Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ni kati ya viongozi wanaopendwa zaidi Tanzania na Dunia kwasababu anajari maslahi ya wananchi na ya nchi pia , zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazofanya Rais Samia kua kiongozi Bora

1. Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha 6. Mikopo kwa wanafunzi wote wenye vigezo kwaajili ya kupata elimu ya Juu katika Vyuo vikuu vya Umma na Binafsi.

2. Ujenzi wa madarasa 15,000 kuwawezesha wanafunzi wote 907,803 waliopaswa kuanza masomo ya sekondari kuanza masomo kwa wakati mmoja.

3. Kupandisha mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi kuanzia wale wa kima cha chini. Kuongeza posho kwa zaidi ya asilimia 100.

4. Kupandisha madaraja watumishi wa umma wenye sifa, kulipa malimbikizo ya madeni kwa watumishi na kulipa madeni yote halali kwa wazabuni.

5. Kuondoa kodi katika mahitaji muhimu ya wakulima, dhana na vifaa vinavyo athiri moja kwa moja mnyororo wa thamani katika maeneo ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

6. Kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mbalimbali Duniani na Taasisi zenye umuhimu kwa ustawi wa Tanzania.

7. Kuimarisha Sekta binafsi hususani katika biashara na uwekezaji na kutangaza vivutio vya utalii kwa namna ya kipekee Duniani.

8. Kutoa fedha katika miradi yote muhimu na kuanzisha miradi mipya ya maendeleo inayogusa malengo ya muda mrefu na mfupi ya Taifa.

9. Kuboresha huduma za jamii na kuchochea utekelezaji wa mipango endelevu kwa kasi kubwa. Miradi katika huduma za Maji, Afya, Elimu, Kilimo n.k

10. Kutoa vibali vya ajira kwa kila Taasisi yenye uhitaji, kuwawezesha vijana na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwatambua wale wanaochipukia katika eneo la ubunifu na Teknolojia (startups).

Kwa hakika, Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi aliyeweka rekodi ya kipekee Barani Afrika kwa kutekeleza adhma yake ya kuona wananchi wanakuwa na maisha bora. Mungu ambariki ili aendelee kuwatumikia watanzania kwa upendo na aweze kufikia adhma yake kwa 100%.
 
11. Kuongeza matumizi ya serikali na safari za nje pamoja na ufisadi
12. Kuongeza mfumuko wa bidhaa + gharama za maisha
13.. Kuongeza rushwa kwenye taasisi za umma
14. Kurudisha mafisadi kwenye system, udini na ukanda.
15. Kuongeza tozo zisizo na tija
 
Rais Samia ni kati ya viongozi wanaopendwa zaidi Tanzania na Dunia kwasababu anajari maslahi ya wananchi na ya nchi pia , zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazofanya Rais Samia kua kiongozi Bora....
Umesahau haya; Umeme kukatika hovyo, watu kula kwa urefu wa kamba, tozo, bidhaa kupanda bei,maisha kuzidi kuwa magumu,miradi kwenda kwa kusuasua,wizi,uzembe ufisadi,ziara za mabilioni,royal poor,upigaji madini n.k.

 
KWA YANAYOENDELEA NCHINI, NINATOA WITO KWA WATANZANIA WOTE WENYE NIA NJEMA KUANDAMANA MPAKA PALE RAIS ATAKAPOJIUZULU NA UCHAGUZI UITISHWE
 
Ikitokea JPM anafufuka leo na kukuta mambo ambayo Rais Samia Suluhu anayafanya, basi atajawa na tabasamu kubwa sana usoni mwaka na kuona kweli aliacha mtu.

Magufuli atakuta watumishi wa kima cha chini cha mshahara wameongezewa 23.3% kwenye mishahara yao kitu ambacho hajawahi kukifanya ndani ya miaka mitano aliyokaa.

Magufuli atakuta Rais Samia Suluhu amepandisha watumishi madaraja na vyeo, kitu ambacho amekaa madarakani miaka yote mitano aliyokaa madarakani.

Magufuli atakuta watoto waliopewa wa kike waliopewa mimba kwa kubakwa, wamerudi shuleni na wanapata haki yao kikatiba ya kupata elimu, atafunzwa namna bora ya kushughulika na matatizo kama hayo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Magufuli atakuta Tanzania hakuna mwanafunzi aliyemaliza darasa la saba ambaye ana vigezo vyote vya kwenda kidato cha kwanza, eti amebaki nyumbani kisa shida ya madawati, walimu au madarasa. Kwani Rais Samia amejenga madarasa 15,000 nchi nzima ndani ya miezi mitatu tu.

JPM akizinduka kutoka kuzimu leo, atakuta Royal Tour film, filamu ambayo imeleta zaidi tija kwenye ndege ambazo yeye ndiye muazilishi wa kuzinunua. Magufuli atafurahi kuona utalii umekuwa zaidi ndani ya siku 494 za Rais Samia Suluhu madarakani kuliko miaka yake mitano.

Magufuli atacheka na kutabasamu akikuta hakuna mradi hata mmoja wa kimkakati aliyouacha umesimama, hakuna. JHNPP, SGR na miradi yote inatekelezwa kwa kasi ya ajabu.

JPM alifufuka, atampa mkono Samia Suluhu ni kumwambia, "Unaupiga mwingi sana"... hii na kutokana JPM atagundua kwamba alipigwa changa kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwamba ni yeye ndiye hakuelewa muktadha mzima wa bandari ile, ila hivi sasa ndani ya Samia Suluhu, mambo ni beauty beauty.

Hakika JPM alizindua, atafurahishwa na mengi sana ya Samia Suluhu.
 
Dah.... 15. Kudhulumu Mali za masikini na kuzitumia kwa kulamba asali πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Saf
 
Jana nimemsikia Rais Samia kwenye hotuba yake wakati wa kuapisha viongozi aliowateua

Pamoja na kuunga mkono sehemu kubwa ya hotuba yake ila Rais wangu aliniangusha pale alipozungumzia kuhusu watu kuchoma nyama na kunywa kama marafiki

Rais Samia kama mtu ninayekwambia na kukushauri ukweli, napenda kukushauri leo, achana na hayo mambo binafsi ya watu

Hata vitabu vitakatifu vinasema kuhusu kupendana kama ndugu. Mambo ya watu kukutana kama marafiki/ ndugu na kuamua kuchoma nyama huku wakifurahi na kubadilishana mawazo ni mambo binafsi sana na nakuomba usijihusishe na mambo binafsi ya watu maana utakuwa unarudia kosa la mtangulizi wako ambapo alifikia hadi hatua ya kuanza kufuatilia mawasiliano binafsi ya wateule wake.

Rais Samia, napenda kukuhusia kwenye teuzi zako angalia weredi wa mtu, uwezo wake kiakili na kikazi, uzalendo wake na uaminifu wake kwa Taifa na wananchi!

Mambo ya kuangalia kama watu wanakutana kuchoma nyama na kula hayo ni mambo ya kishamba sana na hayana nafasi kwenye dunia ya sasa na hata kwenye vitabu vyetu vya dini. Kwa Wakristo Bwana Yesu alishawai kugeuza maji kuwa divai kwenye shughuli fulani ili watu wanywe na kufurahi.

Kama kuna mshauri wako anakushauri uangalie huo ujinga basi mkaripie maana hakuna binadamu asiye na mambo yake binafsi na ndo mana hata Serikali yetu iliwekaga Leaders clubs kwa ajili ya viongozi kupata nafasi za kupumzika na kubadilishana mawazo

Kwa leo naomba niishie hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…