Enzi za utawala wa Magufuli umeme haukua changamoto kabisa,na hata siku ambayo kulikua na marekebisho ya miundombinu ya umeme basi TANESCO walikua wanatoa taarifa siku mbili kabla ya nini kitatokea na masaa ambayo huduma ya umeme haitopatikana.
Sasa tokea mheshimiwa SSH aingie madarakani mambo yamekuwa vice versa,umeme unakatika hovyo tu na tena hata bila taarifa kwa wateja, mfano siku ya leo sehemu kubwa ya Dar haikua na umeme na hakuna hata kiongozi yeyote wa serikali anayejali hilo suala.
My point is, Mama Samia usipokua makini na hawa Tanesco watakujengea chuki kubwa sana kwa wananchi. Nakuomba uwe mkali mama na ikiwezekana tumbua kuanzia waziri wa wizara husika na menejiment ya Tanesco, tuwekee watu wanaojua kuchapa kazi, sio hao uliowaweka kwani ni kama wanakuhujumu tu.