Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hivyo vyote vitakamilika lakini kuhusu bei maza hana control nayo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hapo la mkongo tuu ndio linawezekana.Mama kapata pesa bil.92 huko UE kwa ajili ya mambo ya kidijitali so stay tuned next budget.
Uwekezaji wa serikali nyingi duniani ktk kukuza technologia ya mawasiliano ni mzuri na kwa dunia ya sasa ni chachu ya maendeleo.

Tatizo kubwa serikali hizi (state) zinaweka nguvu kucontrol watu kupitia technologia kwa sababu teknologia imekuwa nguzo muhimu ya kuhamisisha maandamano yenye nia za kuleta mabadiliko au mapinduzi ktk serikali
 
Leo nimesikia Waziri wa habari akidai yakuwa hii ni serikali ya awamu ya sita,na mambo yake ni kinyume Yale ya awamu ya Tano kusema hivyo ni kutaka kuipaka matope serikali ya awamu ya Tano Ili ionekane ilikuwa mbaya sana.

Nafahamu kabsa yakuwa Nape kwa historia yake, lazima atakuwa Hana Nia njema ya serikali ya awamu ya Tano, maana ilimtumbua baada ya kumtusi Mh Rais wa awamu ile kwa kumuita mshanba na Masaki yakuwa alikuwa akitawala kishamba.

Nape alikuwa Waziri wa habari, aliyoyafanya ana tajua chini ya maelekezo ya kidume Magu leo hii anataka amvue nguo mithil yake alivyovuliwa nguo enzi hizo baada ya kumtusi.

Kama hiyo haitoshi Makamba Jr nae kupitia kwenye wizara ya nishati hasa Tanesco Huyu bwana amekuwa akitoa kauli zinazojichanganya Sana Kila uchwao hasa kuhusu kuunganishwa umeme,na kukatika kwa umeme, amefika atua anatamka wazi eti mitambo haikufanyiwa service muda mrefu kwa sababu jamaa alikuwa anaigopwa HIVi Kuna mtu aliyesoma sayansi kama mwendazake?masuala ya kukatika kwa umeme nani hasiye jua yakuwa Waziri kala dili na wauza majenereta, na Sola wamempa fungu la kufanyia kampeni mapema?kama anabisha aseme .

Kimsingi sisi Kambi ya mwendazake hatufurahiii kamwe uzalilishwaji unao fanywa na mawaziri hasa wale walio tumbuliwa na mwendazake kwa kumtusi leo hii wanaanza kumvua nguo Ili Hali hata boxa aliyozikwa nayo imeisha oza Sasa mnamvua nguo nani akamvalishe?ndugu Samia tafadhali tukumbuke team magu maana na wewe ulikuwa mwenzetu ila Sasa sio wetu ila tulinde.
 
Wakuu habari,

Bwana tulikuwa na kesi since 2019, ya economic case high court, siunajua kipindi Cha magufuli wafanyakazi na wafanyabiashara kupewa mikesi ya ajabu na Mali zako kuzuiwa ilikuwa jambo la kawaida kabisa,Basi mwaka 2019 tulifunguliwa kesi mahakama ya mafisadi ubungo,na dhamana zetu ilikuwa kuweka fedha taslimu au hati za nyumba,bahati nzuri tulifanikiwa kutimiza masharti tukapata dhamana, kila mmoja wetu aliweka dhamana ya tsh. Milioni kumi na mbili, watu wanne jumla milioni 48,
Hapo tulishakaa gereza la keko Kama miezi miwili aisee, na Mali zetu zilizuiwa na serikali,

Hila kwa miujiza ya Mungu, na pia huyu DPP mpya hapendi kuendelea na kesi ambazo hazina mashiko Kama alivyoagizwa na mh. Rais Samia,

Basi bwana week mbili zilizopita bila kutegemea tukaachiwa kwa NOLLE , tukafutiwa mashtaka na DPP,

na tulikuta watu wengi wamefutiwa mashtaka sikuile,kuna mama mmoja alizimia kwa furaha ya mumewe kufutiwa mashtaka baada ya kusota ndani Tangu 2016
 
Korona ilipoanza wachina walijenga hospitali kuanzia msingi mpaka paa kwa siku 10 tu.

Katika historia ya dunia, mama Samia anakuwa rais wa kwanza duniani kujenga shule nzima mpya ya Sekondari kuanzia kuchimba msingi mpaka kupigilia msumari wa mwisho kwenye paa kwa wiki tano pekee.

Shule hii mpya itakuwa msaada kwa watoto wanaotoka Buzuruga na kata za jirani kama vile Mecco, Mahina, buzuruga, Nyasaka nk.
 
Hayo majengo hayakuwa na mabimu? Mda gani yalimwagiliwa
 
Rais kafanya mengi tuu ya maana ya kumpongeza,mbono shule tuu kila siku? Mnaudhi aisee.

Kuna miradi kibao inaendelea
 
Wapingaji wa hii thread wanatakiwa wajiulize, kama viongozi wakuu wa upinzani Mbowe, Lisu na Zito wanamkubali raisi wetu, wao ni nani mpaka nimkatae?! Pongezi za dhati zimuendee raisi wetu na kipenzi cha watanzania wengi mh Samia Suluhu Hassani.
 
~MWANAMKE JASIRI~



[emoji673]Ni mcha Mungu, mwanamke huyu humwambii chochote kuhusu Mungu, anakiwango cha kumpenda Mungu cha hali ya juu, kwenye mambo yote yanayomhusu Mungu yupo mstari wa mbele always, nothing she does bila kumtanguliza Mungu, Ibada zote yumo bila kuchelewa and she writes down the teaching for reference... #GodFirst

[emoji673]Anajipenda na kujithamini..
Anajipenda jinsi alivyo, anapenda uumbaji wa Mungu juu yake na kuthamini kila alichopewa na Mungu. Kumbuka unapojipenda mwenyewe kwa kiwango cha ajabu ni rahisi sana kupenda wengine upendo wa kiungu. Kujipenda ni pamoja na kuwa msafi wa mwili na roho, usafi ni pamoja na kuupenda mwili wako na kuvaa vizuri hata kama una nguo mbili za chafuka nikufue, kauka nikuvae....kuwa na nguo nyingi hakukufanyi ujipende zaidi, kama hujipendi, hujipendi tu #divineLove

[emoji673]Anaheshimu wengine na kujiheshimu.
Kuna siri kubwa sana katika kuheshimu wengine haijalishi umri. Wazungu wanasema #respect is a #reciprocal. Heshima siku zote ina-reciprocate. Mwanamke jasiri hutamani kuona kila mwanamke ama kila mtu anaheshimiwa.
heshima ni tabia, hainunuliwi dukani, ni kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya kwa mwingine bila kujali madhaifu ya mtu kwani binadamu hajakamilika, wote tuna mapungufu, endelea kujiheshimu ili uheshimiwe. #SelfRespect

[emoji673]Hukubali kukosolewa.
mwanamke jasiri anajifunza kila iitwapo leo na yupo tayari kukosolewa pale anapokosea, huthamini mawazo ya watu katika shughuli zake, wakati mwingine hujifanya hajui kitu ili kujifunza. Hamna mwanamke yeyote aliyefanikiwa kwa kujifanya anajua sana, mwanamke jasiri hufurahi pale anapopata mtu wa kumkosoa kwani ni njia rahisi kwake ya kujifunza na kukua kwenye kile akifanyacho #AcceptCriticism

Mwanamke hiyu ni mama bora kwa Taifa letu, Namuunga mkono kwa jitihada zote anazozifanya kulipigania Taifa letu. Mungu ibariki Tanzania na watu wote.

KAZI IENDELEE
 
Tanzania ingekuwa wapi bila Rais Samia?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…