Mkuu umeongea la muhimu sana! Hasa kwenye sector ya ajira! Je ajira zitatoka wapi? Je serikali inauwezo wakuajiri Graduates wengi sana?? Jibu ni! Hapana! Je serikali itoe wapi sasa hizi ajira??
1. Serikali ikubali kwamba,imeuwa sana sekta binafisi,kwa kuhodhi mambo mengi ikidhani itayaweza! Mfano kwenye Tech,kuna kampuni kama Max Malipo zilitolewa kwenye system baada ya Serikali kuanzisha mfumo wake! Je watu wangapi walipoteza ajira hapa?? Sasa basi inabidi Serikali iziachie sekta binafisi zishindane na Serikali, kama ilivyokua awali! Je Serikali itakubali?? Kugawana mapato na sekta binafisi?? Biashara harali na haramu labda zianze,ndiyo tutaweza kupata pesa! Tusisubiri Serikali,itoe ajira! Hata Rais Samia kipindi anapiga kampeni kule Ludewa mwaka jana alisema,kwamba Serikali haiwezi kuajiri watu wote,tujiajiri! Serikali haina pesa zakuwalipa watumishi! Trust me!
2. Serikali imekua na tabia yakurundika pesa za serikali bank kuu,Je watakubali pesa za Serikali waziachie,ziende kwenye bank za biashara,zikazunguke huko,then zirudi tena mikononi mwa Serikali?? Je Serikali huoni hapo inaruhusu tena watu kutakatisha pesa?? Miradi iliyopo unadhani wataiacha hivi hivi?? Lazima pesa ziende kuendeleza miradi ya Serikali!