Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Ushauri wangu kwa mama Samia in huu
1. Asirithi marafiki wala maadui wa JPJM. Awe makini sana. Wapo watakaoanza kujipendekeza kuwa wao ni waaminifu na bora kuliko wengine. Wko watakao taka kuonesha JPJM alikuwa mkorofi ila yeye ndiye mzuri. Waepuke sana watu hao

2. Futa kesi zote za kisiasa zilizofunguliwa wakati wa JPJM

3. To a msamaha kwa wafungwa wote waliopo magerezani kutokana na masuala ya kisiasa.

4. Ruhusu shughuli za kisiasa ziendelee kwa mujibu wa katiba. Acha vyama vya siasa ikiwemo CCM vifanye shughuli zao bila bughudha wa kuzingatia katiba na sheria ya vyama vya siasa

Pitia upya safu ya viongozi wote wa kuteuliwa kama maDAS, RAS, Wakurugenzi, DC, RC na mawaziri kuona wale ambao in wababaishaji waliopata nafasi hizo kwakujikombakomba na kujiramba ramba kwaJPJM

5. Be humble and kind
 
Nakumbuka ilikuwa mwezi uliopita yaani Februari 2021, wakati wa uzinduzi wa stendi mpya na ya kisasa ya Magufuli, Mh Hayati JPM alituahidi wana Kibamba kuhusu kutujengea barabara za lami kwani ni ndani ya wilaya ya Ubungo ambapo kuna asilimia 5 tu za lami. (Nadhani kati ya hii asilimia tano jimbo la Kibamba tuna asilimia 1 na zilizobaki ni za jimbo la Ubungo).

Nakumbuka baada ya Mh mbunge wetu kuomba kwa unyenyekevu mkubwa mbele ya Rais, Mh Hayati JPM aliagiza pale pale TANROAD kwa kushirikiana na Mbunge waandae mara moja barabara za jimbo la Kibamba ili mheshimiwa atuwekee lami. Kwa jinsi ilivyomuumiza mheshimiwa kuona tuna asilimia ndogo sana ya lami kulinganisha na majimbo mengine ya Dar es Salaam, mheshimiwa Rais kama alivyokuwa hachelewi kwenye kuamua, basi mwaka wa fedha ujao na sisi tungepata hata kuongezewa lami ili angalau tufikie asilimia 25.

Najua, Mheshimiwa Rais Mama Samia na wewe hili ombi uliliona na najua litakuwa tayari mezani kwako. Kwa kuwa umetuahidi kumuenzi Mheshiwa Hayati JPM kwa kutimiza ahadi zake, basi tunaomba tuje mbele zako kwa unyenyekevu mkubwa ili utuangalie kwa jicho la huruma. Wakazi wa kibamba tunapata shida sana. Usafiri wa Umma upo lakini kuna kipindi kinafika tunachelewa makazini make wenye magari hawayapeleki kwenye route hizi kwa kuogopa kufanya magari yao vyuma chakavu. Lakini pia kipindi hiki hata wenye magari binafsi huwa hawatoi lift kabisa. Kwa kweli tunapata shida sana.

Lakini pia, mfano njia ya kupita pale Mbezi High school kwenda Bunju ingekuwa ni njia ya mkato kabisa ya mabasi yote yanayotoka Mbezi kwenda Kaskazini kupitia barabara ya Bagamoyo.

Pia, stendi ya Mbezi tunasema ni Mapokezi ya Taifa (Sebuleni kabisa) kwa maana wageni kutoka nchi mbali mbali watakuwa wanafikia hapo kabla ya kwenda maeneo mengine kufanya biashara zao na shuguli zao zilizowaleta. Litakuwa ni jambo la aibu pale mabasi yanapoingilia ambapo ni Mbezi High school ( kwa maana pameandaliwa hivyo na kuwekwa round about kabisa) kuna lami ya kwenda stand alafu pembeni kidogo tu kwenye barabara inayoelekea Mpigi Magoe ni vumbi na mashimo tupu. Hii itakuwa ni sawa na kusafisha sebule na kurundika uchafu mlangoni.

Sisi wakazi wa jimbo la Kibamba tuna imani na utendaji kazi wako mama na tuna imani mwaka wa fedha ujao na sisi tutakumbukwa kwa maana lilikuwa ni lengo la Hayati Rais JPM kwa sasa kulikumbuka jimbo la Kibamba baada ya kumchagua mbunge wetu kijana kutoka Chama chetu pendwa sana cha Mapinduzi (yaani CCM).

Tunakupenda sana mama na tunakutakia kazi njema. Mungu akubariki katika kazi zako.
 
Ofisi yangu ipo Kibamba, daah full vumbi ilibidi nisogee kidogo. Mama Samia mama la mama fanya kitu baasi
 
Kuhusu malipo ya kubomolewa nyumba vipi tusimkumbushe?
 
Ondoa hofu, tupo kwenye uratibu wa kupata engineer wa Mbezi-Mpiji Magoe na Mbezi-Makabe, hii ya Bunju ipo kwenye uratibu.
___________________
Future thoughts
 
Ofisi yangu ipo kibamba , daah full vumbi ilibid nisogee kidog ..... mama Samia mama la mama fanya kitu baasi
Tuna imani hii ahadi ya wana jimbo la Kibamba aliyoitoa JPM (R.I.P), mama ataitekeleza make ameahidi kumuenzi kwa kutimiza ahadi zake
 
Ondoa hofu, tupo kwenye uratibu wa kupata engineer wa Mbezi-Mpiji Magoe na Mbezi-Makabe, hii ya Bunju ipo kwenye uratibu...
___________________
Future thoughts
Mkuu mnafanya utaratibu wa kumpata Engineer au Contractor? Sijakuelewa mkuu. Nifafanulie kidogo boss.
 
Ni hulka ya binadamu kumheshimu aliemteua na kufanya kiapo mbele yake.
Baada ya kuvaa kofia c.man anza upya unda serikali yako na wateule upya. Wenye sifa ikikupendeza warejeshe.
 
Mimi kwa ufupi nina imani kubwa na huyu mama, kwa wazanzibar kwa kwelinsi wapenda makuu hawana majusifu, kujimwambafya, dharau, tamaa za kujinga, hivyo nategemea kutenda haki na kufuata misingi ya sheria na bila kuingiliwa na mtu. Ushauri ataupokea lakini sio wa kulazimisha. Sina shaka nae hata chembe. Maana katiba ndio msingi wa yote.
 
Nakumbuka ilikuwa mwezi uliopita yaani Februari 2021, wakati wa uzinduzi wa stendi mpya na ya kisasa ya Magufuli, Mh Hayati JPM alituahidi wana Kibamba kuhusu kutujengea barabara za lami kwani ni ndani ya wilaya ya Ubungo ambapo kuna asilimia 5 tu za lami. (Nadhani kati ya hii asilimia tano jimbo la Kibamba tuna asilimia 1 na zilizobaki ni za jimbo la Ubungo).

Nakumbuka baada ya Mh mbunge wetu kuomba kwa unyenyekevu mkubwa mbele ya Rais, Mh Hayati JPM aliagiza pale pale TANROAD kwa kushirikiana na Mbunge waandae mara moja barabara za jimbo la Kibamba ili mheshimiwa atuwekee lami. Kwa jinsi ilivyomuumiza mheshimiwa kuona tuna asilimia ndogo sana ya lami kulinganisha na majimbo mengine ya Dar es Salaam, mheshimiwa Rais kama alivyokuwa hachelewi kwenye kuamua, basi mwaka wa fedha ujao na sisi tungepata hata kuongezewa lami ili angalau tufikie asilimia 25.

Najua, Mheshimiwa Rais Mama Samia na wewe hili ombi uliliona na najua litakuwa tayari mezani kwako. Kwa kuwa umetuahidi kumuenzi Mheshiwa Hayati JPM kwa kutimiza ahadi zake, basi tunaomba tuje mbele zako kwa unyenyekevu mkubwa ili utuangalie kwa jicho la huruma. Wakazi wa kibamba tunapata shida sana. Usafiri wa Umma upo lakini kuna kipindi kinafika tunachelewa makazini make wenye magari hawayapeleki kwenye route hizi kwa kuogopa kufanya magari yao vyuma chakavu. Lakini pia kipindi hiki hata wenye magari binafsi huwa hawatoi lift kabisa. Kwa kweli tunapata shida sana.

Lakini pia, mfano njia ya kupita pale Mbezi High school kwenda Bunju ingekuwa ni njia ya mkato kabisa ya mabasi yote yanayotoka Mbezi kwenda Kaskazini kupitia barabara ya Bagamoyo.

Pia, stendi ya Mbezi tunasema ni Mapokezi ya Taifa (Sebuleni kabisa) kwa maana wageni kutoka nchi mbali mbali watakuwa wanafikia hapo kabla ya kwenda maeneo mengine kufanya biashara zao na shuguli zao zilizowaleta. Litakuwa ni jambo la aibu pale mabasi yanapoingilia ambapo ni Mbezi High school ( kwa maana pameandaliwa hivyo na kuwekwa round about kabisa) kuna lami ya kwenda stand alafu pembeni kidogo tu kwenye barabara inayoelekea Mpigi Magoe ni vumbi na mashimo tupu. Hii itakuwa ni sawa na kusafisha sebule na kurundika uchafu mlangoni.

Sisi wakazi wa jimbo la Kibamba tuna imani na utendaji kazi wako mama na tuna imani mwaka wa fedha ujao na sisi tutakumbukwa kwa maana lilikuwa ni lengo la Hayati Rais JPM kwa sasa kulikumbuka jimbo la Kibamba baada ya kumchagua mbunge wetu kijana kutoka Chama chetu pendwa sana cha Mapinduzi (yaani CCM).

Tunakupenda sana mama na tunakutakia kazi njema. Mungu akubariki katika kazi zako.
Nakubalina nawe kuhusu njia ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini iwe ni ile ya kutoka Mbezi kutokea kule Bunju(nafikiri inapita msitu wa Mabwepande)!. Hii itafaa baada ya kituo cha mabasi kuhamishiwa Mbezi
 
Mama yetu Mh.Rais Samia tayari baadhi ya wanyalokole wameanza ,sijui niiteje,ila kuna mtando uliandika wanadai Mh.Rais MamaSuluhu ni Rais wa katiba na si Rais wa watanzania.ninajua wanamaanisha nini.itakubidi uache porojo za baadhi ya wanasiasa na uanzishe slogan yako kama ambavyo marais waliokutangulia walivyofanya.Hayati JPM bila ya kujali chochote alisimamisha kama sio kuifuta miradi mingi ya Mh Rais mstaafu Kikwete.

Kwa ufupi ni bandari ya bagamoyo.mradi huu ulikuwa na manufaa makubwa.Sasa mpira upo kwako.Nakuomba sana usiige ya watangulizi wako.utashindwa tu.pia utazame ni madeni.kwa kujibu wa gazeti la financisl times la uingereza,si kweli miradi yote na bajeti pesa za ndani.mfano SGR riba au interest ni 22%.ukipiga hesabu ni pesa nyingi sana zitalipwa kama interest.

Anza kwa kudumisha umoja na mshikamo kwa kuwaruhusu vyama vya upinzani uhuru wa kueleza sera zao,kuachia uhuru wa vyombo vya habari n.k.demokrasia ichukue mkondo wake. Uhudhurie mikutano ya kimataifa kama ya DAVOS,UN annual assembly n.k,ipige vita hili gonjwa linalotumaliza la corona kwa wewe kuanza kuvaa barakoa,kukubaliana WHO kuhusu chanjo,kutowakandamiza wafanyabiashara kwa kuwabambikia makodi kibao,kuanza mchakato wa katiba mpya kama wenzetu wa jirani,hili pia litakusaidia kwani mawaziri,majaji na viongozi wengine watawajibika kwa Bunge.

Mawaziri hawatakua wabunge.jopo maalum litawasaili kila mmoja kutokana na taaluma yake.kwa hili utapata timu nzuri sana.haya ni mawazo yangu ingawa ninayo mengi.Naomba kuwasilisha.
Mawazo yako bado yapo katika kuomba omba. Hivi ni lini utakuja kuelewa hakuna msaada wa bure? Huko davos si wataenda mabalozi inatosha. Hata kama tutalipa 22% si ni fedha zetu ya nini upangiwe matumizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubalina nawe kuhusu njia ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini iwe ni ile ya kutoka Mbezi kutokea kule Bunju(nafikiri inapita msitu wa Mabwepande)!.Hii itafaa baada ya kituo cha mabasi kuhamishiwa Mbezi
Kabisa kabisa
 
Ushauri wangu kwa mama Samoa in huu
1. Asirithi marafiki wala maadui wa JPJM. Awe makini sana. Wapo watakaoanza kujipendekeza kuwa wao ni waaminifu na bora kuliko wengine. Wko watakao taka kuonesha JPJM alikuwa mkorofi ila yeye ndiye mzuri. Waepuke sana watu hao

2. Futa kesi zote za kisiasa zilizofunguliwa wakati wa JPJM

3. To a msamaha kwa wafungwa wote waliopo magerezani kutokana na masuala ya kisiasa.

4. Ruhusu shughuli za kisiasa ziendelee kwa mujibu wa katiba. Acha vyama vya siasa ikiwemo CCM vifanye shughuli zao bila bughudha wa kuzingatia katiba na sheria ya vyama vya siasa

Pitia upya safu ya viongozi wote wa kuteuliwa kama maDAS, RAS, Wakurugenzi, DC, RC na mawaziri kuona wale ambao in wababaishaji waliopata nafasi hizo kwakujikombakomba na kujiramba ramba kwaJPJM

5. Be humble and kind
Yaaani vikirudi tu hivyo tutabaki hapahapa kwa miaka 50 ijayo, nchi inaongozwa kisayansi. Ukiruhusu hayo unayoyatka itakuwa kazi kila siku majukwaaani na matumbo. We need kazi hapa kazi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First appearance matter.

Nina muda mrefu sihangaiki kusilikiliza speech za viongozi wa Tanzania.

Leo si tu nimetazama pia nimeona leadership.

Yan Kuna vitu unavitaraji kwa kiongozi na unaviona.

Kwa wasomi ilikua ngumu Sana kuelewa propaganda dhidi ya reality.

Kongole mama

Wananchi wote tumuunge mkono
 
Back
Top Bottom