Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ,wote tuitikie Kazi iendelee.
Nimefuatilia hotuba ya Madam President na ilikuwa nzuri na kitu kizuri ametupa muelekeo wa serikali yake na tumefahamu falsafa na itikadi anayoimani.
Mama anaamini kwenye mfumo wa soko huria yaani free market economy na democracy ambako definitely ana uzoefu kwa kuwa amefanya Kazi sekta binafsi ikiwa ndio injini ya uchumi wa soko huria.
Binafsi nimefurahia hilo maana hata mimi ni muumini wa soko huria na nachukia ujamaa au centralized economy aliyokuwa nayo Magu.
Pamoja na hayo nitoe tahadhari na maoni yangu kwa ufupi.
1. Mama ahakikishe wafanyabiashara/ wawekezaji wenye pesa hawawaweki mfukoni viongozi wa serikali Ili kudhibiti dhuluma kwa wasio na pesa na kushagihisha haki.Mambo ya siongei na mbwa bali na mwenye mbwa hapana.
2. Kwenye ishu ya vibali vya Kazi,wahusika wakitoa vibali wahakikishe Kazi walizoomba ndio wahusika wanafanya,mambo ya kukuta wachina ni machinga kariakoo hapana.Hapo wakikuta hivyo wapigwe penalty na wafutiwe vibali.
3. Badala ya kuteswa na kivuli cha Magu nashauri useme tuu wazi kwamba wewe sio Magu lakini Uwajibikaji, kutovumilia uzembe na uthubutu kama Magu utavizingatia kama somo kubwa ulilojifunza kwa Magu.Hilo ndilo jambo zuri pekee alilokuwa nalo Magu ila kwenye uchumi alifeli Sana.
4. Toa kipaombele kwenye kuinua sekta ya ndani kwenye uwekezaji Ili kujenga hali ya kujiamini zaidi na incentives ulizosema zisiwe kwa wageni tuu bali hata sisi locals ,wageni iwe ni kwenye maeneo ambayo hatuna uwezo nayo na hasa kwenye usindikaji wa Mazao ya kilimo ,mifugo na samaki kwa ajili ya soko la nje.
5.Ongeza nguvu kwenye sekta ya Afya,maji,afya na miundombinu hasa barabara zote za Vijijini na kuu.Watanzania hawahitaji mamiradi yale makubwa ya Magu maana ni liabilities tuu bali ukitia pesa kwenye hizo sekta nakuhakikishia utashinda uchaguzi kirahisi Sana.
Mathalani sekta ya Afya hadi sasa kuna upungufu wa huduma za afya kwa zaidi ya asilimia 70% nchi zima,,inamaana ukipunguza hadi 50% utakuwa umefanya jambo kubwa Sana.Nchi hii ina zaidi ya vijiji 12,000 zahanati hazizidi 4,000..Kata zaidi ya 3,000 vituo vya afya havizidi 700,, Halmashauri na miji kibao hazina hospital
Kwenye barabara ukiweza kuwapa Tarura angalau bil.500 kutoka bil.270 za sasa ina maana kitakuwa na uhakika wa mawasiliano nchi nzima.
Barabara kuu via Tanroads so far sera ya kuunganisha mkoa kwa mkoa ,nchi yetu na nchi jirani kwa barabara kuu bado haijatekelezwa toka enzi ya Mkapa.Ukifanikisha hili utasidia Sana nchi na watu kiuchumi maana barabara zinachochea maendeleo zaidi kuliko reli na ndege.
5. Mwisho nikupongeze kwa kuturejesha tena kwenye mfumo wa uchumi wa sekta binafsi Ili tujiajiri,tuone kujiajiri ni bora kuliko kutegemea ajira za serikali ambazo hazipo huku tukiitwa wanyonge.
Mwisho kabisa nikupongeze na nikutakie utekelezaji mwema but usilege kukusanya kodi but usiingie kuiba kwenye account za watu kama mwendazake.