Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mama anapiga kazi vizuri mno, anaupiga mwingi sana.

Zile bifu za kuwekeanza vikwazo na majirani ziliondoa ujjirani mwema ila saizi mama yupo kwenye nyumba basi ujirani mwema umerudi.

Mama kapiga pini kile kikundi cha ngoma cha sukumawiki gang, Raha sana kuona anavyokisambaratisha kwa kutumia peni pekee.

Madarasa yanajengwa

Wafanyabiashara wameanza kurudi kwa kasi kubwa mno.

Sasa hawa vibaraka wa mabeberu nadhani hawajui jinsi watanzania wengi tunavyompenda mama na tupo tayari kumfia, jichanganyeni ndipo mtajua hamjui..

Pia mipango ianza kutekelezeka ya kumuandaa Raisi wa 2030 ambae atakua na mind set kama ya mama
 
Mama anapiga kazi vizuri mno, anaupiga mwingi sana..

Zile bifu za kuwekeanza vikwazo na majirani ziliondoa ujjirani mwema ila saizi mama yupo kwenye nyumba basi ujirani mwema umerudi.
Ahahahahah kwakuwa unapitisha magendo bila tatizo! Wacha nifufue kijiwe cha usadali tu now!
 
Rais/Mama Samia hebu shuhulikia Katiba Mpya ili uwape Wazanzibar wenzio wanachikitaka kwenye muungano kwa muda mrefu huku bara utupe katiba inayoheshimu wananchi na Tume huru ya uchaguzi uone legacy yako haitosahaulika kirahisi.

Ila ukiiacha hii katiba Wanzibar wenzio hawata kuheshimu kwa lolote. Iachie nchi serikali tatu maana yake Serikali la shirikisho na Tanganyika ina ile ya Zanzibar.

Au uache serikali ya majimbo na Zanzibar wawe na serikali yao.
 
Imani na tamaduni nyingi zinaamini kwamba mwanaume ndio pekee anaweza na anatakiwa kuongoza na mwanamke ni wakuongozwa tu na pengine kwa kufuata imani wanaamua kukudharau bila kujua hawakudharau wewe Bali katiba yetu.

Tumesikiliza hotuba yako na tumeilewa dhamira yako kwa rasilimali za nchi yetu ni njema kabisa, tumeelewa Mhe.Rais unapenda haki katika maamuzi yako na zaidi ya yote tumeelewa kwamba daima upo pamoja na wananchi na watendaji wako wanaenda kinyume na maagizo yako ili ujengewe chuki.

Wananchi tunatambua rasilimali zetu zipo mahali salama licha ya baadhi kuona wanaweza kufanya chochote bila kujua wao ndio wanaweza kufanywa chochote. Tunashukuru kilio cha wananchi umekisikia na wasaidizi wako wanakuelewa kuwa hawapambani na wewe bali wanapambana na wananchi, umejenga imani ya kutosha kwa wananchi kuamini kazi iendelee ni falsafa ya kweli kweli.

Unaonesha wasaidizi wako nguvu na mamlaka aliyonayo Rais wa JMT ni kubwa sana bila kutumia nguvu sana na pengine ni onyo kwa atakayebeza basi itabidi utumie mamlaka yako halisi.
 
Uongozi sio jambo lolote bali kufanya maamuzi mazito na magumu ambayo surbonates na wanaoongozwa hawawezi kuyafanya .
Kama kiongozi lazima uwe na jambo linaloelezea wewe ni nani ,una msimamo gani na umeamua gumu lipi.

Malalamiko na kutokukubaliana nawe ni jambo la kawaida sana dhidi ya kiongozi.

lakini lazima kama kiongozi uchukue upande,ufanye na kusimamia maamuzi yenye kukupa upekee.

Katika hili Mhe. Rais Samia so far has been bold enough.

Sisi tunaongozwa hatunabudi kuadapt .


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Ungekuwa ni mtu wa kuwaza kwa kina, ungejiuliza why today and not yesterday.

Hayuko hivyo, bali kuna jambo limemsikuma na likitulia, atarudi Kule kule kwasababu ndio nature yake.
 
Kidogokidogo UTAMKUBALI TU....

Chifu Hangaya ni mtu mstaarabu sana....tatizo nchi hii ni NGUMU....NGUMU MNOOOOO


SIEMPRE CHIFU HANGAYA 🙏
 
Kwa upande wa kwenda na beat nakuaminia hujivungi kbs 🤣🤣🤣🤣
 
Kidogokidogo UTAMKUBALI TU....

Chifu Hangaya ni mtu mstaarabu sana....tatizo nchi hii ni NGUMU....NGUMU MNOOOOO


SIEMPRE CHIFU HANGAYA 🙏
Wewe ni mfuata upepo.
hukumkubali wakati akiwa mgombea mwenza
 
Hamia kwenye madarasa ya Polepole sasa
Sijawahi kumkataa kiongozi wa CCM....

Niliutetea utawala wa JPM kama ninavyoutetea utawala huu.....

Madarasa ya ITIKADI yameniivisha hivyo.....

Siempre JMT
 
ITIKADI ya chama chako ni ipi?
Sijawahi kumkataa kiongozi wa CCM....

Niliutetea utawala wa JPM kama ninavyoutetea utawala huu.....

Madarasa ya ITIKADI yameniivisha hivyo.....

Siempre JMT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…