Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Leo nimesikia Waziri wa habari akidai yakuwa hii ni serikali ya awamu ya sita,na mambo yake ni kinyume Yale ya awamu ya Tano kusema hivyo ni kutaka kuipaka matope serikali ya awamu ya Tano Ili ionekane ilikuwa mbaya sana.

Nafahamu kabsa yakuwa Nape kwa historia yake, lazima atakuwa Hana Nia njema ya serikali ya awamu ya Tano, maana ilimtumbua baada ya kumtusi Mh Rais wa awamu ile kwa kumuita mshanba na Masaki yakuwa alikuwa akitawala kishamba.

Nape alikuwa Waziri wa habari, aliyoyafanya ana tajua chini ya maelekezo ya kidume Magu leo hii anataka amvue nguo mithil yake alivyovuliwa nguo enzi hizo baada ya kumtusi.

Kama hiyo haitoshi Makamba Jr nae kupitia kwenye wizara ya nishati hasa Tanesco Huyu bwana amekuwa akitoa kauli zinazojichanganya Sana Kila uchwao hasa kuhusu kuunganishwa umeme,na kukatika kwa umeme, amefika atua anatamka wazi eti mitambo haikufanyiwa service muda mrefu kwa sababu jamaa alikuwa anaigopwa HIVi Kuna mtu aliyesoma sayansi kama mwendazake?masuala ya kukatika kwa umeme nani hasiye jua yakuwa Waziri kala dili na wauza majenereta, na Sola wamempa fungu la kufanyia kampeni mapema?kama anabisha aseme .

Kimsingi sisi Kambi ya mwendazake hatufurahiii kamwe uzalilishwaji unao fanywa na mawaziri hasa wale walio tumbuliwa na mwendazake kwa kumtusi leo hii wanaanza kumvua nguo Ili Hali hata boxa aliyozikwa nayo imeisha oza Sasa mnamvua nguo nani akamvalishe?ndugu Samia tafadhali tukumbuke team magu maana na wewe ulikuwa mwenzetu ila Sasa sio wetu ila tulinde.
Mwaka 2025 ndio atajua kuwa sisi sio wa Samia!!!!!
 
Subiri 2025 mtajua tu"
Tumeshajua
IMG-20220329-WA0015.jpg
 
Nchi Sasa hivi inaendelea kwa kasi na katika nyanna zote kijamii, kisiasa na kiuchumi siyo kama.kipindi kilichopita ambapo nchi ilikuwa angalau inapiga hatua kiuchumi tu Mambo mengine ikatelekeza.

Sasa hivi kila mtu ana raha ndani ya nchii hii. Hakuna uonevu tena wa kunyanyasana na watu wasiojulikana ama kutumbuana bila sababu za msingi.

Sasa hivi mihimili yote inajitegemea na iko huru kabisa
Mtajua 2025 tunawazo letu
Hii sio nchi ya wanawake???
 
Mama Samia punguza kauli za kishujaa hasa wakati huu wa mfumuko wa bei na vitu kupanda.

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Kifupi unataka aseme ndugu watanzania wakati soko la mafuta duniani linaonesha bei kupanda hapa nchini haita kuwa hivyo. Tutafanya kila tunaloweza kushusha bei hiyo kwani tunayo seserve ya kutosha 😁
 
Ni mwanamke kiongozi katika jamii inayotawaliwa na mfumo dume,ambayo ndani yake wanawake wanaamini kuwa nao pia wanapaswa kuwa viongozi!.. hili sio tatizo ila tatizo ni mwanaume na mwanamke kutotambua nafasi zao!.

Wao lazima wa feel hivyo kwasababu ya ugeni huo katika hiyo nafasi,nafikiri ni muda wa kuonyesha matakwa yake kama kiongozi maana nafasi ameshaipata na sio kuonyesha kama anaweza au wanaweza bali kazi sasa iwe kazi!.
 
Katiba mbovu tuliyonayo imetuletea Rais wa wafanyabiashara sio wa wananchi, kila siku anawapa wafanyabiashara visingizio vya kupandisha bei za bidhaa zao.
 
Wakati wenzetu wanapambana kutatua changamoto za uchumi zilizosababishwa na vita ya Ukraine huku kwetu Mapaka yanatutangazia kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na vita hiyo.Nitaendelea kuimba kuwa Tanzania inaongozwa na vibaka.
AARD4K.jpeg
 
Kama huna uhakika wa Jambo usiliongelee ( usikurupuke ) nalo Kwanza halafu ukiwa unaliongelea unasema 'Unadhani' bali achana nalo mpaka pale Wasaidizi wako watakapokupa Ufafanuzi wake wa Kina ili ukija sasa mbele ya Hadhira ( Public ) kutuambia uwe una uhakika nalo 100% pasi na Mashaka.

Katika Hotuba zako nyingi huwa unapenda mno kutumia neno Nadhani / Unadhani kitu ambacho Binafsi kama GENTAMYCINE sioni kama kwa Mtu wa Hadhi yako, Kiongozi wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu ( Commander in Chief ) kutumia neno hilo ni sahihi bali litaanza kutoa / kutupa Mashaka unaotuongoza.

Tunaogopa kuwa ukilizoea sana hili neno la Nadhani / Unadhani yawezekana kuna Siku Taifa Letu likawa Matatizoni ( kwa Majanga au Vita japo GENTAMYCINE siombei ) huku Watanzania tukiangamia na Kufa halafu Wewe ukihojiwa utasema kuwa unadhani 'tunakufa' wakati kumbe 'tunakufa' kweli tena kwa idadi Kubwa tu.

Hili neno la Kudhani / Unadhani acha tu tulitumie Sisi tu Watu wa Kawaida mno huku Mtaani / Mitaani ila Wewe kama Mheshimiwa Rais kiukweli halikupendezi, linakuharibia na hata kufanya baadhi ya Watu ( wenye Umakini mkubwa Kichwani ) waanze kuwa na Mashaka nawe Kiuwezo na Kiutendaji.

Ninaamini hutonichukia Mheshimiwa!!!!!
 
Biblia inasema 'mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru kwelikweli ' kumradhi kwa watu wa imani nyingine lakini kwa sisi wakristo tunaoamini maandiko ya Biblia Takatifu tunaona sasa ni wakati wa watu kuijua kweli. Kwa nini?

i) Uelewa wa watu ni mdogo sana juu kinachoendelea kwenye uchumi. Kukaa kimya kwa serikali kunatafsirika kwamba nao ni sehemu ya vitu kupanda bei.

ii) Samia hajatafuta ushujaa ila amaekuweka tayari kwa ajili ya kufunga mkanda kwa hali inayokuja. Inabidi watu wajue mzalishaji mkubwa duniani wa nishati, madini, nafaka na sunflower yupo vitani na uzalishaji na usambazaji lazima utikiswe.

iii) Nampongeza kutoa taarifa ya hali ilivyo na kwa jinsi ilivyo huo ndio ushujaa.
 
Mama Samia punguza kauli za kishujaa hasa wakati huu wa mfumuko wa bei na vitu kupanda.

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Mama usiingie kwenye mtego wa kijinga huu wa kutaka kudanganya watu Ili kutafuta kupendwa kwa vijimaneno vya sijui comforter and such upuuzi.

Tunaokuunga mkono tunafurahi kwa kusimamia ukweli bila kujalisha waliozoea uongo wanatakaje.

Ukweli na usemwe kama ulivyo

Screenshot_20220330-205324.png
 
Back
Top Bottom