Tunajua wazi Rais anaongoza serikali ambayo ni Mhimili kati mihimili 3 ya dola, mingine ikiwa ni Bunge na Mahakama.
Serikali ndiyo injini ya shughuli zote za nchi ikiwemo kukusanya mapato na kupanga matumizi. Bunge linapokea mapendekezo yake na kuyakubali au kuyaboresha au hata kuyakataa. Mahakama itashughulika na haki za watu zilizovunjwa na watu ikiwemo serikali yenyewe.
Tangu serikali ya awamu ya 5 ilipoingia madarakani ilijinasibu kwa kutokubali matumizi ya fedha za Umma yasiyo ya lazima, lakini ikaasisi utamaduni mpya wa Mikusanyiko ya viongozi isiyo na umuhimu Bali ni matumizi mabaya ya fedha za Umma. Kikao Kama cha Jana cha kuliana saini ujenzi wa SGR Mkutopora - Tabora anakuwepo Spika, Jaji Mkuu, na Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na Usalama, Mawaziri wote, manaibu wao, Makatibu Wakuu wa Wizara zote, Wakuu wa Mikoa na wilaya za karibu. Wakati mwingine mambo kama haya yalifanyika Chato na niliowataja wakasafiri toka Dodoma na Dar es salaam na wasaidizi kibao kwenye misafara yao.
Utamaduni huu ukaigwa na mikoa na wilaya zote nchini. Naibu waziri Elimu akifika wilayani kukagua miradi msafara wake kama wa Waziri Mkuu. Gari la DMO, Mhandisi Ujenzi, Afisa kilimo wilaya, DC, OCD, DSO, Mshauri wa Mgambo wilaya na msafara unaongozwa na gari la Polisi lenye askari sita au zaidi. Unajiuliza nchi hii ni masikini kweli au Mimi tu ndo masikini?
Hebu angalia utamaduni huu wa ovyo unaotafuna raslimali za nchi kwa kisingizio cha team work.
Huu ni ulaji tu hakuna la maana linalofanyika maana wengine tangu mwanzo wa ziara mpaka mwisho wa ziara hakuna wanachofanya zaidi ya kusaini Posho. Hata kama litajitokeza swali liailohusiana na wizara husika DED ni overall atajibu badala ya Mkuu wa Idara isiyohusiana na Waziri.