Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Binafsi naanza kuona vijembe na mizaha jukwaani. Mara mwenye jinsia ya kike, Mara macho yamelegea, hii yote ya nini? Kweli hadi hapo bado unataka sifa za maumbile? Rais akumbuke kuna kundi pembeni linaangalia kama kabadilika tabia...
Umeongea vizuri sasa tunaomba uende pale geti la Ikulu ukagonge waambie umeenda kumshauri Muheshimiwa aache vijembe watakufungulia tu
 
Hawezi kuwafurahisha wote. Kama wewe huoni furaha kwa aliyoanza nayo SHAURI YAKO. Kaanza vizuri.
 
Wewe mwandishi awamu ya 5 ishapita,mwache Mama yetu Samia atuongoze kwa jinsi anavyoona sawa.Acheni kuandika upuuzi.Wewe unamzungumzia kiongozi wa nchi.Uwe na heshima na adabu.
 
kafanya lipi la ajabu mpaka wewe kukerekwa.au kwa vile mwensio anakimudu kiswahil sasa unaona gere
mbona kaongea kawaida na kwa fasakha kabisa kwa hadhila ile.wewe unavyomuona unahis wa vimemo kisa hajafokq?
 
Mhe Raisi kama itakupendeza kurugenzi ya mawasiliano ikulu mpe Zuhura Yunus wa Bbc. Kwani yeye ni mbombezi, pia wakumbuke wale vijana 5000 walioahidiwa ajira za ualimu mwisho wa siku wakatelekezwa
 
Bila mzaha maisha hayaendi. Kuna mtu alikua anaongea ujinga mtupu na kwa makelele kama visu vinanolewa lakini mlikua mnashangilia tu.
 
Mbona Meko alikua anaongea ujinga mutupu? Waanake weupe blah blah. Samia ndio rais yule kiongozi wa maraika kapangiwa kazi ingine
Ijue jamii inategemea nini kwa wanaume na ni nini toka kwa wanawake. Hukawii kuambiwa malaya! Ulishasikia mwanaume malaya?
 
We acha upuuzi wako
Naona kama upuuzi lakini nakuwa na mashaka na society. Kumbuka yaliyompata Joyce Banda. Baadaye wataanza kutoa maneno ya kudhalilisha ambayo kwa wanaume hayana impacts. Onyo na tahadhari ni muhimu. Kumbuka tahadhari aliyokuwa nayo Obama kwa sababu ya race issue.
 
Kanifurahisha sana alipomnyoa manyoya yule mjivuni aliyelewa madaraka kwa kumtegemea binadamu.

Jana na Leo huyo mjivuni alikua Kama mtu aliyepigwa na mkewe mbele ya watu.
 
Huwezi toa hutuba umenuna tuu muda wote utawachosha wanaokusikiliza,kwani sio kweli maumbile yake ni kike je macho yake hayajalegea utani uko wapi!
Jamani hivi nyie majitu mnaishi nchini au kwa huyo mshenzi na msaliti anayejiita kigogo.Mama yetu Mh Rais Mama Samia ni Rais wa awamu ya 6.Anakwenda kwa spidi ya 5G tena kwa uhakika.

Zile zama za vyuma vimekaza zitaanza kuyeyuka pole pole.Isitoshetunakoelekea sote tutafurahi.Naamini ataheshimu uhuru wa vyombo vya habari,demokrasia,vyama vya siasa kunadi sera zao bila kubugudhiwa,na hata wewe na mimi tutaweza kutoa mawazo yetu kwa uhuru kamili.Rule of Law itakuwepo,kubambikiwa kesi kutaisha,na mengi mengineyo.

Tumuombee aweze kutuongoza kwani ni mpole,lakini anaejua anafanya nini.Keep it Up Mama yetu mpendwa.Tupo Nyuma yako.
 
Ogopa sana watu wenye mizaha..

Kubadilika ni jambo la dk 1 tuu

Kwani humuoni ndugu yako Ndugai?
 
Sioni mapungufu yoyote hapo.

Sense of humour ni bora.

Wakati mwingine ili kuwafanya watu waende na wewe inatakiwa uwe pande zote sio kuwa na ukorofi na ubabe pia kila mmoja na tabia yake hata wewe kuna wengine hawakuelewi
 
kumbe macho ya Mlegezo imekukera?
je angesema ule msemo wa Kwiooo naona ungepasuka
 
Basi baki nayo nyumbani, hapa stendi uwe unakuja kukaa tu....
 
Back
Top Bottom