Mhe. Raisi, nimekua nikifuatilia sana hoja ya uhitaji wa Wahadhiri wenye sifa katika vyuo vikuu vyetu vya uma hapa nchini na kugundua kwamba bado kuna upungufu mkubwa sana. Baada ya kutafakari na kufanya utafiti mdogo, kuna haja ya kutafakari upya kama ifuatavyo;
1. Kuna wahadhiri waliosomeshwa kwa pesa za serikali katika ngazi mbali mbali ikiwemo Masters na PhDs, lakini wameondolewa vyuoni mwaka 2015 na 2020, kisa tu wamegombania aidha UBUNGE au UDIWANI, ilihali wanazo sifa za kuendelea kufundisha na hawana makosa yoyote mengine ya kinidhamu.
2. Wengi wao wanao umri mdogo lakini hawawezi tena kurudi katika utumishi wa uma kwa sababu tayari walikua na account zao ambazo ni ngumu kuzihisha bila kibali maalumu kutoka ofisi ya RAIS - UTUMISHI.
3. Gharama walizotumia (Pesa za serikali) zilizotumiwa kuwasomesha ni kubwa mno, hivyo kuendelea kuwakataa ni hasara kubwa kwa nchi na serikali.
4.Serikali italazimika kutumia fedha nyingi kuwasomesha watanzania au wahadhiri wengine kwa miaka mingi ijayo ilihali wapo wengine waliosomeshwa na kuondolewa kwa sababu ya hoja nyepesi kama kugombania nafasi za kisiasa.
5. Sidhani kama ni sawa kwamba yeyote anaegombania udiwani ama ubunge ni kos lisilo na msamaha hata mtu kutoruhusiwa kabisa kufanya shughuli nyingine za utumishi wa uma.
Hivyo Mhe. Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan tunaomba kada hii ya wahadhiri tuwatambue na tuwaruhusu warudi na kuendelea kulitumikia taifa badala tu ya kuwakataa kisa waligombania nafasi za kisiasa.