Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Raisi Samia angeleta katiba mpya na chaguzi ziwe huru angepewa Nobel Peace Prize. Lakini sidhani kama ana weza bado kufikiria nchi juu ya matakwa binafsi.

Kwa hili kutokea inabidi tupate Rais ambaye Tanzania ni muhimu kuliko madaraka binafsi kama yule wa Botwasana.

Tuiombee nchi hii na tamaduni za ubinafsi kwa uongozi
 
Sijui kama kuna la maana na la kweli zaidi ya uchawa la kumpongeza huyu muungu wenu anayekula na kunonihino.
 
Mama Samia angepumzika nafasi ya uRais imemzidi kimo.

Kukodisha Bandari za Tanganyika na kuziacha Bandari za Zanzibar ilikuwa kosa kubwa ambalo Watanganyika hatuwezi kumsamehe.
 
Katiba Mpya haileti chakula mezani au wewe itakisaidiaje kuongeza kipato chako kama mwananchi?

Rais anatakiwa kuongeza juhudi zaidi kwenye sekta zinazogusa maisha ya wengi eg Kilimo πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://x.com/TanzaniaYaMama/status/1887788912895988067?t=2gR0TWd-cM3ldeMKQ4HOKw&s=19
 
Na Samia hajawahi kuwa na shoo mbovu kamwe πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://x.com/TanzaniaYaMama/status/1887386647479853135?t=KdNHULIPkbfzBIOuE0atTA&s=19
 

View: https://youtu.be/jtDpV2bTh1k?feature=shared
 

Katiba ni mfumo wa uendeshaji shughuli zote za nchi. Kwa sasa kila mtu hata CCM wenyewe wanakubali mfumo wa Tanzania kwenye sehemu zote si mzuri au umepitwa na wakati. Kubadilisha mfumo ndiyo kubadilisha katiba. Mfano modogo tu ambao hauna uhusiano na siasa maana nyie mkisikia katiba mnafikiri chaguzi tu.

Uchumi
Kwa nchi zinazoendelea mfano bank kuu imepewa mandate kwenye katiba kushughulikia ajira. Kwasababu hii bank kuu zinahakikisha mikopo ipo chini ili biashara ziweze kukopa na kuongeza ajira. Hii mandate bank ya Tanzania haina hivyo ajira sio agenda yake. Hivyo kwa sasa bank kuu haijali ajira badala yake inajali faida za mabank tu na hii inasababisha mikopo riba kuwa juu kila mara na kukoshesha ajira vijana. Hii ni ngumu kuielewa kama hujui uchumi.

Kilimo
Migogoro wa Ardhi pia ni tatizo la kikatiba kwa ardhi kumilikiwa na vijiji. Hii inaweka utaratibu wa ununuzi kuwa mrefu na kupunguza uwekezaji. Uwekezaji wa kilimo ndiyo chakula chenyewe

Mahakama
Kwa utaratibu wa sasa kesi za chaguzi zinaweza kuchukuwa zaidi ya miaka 5 ! wakati nafasi za nyeo hazizidi miaka mitano. Yaani mtu anaweza kushinda kinyemela ukaenda kumshitaki halafu ukamshinda miaka mitano ambayo amepata pesa na mshahara bila kuwa na haki. Hii inatakiwa ibadilishwe kwenye katiba

Uraia sheria zimepitwa na wakati

siasa
Tume inatakiwa kuwa huru na wateuliwa wasiwe wateuliwa wa Raisi wapewe budget kikatiba kama mahakama. Kwa faida ya vyama vyote ili chaguzi ziwe huru

Muundo wa serikali idadi ya mawaziri ipunguzwe kikatiba.

serikali za zone zipewe nguvu badala ya kusubiri pesa kutoka Dar au Dodoma

Haya yote yanahusu pesa , uwekezaji na miradi. Yanahusu uchumi ambao ni chakula . Hii ndiyo maana sisi bado ni masikini ni miundo.

Katiba iweke sheria imara za rushwa


Sasa hayo yote hapo ni mifano tu. Katiba ndiyo chakula ndugu yangu acheni kujifanya wajinga
 
Katiba haileti ugali na kwani hayo uliyosema hayapo Kwa Sasa?
 
Hizo tender nyingine anapanga mwigulu na hakuna wa kumuhoji! na ndiyo maana kuwe na katiba na sheria nzuri na mifumo mizuri kwasasa matajiri ni mawaziri tu
Mwigulu ametamkwa kwenye Katiba ipi kwamba anaweza kupanga mipango bila kuhojiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…