Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Raisi Samia lazima uelewe kupigania uhuru wako na haki zako ni nafsi na sio kama kula rojo rojo.

Utashangaa watu watakavyo pigania uhuru na haki zao mwaka huu. kupigania haki hakutaisha mpaka haki ipatikane kwa jasho au kwa damu uhuru na haki za kila Mtanzania zitapatikana
 
Huyo mama Abdul, hana akili kama ilivyo akili yake ilivyo ya chini, elimu yake ya kuunga unga haifahamiki.
 
Naunga mkono hoja ya kupigania haki, ila tumia basi lugha ya kiungwana, lugha ya kistaarabu, kwavile Rais Samia ni Mzanzibari, na Wanzanzibari ndio wala rojo, kumfananisha rais wa nchi na.kula rojo sio lugha ya kiungwana!. Tupiganie haki ila pia tuwe waungwana! . Naendelea kusisitiza Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Rais Samia ni mpenda haki na
Mtenda haki, ana nia njema na ya dhati watu wspate haki zao, ila kuna matatizo mawili, yanamkwamisha...
Tatizo la kwanza ni sisi Watanzania wenyewe hatujui haki zetu, ukiondoa elimu ya sheria, hakuna somo lolote la kuwafundisha Watanzania haki zao, katika mtaala wowote, as a results Watanzania hatujui tudaije haki zetu!. Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?

Tatizo la pili ni watu wake wa vyombo vya utoaji haki, polisi, mahakama etc Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Angalia niliwahi kuandika nini kuhusu Samia na haki


P.
 
Ni kweli kwamba haki za raia na haki za binadamu ni vitu vya msingi kabisa kwa binadamu yoyote yule, ndo maana hata wahalifu wana haki ya kulindwa wasiuliwe au kudhuriwa bila kujali wapo rumande au wapo nje kwa dhamana.

Haki za binadamu na uhuru ni vitu ambavyo vipo na vyatakiwa kuzingatiwa na serikali yoyote ile duniani tangia itangazwe rasmi mwaka 1948 kutambuliwa kwake. Tangazo hili la kutambua haki za binadamu kwa wakati huo lilitangazwa na wazungu baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

Miaka miwili baadae yaani mwaka 1950 bara la Ulaya likatangaza kutambuliwa kwa haki za binadamu barani humo (European Conventions on Human Rights).

Kila nchi barani Ulaya ikatambua sheria hii ya haki za binadamu na ikawa hivyo ikaenda ikarudi haki leo hii. Sheria hii ya haki za binadamu (huko barani Ulaya) yatambua haki na uhuru katika eneo lote la bara la Ulaya, ikimanisha kwamba raia yoyote ndani ya bara la Ulaya ana uwezo wa kutetea haki zake za binadamu kwenye mahakama yoyote barani humo, mahali afanyapo kazi, polisi, manispaa anapoishi kutaka vyombo hivyo kuheshimu haki za raia, uhuru wao, usawa, heshima na utu wao.

Sasa tuangalie ni haki zipi hizi za binadamu wenzetu huko Ulaya wamejiwekea na hadi leo hii haki hizi bado zipo na zazingatiwa katika mazingira yoyote yale iwe kwenye sheria, mahala pa kazi au sehemu zingine.

1. Haki ya kuishi

Serikali ni lazima ilinde maisha ya watu na mtu akifa au kupotea katika mazingira ya kutatanisha ni lazima ufanywe uchunguzi unojotosheleza.

2. Kutoteswa

Mtu hawezi kuteswa kuromaniwa au kudhalilishwa utu wake bila kujali mazingira yoyote yale

3. Kutofanywa mtumwa.

Hakuna mtu kufanywa mtumwa au kushurutishwa kufanya kazi za kitumwa na endapo kuna hali hiyo nilazima uchunguzi ufanywe.

4. Haki ya kuwa huru.

Haki ya kuwa huru iheshimiwe na hata kama mtu awekwa ndani au kukamatwa na polisi ni lazima kuwepo na mingozo inozuia kuwepo uwezekano wa haki hii kukiukwa.

5. Haki ya kusikilizwa mahakamani bila kukandamizwa.

Hii ni haki kusikilizwa ksei yako mahakamani na mbele ya jaji na pia kusikiliza ushahidi wowote dhidi yako.

6. Haki ya kutosulubiwa au kuteswa bila sheria au kufikishwa mahakamani.

7. Haki ya kuheshimiwa usiri wako weye na familia yako.

Kuchungulia dirishani mwa nyumba ya mtu bila sababu maalum, mtu na familia yake wana uhuru wa kuchagua aina ya maisha watakayo.

8. Haki ya uhuru wa kutoa maoni.

haki ya kujieleza na kutoa maoni hata kama maoni hayo hayampendezi yoyote au yanaudhi.

9. Haki ya kutoa maoni

Haki ya kutoa moani na kuyaelezea hata kama hayapendezi au yataudhi watu.

10. Haki ya kuandamana

Haki ya kukusanyika na wengine na kutoa dukuduku kwa amani na polisi na vyombo vingine waruhusu maandamano, mikusanyiko na mikutano.

11. Haki ya kuoa umpendae.

12. Haki ya kutobaguliwa.

13. Haki ya kuheshimiwa mahala unapoishi (nyumbani kwako).

14. Haki ya kupata elimu.

15. Haki ya kupiga kura.

Serikali nyingi za kiafrika baada ya uhuru hazikuketi na kuzungumza kujadili masuala kama haya licha ya kuamua kuunda umoja wa nci huru za kiafrika OAU mwaka 1963. Lengo kuu la kuundwa kwa OAU lilikuwa ni kutaka kuunganisha nchi za kiafrika katika maeneo mawili tu ya kiuchumi na kisiasa.

Malengo mengine makuu kwa wakati huo kwa viongozi walokuwepo akina Kwame Nkruma, Julius Nyerere, Ahmed Sekou Toure Keneth Kaunda, na wengine yalikuwa ni kutokomeza ukoloni na kuzuia kuendelezwa kwa ukoloni mamboleo.

Lakini hadi leo hii na tena baada ya OAU kubadilishwa na kuitwa AU bado taasisi hii hijaketi kuzungumza kuunda au kutoa tamko lolote la kuweka sheria inotambua hakiza binadamu barani Afrika.

Lingekuwa ni jambo la heshima na la maana sana kama OAU wangenaza na kuweka sheria zinosimamia haki za binadamu barani Afrika ambako baadhi ya nchi wanachama wa umoja huo na waanzilishi waandamizi wakikiuka kwa kiasi kikubwa misingi ya haki za binadamu.

Ndo maana umoja wa Ulaya mara kadhaa kwa miongo mingi umekuwa ukisisitiza kwa nchi za kiafrika kuheshimu misingi ya haki za binadamu lakini msisitizo huo umekuwa hauna nguvu yoyote kutokana na kutokwepo kisheria kwa sheria inotambua rasmi haki za binadamu barani Afrika.

Umefika wakati sasa kwa viongozi wachanga kuanza kufikiri kuushawishi umoja huo wa AU au kupitia moja ya vikao vyake kutoa tamko rasmi la kutaka kuwepo kwa sheria rasmi itayotoa onyo kwa nchi wanachama kuheshimu haki za raia wake na liitwe African Conversion on Human Rights.

Ndani ya Conversion hiyo kuwepo sheria ya haki za binadamu Human Rights Act ambayo itaheshimiwa na nchi zote wanachama wa AU. Kuwepo kwa shirika linotetea haki za binadamu barani Afrika kumekuwa kwaonekana kwa kiasi fulani kuwa ni ushawishi wa nchi za magharibi katika siasa za ndani.

Afrika ni lazima sasa tuamke na tuanze kudai kuwepo sheria rasmi ya mtindo wa kiafrika au African Style of Human Rights Act.
 
Ameeeen.
 
Akina Wassira & co wao wanatumia lugha ya staha kutetea uminywaji wa haki Kwa watanzania kunakofanywa na serikali ya ccm?
 
We ni zuzu tu baada ya uchaguzi utakuja na upuuzi mwingine. Mwanaume mzima eti haki, haki ipi umenyanganywa, na nani? Pumbav we kafanye kazi utimize wajibu kwa Taifa lako acha tabia za kike
 
Paskali, Huyu mama anaudhi ndiyo maana wananchi wanamjibu ovyo, ana madharau. Anaendesha nchi vibaya, watu wanaendelea kuiba anaruhusu akina Lugumi waendelee kuiba pesa zetu. Sijui anafanya nini. Hakuna kinachoendelea kizuri kwenye nchi yetu. Leo anasema katiba ni kijitabu tu, yaani nafuu Quran, mbona kwenye hicho kitabu kimeandikwa asifanye uonevu, asiue na asifanye dhulma, yeye hajali hiyo, ni rais wa ovyo kupata kutokea katika nchi yetu.Huyu mama hafai kuwa rais wa nchi yetu, hata uwaziri hafai.
 
Kwa hiyo wewe unatakaje? Urojo.utawanyoosha hadi muombe poo.
 
Pesa zako na nani na kwa nn ushikiwe
 
We ni zuzu tu baada ya uchaguzi utakuja na upuuzi mwingine. Mwanaume mzima eti haki, haki ipi umenyanganywa, na nani? Pumbav we kafanye kazi utimize wajibu kwa Taifa lako acha tabia za kike
We ndio unatabia za kike kbs, kutegemea kudra za watawala ili uishi...wanakushika trako we unaona poa tu kisa ni viongozi!
 
Uvunjifu wa haki za raka unatokana na watu kutokujua namna ya kudai haki zao,, kwa hiyo, ili watz watęndewę kwa haki hawana budi kwanza wasome masomo ya namna ya kudai haki! Kwa mantiki hiyo wanasheria ndio pekee wanaopata haki zao kwa sababu kwenye masomo yao wamefundishwa namna ya kudai haki. Hoja kuntu kutoka kwa mwandishi habari mbobezi na ‘seasoned lawyer’!
 
Kwenye mwili wa Binadamu tumeumbwa kutafakari,kusikiza na kusikilizwa,Raisi ana Kazi Nyingi sana za Nchi kwa ujumla.Hivyo anawashauri wa kumshauri na Huwa anawasikiliza! Kwenye ushauri,huenda wanamshauri vibaya nae huwasikikiza,akiamini wako sahihi na viapo vyao! Mungu mwema atamfumbua macho na Akili ya kutafakari na kutoa maamuzi.Ningekuombea pascal Mayalla, Mungu akupe wepesi na upate teuzi ukawe upande wa ushauri wa Raisi na Nchi isonge kwa Furaha.Ahsante.
 
Pesa zako na nani na kwa nn ushikiwe
Wewe ni mpumbavu na huna akili, ina maana hujui kodi zetu zinalipa mishahara ya hao walio serikalini? Wewe na familia yako mnakaa tu bila kulipa kodi, tuache sisi tunaolipa kodi kwa miaka tuongee, wewe huelewi chochote unaongea kwa kutumia tumbo. Wewe hizo pesa hazikuhusu kupe wewe, mshenzi mkubwa. Hufanyi kazi hulipi kodi, unafanya uchawa kwa kulipwa na hao CCM. Shame on you!
 
CCM hubirini amani na haki kwa pamoja na mfanye kwa vitendo na sio kwa maneno.
Bila haki hakuna amani popote na hili ndio tunatakiwa tuelewe.
Kote duniani watu walipokosa haki walidai kwa nguvu, CCM tusipuuze hili.
 
Good thinking
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…