Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Ukitaka kufurahisha wote, hutomfurahisha mtu.
Unamtumbua halafu unampetipeti. Ndiyo maana 90% ya budget inaishia kwenye uendeshaji maendeleo 10%
 
Kifupi hatuna mtu hapo, tumepigwa vibaya sana. Aliyeweka kipengele cha kuwa rais lazima awe angalau na degree moja aliona mbali sana., mtu ameinga unga elimu kweli awe rais. Yaami ukimsikilia maamuzi yake ni kama anapata ushauri kwa wake wenza very strange.!
 
Bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi hatutaenda mahali popote, tutapiga mark time tu.
 
Tangu ile Machi aliposema, ^Taifa litakuwa kwenye maombolezo ya siku 14,^ wenye akili tukajua hapa tumepigwa si kidogo!

#KilaMbuziAleUrefuWaKambaYake!
 
Hii nchi tulishapigwa tayari hatuna namna acha waendelee kujipimia.
Hivi Madelu na kiparangoto uwaambie wale ila wajipimie si utakuta sufuria zima halipo matokeo yake wazee wangu wanaostaafu NSSF na PSSF watajuta kuzaliwa kwa kipindi hiki.
Samia ameishashauriwa kuwa Madelu hapo wizara ya fedha hafai, lakini hasikii. “ Sikio la kufa halisikii dawa”
 
Mh Rais nakusabahi kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu na Mh Rais, Nina hakika utakuwa umeskia kauli ya kijana wako Patrobas Katambi, dhidi ya vijana wa Kitanzania.

Mh Rais nina hakika utaungana na mimi sifi leo kuamini yakuwa hiyo ni kauli ya kijana aliyeshiba na kuvimbiwa na urefu wa kamba yake.

Hii ni kauli ya mtu aliye vimbiwa sasa anatapata kupata wapi abeue Ili arufu chafu itoke tumboni mwake, au ni mithili ya aliyevimbiwa Sasa anatapata Ili ewa chafu itoke tumboni mwake tatizo hataki kuchagua harufu hiyo aitolee wapi? Hajui mazingira lakini pia hajui ajibane, itoke taratibu au ajiachie itoke kwa nguvu na mbele ya vijana wenzake.

Silalamiki kwani ruhusu ya kula kwa urefu wa kamba zao uliiitoa wewe, tafadhali waelekeze vijana wako baada ya kuvimbiwa wachague wapi pa kupitisha uchafu wa kuvimbiwa kwao ila kwa staili hii 2025 wenye nchi ni wananchi wataamua kama akuvyosema Spika aliyejiuzuru baada ya kuvimbiwa na kushindwa kuchagua uchafu autoeje tumboni.
 
Kwa mara yangu ya kwanza kwa kipindi cha miaka 40 niliyo tumia barabara ya Arusha Moshi, leo imekuwa njem sana kwangu,
Vile vijiwe vya trafiki kusimamishwa kila baada ya mita 500 kuulizwa una kwenda wapi umetoka wapi as if hujitambui lro havipo.

Kuombwa hela za kupiga rangi viatu leo hakuna.

Happy birthday Mama Samia. Long live.

Kumbe ina wezekana polisi kujitathmini.
 
Kwahiyo unapiga mkwara mwenyewe?!!!!!

Nje ya mada kidogo, hivi kale kajamaa kalikokuwa kanapinga kuwa hii siyo awamu ya sita kapo wapi vileee? Na kale alikokuwa anakaita 'shule' mwenyewe bado kapo?!!!!!!
 
Hadi 2030 mtafika mkiwa mmechoka sana kwa chuki.
 


Watanzania tupate wapi Rais kama huyu?

1. Rais mwenye hofu ya Mungu

2. Rais mnyenyekevu kwa anaowaongoza

3. Rais mpenda watu wake wote

4. Rais mpole na mwenye huruma

5. Rais Mtulivu wa roho na nafsi

6. Rais mzuri wa sura na nafsi

7. Rais msikivu kwa wote

8. Rais mvumilivu na mkarimu kwa wote

9. Rais Mzalendo wa kweli kwa Taifa

10. Rais Mkweli kwa Mungu na wanadamu

11. Rais asiyependa sifa wala kujisifia

12. Rais mwenye moyo mweupe pee

Nauliza tena, Watanzania tupate wapi mtu kama huyu ambae Mungu yuko ndani yake?
 
Mambo yanavyokwenda huku chini siyo mazuri kabisa. Tabia za uzembe rushwa na ufisadi zimerudi kwa kasi kubwa kwenye tahasisi za SERIKALI.

Watu wengi hawakumwelewa mh magufuli jinsi alivyokua anafukuza watendaji wazembe.

Mama chukua hatua haraka maana nyani wanamaliza maindi ya Watoto shambani hali siyo nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…