukua ya kwako yaliyo bora hata moyoni mwako! Ninakukubali sana sana na nina matumaini makubwa na wewe kuleta upatanishi, furaha na upendo nchini mwetu. Nafasi bado unayo kubwa sana.
 
Huyu Mama naye ni wale wale tu! Yaani mtu ameingia kupitia mlango wa uani, ila anavyo jititumua! Utafikiri alichaguliwa na majority, tena kupitia uchaguzi huru na wa haki!! Kumbe...........!!!!
 
Rais wangu, Mama Samia Hassan Suluhu wewe ni Rais wangu. Ninajua unazungukwa na wengi ambao ni mapro JPM. Umeshindwa kufanya mambo mengi kwa sababu ya kutaka kubeba yale amabyo pengine yanaonekana yalikuwa mazuri ya JPM. Kuna mengi
Mtamuona kila rais mbaya msipo fuata sheria na taratibu za vyombo vya ulinzi na usalama ukakomalia katiba ambayo ni mama huku kuna sheria za miongozo ya mikutano na maandamano

Mnapanga suicide demonstration huku mkijua ni ugaidi mnategemea nini

Tangu zamani tuliwaonya kuwa marais hufuata sheria za kukusanyika nyie mmekalia eti ni haki ok ni haki ila kunamiongozo ya kukunsanyika hata mikutano ya njiri na mihadhara inaruhusiwa kwa kufuata sheria za mikutanoni ya jeshi la polisi


Mtaumia Sana

USSR
 
Mtamuona kila rais mbaya msipo fuata sheria na taratibu za vyombo vya ulinzi na usalama ukakomalia katiba ambayo ni mama huku kuna sheria za miongozo ya mikutano na maandamano

Mnapanga suicide demonstration huku mkijua ni ugaidi mnategemea nini

Tangu zamani tuliwaonya kuwa marais hufuata sheria za kukusanyika nyie mmekalia eti ni haki ok ni haki ila kunamiongozo ya kukunsanyika hata mikutano ya njiri na mihadhara inaruhusiwa kwa kufuata sheria za mikutanoni ya jeshi la polisi


Mtaumia Sana

USSR
Wewe na mimi mwisho wetu unakaribia!
 
Awabadiishe washauri wake wa hotube.
Ameligawa taifa vipande viwili pale aliposema madai ya katiba ni chokochoko na kwamba yasubiri ajenge uchumi.
Angetoa kisingizio cha corona toka mwanzo kila Mtanzania angekuwa bado ana matumaini naye.
Chokochoko kazitaka mwenyewe kwa ulimi wake.
 
Back
Top Bottom