Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nampongeza sana Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wetu wa kwanza mwanamke. Hongera sana mama.

Pili hotuba yako imenipa faraja kubwa kuwa unaelewa tatizo lililokuwa linalikabili taifa chini ya Mpendwa wetu John Magufuli hususan katika suala la siasa na demokrasia.

Kwa maoni yangu tulikwama kwenye upande wa siasa na maeneo mengine kadhaa kwasababu ya hofu ya tu ya Mtangulizi wako ama yake binafsi au ya kujengewa na walinzi wake.

Ukiruhusu siasa hususan mikutano ya hadhara na ukakamilisha miradi iliyoanza hakuna wa kukushinda mbeleni. Usiruhusu hofu mama Mungu aliyekupandisha ndie pekee mwenye uwezo wa kukushusha akiamua sio mwanadamu.

Jambo lingine la muhimu ni mabadiliko ya katiba yetu. Namna ulivyopata urais ni mpango wa Mungu ila katiba hii inaweza pia Ku accommodate mipango ya Wanadamu wenye hila mbaya. Naona hakuna check and balance.

Anakufa Rais anatangaza kifo Makamu wa Rais halafu ndie yeye huyo huyo anakuwa Rais Kamili bila process yoyote ya kidemokrasia ni hatari sana kwa Rais aliyepo madarakani .

Hii ikibaki hivi inaweza kufanya watu wakateua watoto wao kuwa Makamu wa Rais kwa hofu ya kutengenezewa mazingira.

Otherwise tumepoteza Rais mtendaji mtu wa matokeo nitamkumbuka daima. Nimejifunza mengi kwake kwa faida yangu binafsi na jamii
 
Kama ambavyo nimekuwa nikija na Tabiri zangu na Maono yangu juu ya Klabu yangu ya Simba na huwa kwa 99,999% huwa ni sahihi na leo nakupa hili na ukilifuata utaongoza vyema na kwa Baraka zote Tanzania.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa najua upo ( tupo ) katika Msiba huu Mzito ila nakuomba sana Msiba ukimalizika fanya hili upesi sana na usichelewe Mama.

Chagua Magereza makubwa Matano Tanzania Bara na Mawili tu kisha panga Ratiba ya Kuyatembelea na ukifika huko omba Wakuu wakupishe na Uongee nao Wewe tu Kwanza kisha ukimaliza utawaita.

Ukimaliza Kuongea nao nakuomba toa AMRI yako ya Kimamlaka ( Executive ) kuwa Wafungwa wote waliofungwa kwa Mambo ya Kisiasa, Kidini na Kubambikiwa Kesi za Ufisadi na Uhujumu Uchumi waachiwe Huru upesi.

Na Wewe Mheshimiwa Rais Samia ukishamaliza kusema hivyo malizia kwa Kiungwana kabisa kuwaambia SAMAHANI KWA YOTE NA SASA TUANZE UPYA KWA KUIJENGA TANZANIA YETU KWA PAMOJA kisha ondoka zako.

Nimekuambia hivi ( haya ) leo kwakuwa ninakupenda sana Mheshimiwa Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan na nataka uiongoze Tanzania hii uliyokabidhiwa leo bila kubeba Lundo la Nuksi inayotokona na Vilio vya Uchungu vya Wafungwa walioko huko Magerezani na wale Ndugu ( Jamaa ) zao wanaoteseka waliopo Uraiani na hawana kwa Kukimbilia sana sana Wote wameamua tu Kumshtakia Mwenyezi Mungu na Yeye pia alianza, ameanza na umakini usipokuwepo ataendelea tu Kuwajibu.

Wiki ijayo nitatoa pia hapa hapa Maono ( Tabiri ) yangu juu ya Mechi Muhimu ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba SC na AS Vita Club kwani naogopa Kutoa Leo ili Watu ( Watanzania ) wasiendelee Kulia na kuwa katika Majonzi mara mbili zaidi ya Msiba mkubwa tulionao sasa na ya Matokeo ya Mechi hiyo ya tarehe 2 April, 2021 pale Mkapa National Stadium.

Nikutakie tu mwanzo mwema wa Urais ( Uongozi ) wako Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ( Allah ) akubariki, akuongoze, akufanikishe vyema.

Wako Jamvini JF,

All - Rounder ( alias ) Brainiac
 
Samia namuona kwamba ni Rais mwenye lugha ya staha,mwenye uungwana na utu.

anayeshaurika,mchapa kazi bila kutaka 'kuabudiwa',aliye makini lakini bila ubabe; asiyejiamria mipango ya kifedha vyovyote atakavyo,mwenye kuuheshimu muhimili wa BUNGE, asiyeelekeza miradi mingi kule tu alikozaliwa,asiye na viashiria vya ukabila;

muwakilishi wetu mzuri kwenye masuala ya Kimataifa, mwenye 'kuwajali' watumishi wa Umma, asiyebeba visasi moyoni, asiyeua vyama vya Upinzani, mwenye bahati za kipekee,Mtumishi Mzoefu Serikalini,Mchumi,pia kwa Taifa zima(mbali na madaraka aliyonayo) yeye bado ni mama yetu mwema!

UNA LA KUMSHAURI NA KUPENDEKEZA?
 
Ajitahidi sana kuwa makini na kundi la serikali ya awamu ya JK. Rais Magufuli hakuwapa nafasi lakini baada ya kufariki wameanza ya kuwa na ndoto mpya za Kuja kuilalua nchi.
 
Kwanza kabisa nandika uzi huu nikiwa na majonzi makubwa ya kufiwa na jemidari raisi wetu kipenzi hayati John Pombe Joseph Magufuli

Kamanda mwanzisha mwendo.Mungu amwepushe na kiama kwani kila mja wake Ni mkosefu mbele yake na yeye husamehe makosa yetu.

Pia nipende kungana na watanzania wenzangu wenye uzalendo uliotukuka katika kipindi hiki kigumu za majonzi kitaifa.

Moja kwa moja kwenye pendekezo langu kwa Raisi wetu .Hutuba kwa taifa kila bada ya mwenzi ni Jambo linaloongeza imani kwa raia wa taifa hasa ikumbukwe ilizoeleka kwa kipindi kirefu

Raisi wetu wa Sasa Ni msikivu, mwenyewe hofu ya Mungu ndani yake .Namini hili pengine likawa Ni desturi yake kuzungunza na watanzania kuwapa mwongozo wa kipi kinafanyika na yapi malengo ya mbeleni in systematic ways kwa njia ya hutuba kwa taifa
Mungu akulinde Raisi Mama Samia Suluhu Hassan akuongeze imani, busara na maarifa
Mungu ibariki Tanzania [emoji173][emoji1241][emoji120]
 
Nimekuelewa Sana hapo.

''Anakufa Rais anatangaza kifo Makamu wa Rais halafu ndie yeye huyo huyo anakuwa Rais Kamili bila process yoyote ya kidemokrasia ni hatari sana kwa Rais aliyepo madarakani ’'
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1.Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2.Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa...
1 sawa, 2 sawa, 3, ikiachwa itakuwa hasara sana maana iko katikati; 5. kama ingewezekana, lakini haiwezekani sasa kuna investment nyingi zimewekwa dodoma. Dsm kwa mahali ilipo inakua yenyewe, dodoma kasi ya kukua itapungua yenyewe tu maana ujenzi.

ukikamilika hakuta tena vivutio vingi vya watu kuwekeza dodoma, Dsm bandari inaibeba sana. 6 hapana, huu mradi ni long overdue sawa na namba 7.

Namba 8 efd siyo mbaya ila wanaotafsri sheria hiyo ndio wanatupeleka pabaya, Sheria imesema mauzo ya zaidi ya 14milioni lakini utakuta kibanda kidogo tu analazimishwa efd.
 
Nimekuelewa Sana hapo.
''Anakufa Rais anatangaza kifo Makamu wa Rais halafu ndie yeye huyo huyo anakuwa Rais Kamili bila process yoyote ya kidemokrasia ni hatari sana kwa Rais aliyepo madarakani ’'
katafakari kwa upana mno
 
Kipindi hiki cha maombolezo siku 21.
1. Radios,Tvs,Magazeti,Online Media zicheze nyimbo za huzuni tu na maombolezo. Maana tunapaswa tumboleze sote.

2. Bendera za aina zote nchini zipepee nusu mlingoti. Zote...kila sehemu.ikikutikana bendera imesimama wima mhusika ahukumiwe kwa kosa la kutaka sababisha machafuko

3. Hakuna kupiga horn yoyote barabarani.na gari sizijae barabarani.iwe kutoka kwa ulazima sana barabara ziwe nyeupe. Na wale wauzaji barabarani wapigwe marufuku wengine huuza radio na vitu vya anasa.

4. Asionekane mtanzania anatembea huku anatabasamu. Au wamekaa wanacheka na kusogoza. Watu kama wamekaa kikundi wawe wamejiinamia na kujishika tama. Na kuongea waongee kwa kupokezana.

5. Kwenye magari kuwe kimya kabisa...haya ya umma. Kimya sana hata sauti ya simu isiruhusiwe watu waweke simu zao silent mode na vibration.

6. Salama iwe ni kwa kupungiana mikono tu. Hakuna kuambiana habari za asubuhi au mambo vipi. Sabab tayari tunajua mambo yote ni mabaya. Hakuna jambo zuri kwa sasa.

7. Asiruhusiwe mtu kununua condoms au kwenda guest house jinsia mbili tofauti ikiwa si mke na mume kwa kuonesha cheti cha ndoa.watu hawa wakiruhusiwa watakuwa wanaenda kusheherekea au kufurahia hakuna cha kufurahia kitu.

8. Wana ndoa wote waambie hakuna tendo la ndoa kwa siku 21 kuunga mkono maomboleza na waliofiwa. Ukibainika ni kifungo.

9. Hakuna kukusanyika sehemu bila kibali maalum.iwe ni nyumba za ibada tu. Bar,Pub na Clubs zifungwe ndani ya siku 21 wote tuhuzunike.maduka ya vitu vya urembo,umeme na visivyo vyakula yafungwe. Yabaki maduka ya vyakula tu na vinywaji muhimu visivyoburudisha. Soda, Juice,beer visiuzwe.

10. Watu wasionekane wamevaa nguo za kupendeza, wasionekane wamevaa nguo maridadi.wanaovaa nguo fupi na za kubana wakamatwe.

Kifupi ni kuwa tunataka nchi iomboleze. Na iomboleze kweli kweli kwa namna ambayo next time tukisikia Rais anaumwa tufunge na kuomba asije akafa ili kuepuka adha hii ya maombolezo. Kama Taifa tunapaswa kushirikiana.
 
Upo ndotoni bwanamdogo unadhani bado tupo chini ya dikteta
 
Back
Top Bottom