Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mwaka 2025 ndio atajua kuwa sisi sio wa Samia!!!!!
 
Mtajua 2025 tunawazo letu
Hii sio nchi ya wanawake???
 
Mama Samia punguza kauli za kishujaa hasa wakati huu wa mfumuko wa bei na vitu kupanda.

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Kifupi unataka aseme ndugu watanzania wakati soko la mafuta duniani linaonesha bei kupanda hapa nchini haita kuwa hivyo. Tutafanya kila tunaloweza kushusha bei hiyo kwani tunayo seserve ya kutosha 😁
 
Ni mwanamke kiongozi katika jamii inayotawaliwa na mfumo dume,ambayo ndani yake wanawake wanaamini kuwa nao pia wanapaswa kuwa viongozi!.. hili sio tatizo ila tatizo ni mwanaume na mwanamke kutotambua nafasi zao!.

Wao lazima wa feel hivyo kwasababu ya ugeni huo katika hiyo nafasi,nafikiri ni muda wa kuonyesha matakwa yake kama kiongozi maana nafasi ameshaipata na sio kuonyesha kama anaweza au wanaweza bali kazi sasa iwe kazi!.
 
Katiba mbovu tuliyonayo imetuletea Rais wa wafanyabiashara sio wa wananchi, kila siku anawapa wafanyabiashara visingizio vya kupandisha bei za bidhaa zao.
 
Wakati wenzetu wanapambana kutatua changamoto za uchumi zilizosababishwa na vita ya Ukraine huku kwetu Mapaka yanatutangazia kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na vita hiyo.Nitaendelea kuimba kuwa Tanzania inaongozwa na vibaka.
 
Kama huna uhakika wa Jambo usiliongelee ( usikurupuke ) nalo Kwanza halafu ukiwa unaliongelea unasema 'Unadhani' bali achana nalo mpaka pale Wasaidizi wako watakapokupa Ufafanuzi wake wa Kina ili ukija sasa mbele ya Hadhira ( Public ) kutuambia uwe una uhakika nalo 100% pasi na Mashaka.

Katika Hotuba zako nyingi huwa unapenda mno kutumia neno Nadhani / Unadhani kitu ambacho Binafsi kama GENTAMYCINE sioni kama kwa Mtu wa Hadhi yako, Kiongozi wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu ( Commander in Chief ) kutumia neno hilo ni sahihi bali litaanza kutoa / kutupa Mashaka unaotuongoza.

Tunaogopa kuwa ukilizoea sana hili neno la Nadhani / Unadhani yawezekana kuna Siku Taifa Letu likawa Matatizoni ( kwa Majanga au Vita japo GENTAMYCINE siombei ) huku Watanzania tukiangamia na Kufa halafu Wewe ukihojiwa utasema kuwa unadhani 'tunakufa' wakati kumbe 'tunakufa' kweli tena kwa idadi Kubwa tu.

Hili neno la Kudhani / Unadhani acha tu tulitumie Sisi tu Watu wa Kawaida mno huku Mtaani / Mitaani ila Wewe kama Mheshimiwa Rais kiukweli halikupendezi, linakuharibia na hata kufanya baadhi ya Watu ( wenye Umakini mkubwa Kichwani ) waanze kuwa na Mashaka nawe Kiuwezo na Kiutendaji.

Ninaamini hutonichukia Mheshimiwa!!!!!
 
Biblia inasema 'mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru kwelikweli ' kumradhi kwa watu wa imani nyingine lakini kwa sisi wakristo tunaoamini maandiko ya Biblia Takatifu tunaona sasa ni wakati wa watu kuijua kweli. Kwa nini?

i) Uelewa wa watu ni mdogo sana juu kinachoendelea kwenye uchumi. Kukaa kimya kwa serikali kunatafsirika kwamba nao ni sehemu ya vitu kupanda bei.

ii) Samia hajatafuta ushujaa ila amaekuweka tayari kwa ajili ya kufunga mkanda kwa hali inayokuja. Inabidi watu wajue mzalishaji mkubwa duniani wa nishati, madini, nafaka na sunflower yupo vitani na uzalishaji na usambazaji lazima utikiswe.

iii) Nampongeza kutoa taarifa ya hali ilivyo na kwa jinsi ilivyo huo ndio ushujaa.
 
Mama Samia punguza kauli za kishujaa hasa wakati huu wa mfumuko wa bei na vitu kupanda.

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Mama usiingie kwenye mtego wa kijinga huu wa kutaka kudanganya watu Ili kutafuta kupendwa kwa vijimaneno vya sijui comforter and such upuuzi.

Tunaokuunga mkono tunafurahi kwa kusimamia ukweli bila kujalisha waliozoea uongo wanatakaje.

Ukweli na usemwe kama ulivyo

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…