Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
We ni roho mbaya tu ndo inakusumbua,ndo maana daily Mambo YAKO hayaendi kadri ya mipango YAKO kisa roho mbaya
Mfumo wa kujitegemea so wamanisha kila mtumishi afanye kuacha kutimiza malengo yake kwenye ofisi yake ajikite kutekeleza mfumo wa kujitegemea ,je ufanisi katika ofisi za umma utakuepo, bahati mbaya KWA Sasa Rais ulieanza msifia ni mwelevu japo Hana phd, mshahara KWA mtumishi ni haki ya kisheria sema mlimzoea alieona katiba ni Kama daftari kwamba leo waweza nunua unatumia na ukatupa,
Unafikili maendeleo kwenye taifa yanaletwa na rais tu bila ushirikiano mzuri na watumishi kwenye idara mbali mbali, ni mwenda wazimu anaweza kuja na andiko Kama Hili,
 
Mh rais angalia sana hao viongozi wa dini sio wema kwako,walimpigia makofi JPM hata pasipostahili.endelea na mipango yako mizuri uliyopanga
 
Naandika hii thread nikiwa ninaakili timamu. nchi kwasasa inafuraha naamani tele,maisha ya binadamu nimafupi Sana chamsingi kama rais wa nchi naomba nchi yetu ifanye iwe yenye furaha naamani kama Rais wetu jk alivyoifanya. Misingi ya haki iwekipaumbele hatakama wewe ni mwanasiasa ukifanya vyema tutakukumbuka daima, weka pembeni wale wanao taka kujipendekeza et wao hawajasoma lkn wanafikra zajuu kupita wasomi.lkn Mama fikiria kwa kina kuhusu hilo. Nakama nikwel tufute secta ya elimu tuwape kipaumbele wao wasio enda darasani.

Nakumbuka mh. Jk alipokua presidaa nilikua university niliingia ktk genge la kukashifu kila jitihada zake (upinzani) lkn after mh. Magufuli, kunajambo ninaomba nimuombe radhi jk Rais asiyependa sifa na aliyekua hana makuu. Kilakitu alikifanya bilakuonekana kwenye mass media barabara,maboresho ya watumishi, university of dodoma, free expression, wajasiria mali waliweza kupambana kulingana na haliyao. Mama weee kaja mh. Magu..... Cnamajibu..naomba mawaziriwako wafuate sheria za nchi wasikariri nyakati, nimeona baadhi yao wamegundua kitu ola kuna waziri tamisemi bado anamihemuko ya hayati ajirekebishe. Hatutaki sifa Sisi tunataka haki nchi ni yetu site.
 
Naiona hali hiyo ndiyo anayo ipitia Rais mama samia suluhu kwa sasa na cha ajabu hata viongozi wa dini pamoja na filosofia zao wameshindwa kuwa na ufahamu katika hili badala yake wamekuwa wanafiki .
SSH amesema yeye hakuchaguliwa kwa kura
Na amesema yeye na JPM ni kitu kimoja

Pia amesistiza uache kudemka

 
Lakini tukumbuke kauli zake kuhusu kudumisha mazuri ya aliyemtangulia, na pia kuzidi kuimarisha haki, amani, usawa na demokrasia.
 
Lakini tukumbuke kauli zake kuhusu kudumisha mazuri ya aliyemtangulia, na pia kuzidi kuimarisha haki, amani, usawa na demokrasia.
Sio kama yule mnafiki aliye enda kuzimuni huko huku anasema maendeleo hayana chama huku anasema msipo nipa diwani wa ccm sileti maendeleo yaan yule jamaa yule!!! Ashukuriwe sana mungu kwakweli kwa kumuondosha chap kwa haraka.
 
Back
Top Bottom