Rais wangu, Mama Samia Hassan Suluhu wewe ni Rais wangu. Ninajua unazungukwa na wengi ambao ni mapro JPM. Umeshindwa kufanya mambo mengi kwa sababu ya kutaka kubeba yale amabyo pengine yanaonekana yalikuwa mazuri ya JPM. Kuna mengi!
Ulianza na kurudisha Baraza la Mawaziri kwa asilimia kubwa wale wale wa JPM. Kosa kubwa ulifanya hapa. Katika uteuzi wako kwa Makamu wa Rais ulipiga bingo asilimia 100. Waziri Mkuu sitaki kusema lakini mawaziri wengi hukupatia. Awamu yako inatakiwa kuwa na Mawaziri kama yule wa Utumishi - Mchengerewa, Ndugulile, Simbachawene angalau, Ummy angalau, Kitila Mkumbo nafuu, Mkenda bingo kubwa, lakini wengine waliobaki kwa kweli uwongo mbaya hao ni bendera fuata upepo tu. Hawa siku zote wanapoongea sentensi moja inatamka majina ya Rais mara mbili. Hawa ni wabaya watu hawa!
Nilishawahi kumsikiliza Jenister, Mwigulu, Biteko, Ndalichako na hata Gwajima kwa kiasi hawa maneno 50 wanayotamka lazima jina la Rais litajwe! Hawa watu hawafai Mheshimiwa wangu.
Hawa watu walikuwa wanafaa regime iliyopita na hata mambo waliyoyabeba yalikuwa ni regime hiyo. Mhagama ni failure kabisa - kipindi hicho hakufanikiwa kuongeza mishahara ya watumishi na sasa amekuja kukushawishi na wewe usiongeze mishahara ya watumishi wakati nafsi ya moyo wako unakusuta kuwa pengine ungeongeza.
Haki ya Mungu haitakuja kutokea ukaongeza mishahara kwa namna inavyoahidiwa kipindi cha JPM eti alikuwa akisema ni Zaidi ya asilimia 50. Hii haiwezekani na haitakuja itokee. Maneno uliyowapa watumishi yalikuwa ni mazuri na yalitoka moyoni mwako kuhusu kuangalia madai na malimbikizo mengine. Nyongeza ya asilimia moja ya JPM mwaka jana wewe umeifanya vibaya zaidi. Imeongezwa shilingi 2,700/- - hivi kweli hiyo ni nyongeza Rais wangu!?
Hawa watu wanakudanganya - kodi za miamala zimezidi nyongeza ya mishahara, mafuta yaani petrol ya dada Neema imepanda ghafla ili tu eti uendeleze miradi ya JPM. Hilo haliwezekani Rais wangu.
Usitake ku-apply ubabe wa JPM kwenye suala la demokrasia - achana na kuwakamata akina Mbowe! Wewe huna roho ya hivyo - pls usifanye hivyo. Mwendazake alikuwa anaongelea kufa kufa kila wakati akijua nini kilikuwepo mwilini mwake. Wewe haupo hivyo Rais wangu.
Acha demokrasi itamalaki ikusaidie wewe kuongoza vizuri na bila pressure. Nchi hii ni yetu wote hata wapinzani pia. Mie siumii mwanangu kuwa CDM na mimi kubaki na UCCM wangu - je ninakosea? Acha kudeal na hawa watu kwa kuiga roho mbaya ya Mwendazake. Wewe sio wa kukubali watu kupotezwa, wewe sio wa kukubali wastu kupigwa risasi. Usiyabebe hayo kwa ajili ya kuzuia mijadala ya kidemokrasia. Acha watu waongelee Katiba! Kwani kuna ubaya gani? Unapozuia sana hata nafsi yako itaumia siku za usoni.
Rais wangu mpendwa achana na ya Mwendazake chukua ya kwako yaliyo bora hata moyoni mwako! Ninakukubali sana sana na nina matumaini makubwa na wewe kuleta upatanishi, furaha na upendo nchini mwetu. Nafasi bado unayo kubwa sana.