Naomba ujumbe huu uwafikie rais Samia Suluhu Hassan, wapenzi wake, chawa wake na maadui wote wa Magufuli.
Kwanza, siyo nyinyi tu, Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki mnapaswa kumshukuru Magufuli kwa kuwapatia rais Mwanamke wa kwanza kwenye ukanda huu.
Pili, Rais Samia najua chawa wake walioko humu watakufikishia au kukusemea, bila Magufuli ungekuwa rais? Kwa alivyokuwa mbabe, hata angemteua mke wake msingemzuia mlivyomgwaya.
Tatu, shukuruni haya yote mnayojivunia kama vile madege, reli ya kisasa, barabara na mengine mengi ni kwa sababu ya utundu wake. Bila CCM kumsimamisha Magufuli, ingekuwa ilipo Kanu (Kenya), MCP (Malawi, na UNIP (Zambia).
Nne, mshukuruni lau na kumkumbuka kwa flyovers na flyunders zilizojazana Tanzania.
Mkumbukeni kwa kuufufua mji wa Dodoma na kuufanya mji mkuu kivitendo baada ya kukaa miaka 30 ukiwa ni wa kinadharia.
Tano, leo mnalia hakuna dola. Alipofunga maduka ya kutoroshea dola mengi ya wahindi hamkumuelewa. Mmeruhusu kipumbavu cha moto wafanyabiashara wanakipata.
Bila Magufuli bunge mngekuwa na wapinzani wakipinga upigaji wenu.
Mshukuruni Magufuli kwa kukuza uchumi na kupunguza ubangaizaji na uzembe ambavyo vimeanza kujongea tena.
Bila Magufuli chawa manadhani mngekuwa na ng'ombe wenu , Samia, wa kukamua damu?
Japo hakuwa mkamilifu, alithubutu ambapo wengi walishindwa. Kwa hili lau mkumbukeni na mmpe maua yake.
Naomba kutoa hoja.