Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hongera Mh.Rais kwa hotuba yako ya jana Bungeni. Ulianza kuliambia bunge halina afya kwa maendeleo ya watanzania kwani kazi yao ni kudemka. Walifanya hivyo kwani hawakujiamini bali waliishi kwa mazoea ya kutoenda kinyume na mamlaka.

Kilichotokea ni mama kuwaambia hapo jana waikosoe serikali tena bila woga. Hivyo habari ya nguvu za kiume,nani bora zaidi kati ya Samia na Magufuli sio mahitaji ya wananchi.

Fanyeni kazi na sasa bunge lipo live mnaonekana chapeni kazi na kazi iendelee. Ahsante mh. Rais kwa karata hiyo
 
Unapoteza tu muda wako Kumwambia (Kumshauri) hivi (haya) kwani hakuna Mtu ambaye si tu anapenda bali pia huwa hata 'anakesha' humu Mitandaoni kama huyu ( huyo ) unayemshauri hapa.

Usisahau pia kuwa Asili ya Watu wa Pwani (tena hasa hasa wa Jinsia) yake kupenda Umbeya (Ushambenga) ni moja ya 'Tunu' yao walioachiwa na Mabibi zao.
Ndio Rais wako hutaki HAMA NCHI
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ,wote tuitikie Kazi iendelee.

Nimefuatilia hotuba ya Madam President na ilikuwa nzuri na kitu kizuri ametupa muelekeo wa serikali yake na tumefahamu falsafa na itikadi anayoimani.

Mama anaamini kwenye mfumo wa soko huria yaani free market economy na democracy ambako definitely ana uzoefu kwa kuwa amefanya Kazi sekta binafsi ikiwa ndio injini ya uchumi wa soko huria.

Binafsi nimefurahia hilo maana hata mimi ni muumini wa soko huria na nachukia ujamaa au centralized economy aliyokuwa nayo Magu.

Pamoja na hayo nitoe tahadhari na maoni yangu kwa ufupi.

1. Mama ahakikishe wafanyabiashara/ wawekezaji wenye pesa hawawaweki mfukoni viongozi wa serikali Ili kudhibiti dhuluma kwa wasio na pesa na kushagihisha haki.Mambo ya siongei na mbwa bali na mwenye mbwa hapana.

2. Kwenye ishu ya vibali vya Kazi,wahusika wakitoa vibali wahakikishe Kazi walizoomba ndio wahusika wanafanya,mambo ya kukuta wachina ni machinga kariakoo hapana.Hapo wakikuta hivyo wapigwe penalty na wafutiwe vibali.

3. Badala ya kuteswa na kivuli cha Magu nashauri useme tuu wazi kwamba wewe sio Magu lakini Uwajibikaji, kutovumilia uzembe na uthubutu kama Magu utavizingatia kama somo kubwa ulilojifunza kwa Magu.Hilo ndilo jambo zuri pekee alilokuwa nalo Magu ila kwenye uchumi alifeli Sana.

4. Toa kipaombele kwenye kuinua sekta ya ndani kwenye uwekezaji Ili kujenga hali ya kujiamini zaidi na incentives ulizosema zisiwe kwa wageni tuu bali hata sisi locals ,wageni iwe ni kwenye maeneo ambayo hatuna uwezo nayo na hasa kwenye usindikaji wa Mazao ya kilimo ,mifugo na samaki kwa ajili ya soko la nje.

5.Ongeza nguvu kwenye sekta ya Afya,maji,afya na miundombinu hasa barabara zote za Vijijini na kuu.Watanzania hawahitaji mamiradi yale makubwa ya Magu maana ni liabilities tuu bali ukitia pesa kwenye hizo sekta nakuhakikishia utashinda uchaguzi kirahisi Sana.

Mathalani sekta ya Afya hadi sasa kuna upungufu wa huduma za afya kwa zaidi ya asilimia 70% nchi zima,,inamaana ukipunguza hadi 50% utakuwa umefanya jambo kubwa Sana.Nchi hii ina zaidi ya vijiji 12,000 zahanati hazizidi 4,000..Kata zaidi ya 3,000 vituo vya afya havizidi 700,, Halmashauri na miji kibao hazina hospital

Kwenye barabara ukiweza kuwapa Tarura angalau bil.500 kutoka bil.270 za sasa ina maana kitakuwa na uhakika wa mawasiliano nchi nzima.

Barabara kuu via Tanroads so far sera ya kuunganisha mkoa kwa mkoa ,nchi yetu na nchi jirani kwa barabara kuu bado haijatekelezwa toka enzi ya Mkapa.Ukifanikisha hili utasidia Sana nchi na watu kiuchumi maana barabara zinachochea maendeleo zaidi kuliko reli na ndege.

5. Mwisho nikupongeze kwa kuturejesha tena kwenye mfumo wa uchumi wa sekta binafsi Ili tujiajiri,tuone kujiajiri ni bora kuliko kutegemea ajira za serikali ambazo hazipo huku tukiitwa wanyonge.

Mwisho kabisa nikupongeze na nikutakie utekelezaji mwema but usilege kukusanya kodi but usiingie kuiba kwenye account za watu kama mwendazake.
 
Ayapuuze kweli maana na yeye atakuwa anademka na mambo ya mitandaoni

Tunajua alizoea na anapenda tena kama mwanamke huwa wanapenda kujibu but ukishindwa kuwa na kifua kwa hayo basi wote wanaozusha watafute maana kuna sheria ya mtandao pia.

Nakumbuka hata Magu ilimtesa Sana hii hadi akafikia kusema anatamani malaika washuke kuizima,akaleta sheria kali za mtandao na Takwimu,akakamata watu na kuwafungulia kesi, wengine wakapoea,akafunga na kuzima net nk nk lakini mwisho alichoka na mambo yaliendelea

Ko maza achana na hizo habari zamitandaoni,wanaozusha na kusambaza uongo kamata,akina kimambe na kigogo nk achana nao wewe dili na watu wa ndani.

Mwisho gharama ya teknolojia na uhuru wa maoni ndio hiyo.Dunia ya sasa ogopa Sana Mungu na teknolojia.
 
Hawezi kuacha kuingia mitandaoni maana huku ndio bunge la kweli la wananchi. Ni jinsi gani anadeal na haya mambo ya huku mitandaoni, hilo linategemea na utashi wake. Ila kwa kiongozi yoyote anayetaka kufahamu ukweli wa watu wake, kwa sasa mitandaoni ndio sehemu sahihi ya kupata ukweli huo
Mambo ya mitandaoni hayaleti picha halisi kwa kilichopo na huku mitaani, sio kila kilichopo mitandaoni ndio kinachoendelea mitaani huku.
 
Mambo ya mitandaoni hayaleti picha halisi kwa kilichopo na huku mitaani, sio kila kilichopo mitandaoni ndio kinachoendelea mitaani huku.

Kwa taarifa yako mitandaoni ni mtaani katika digital approach. Usidhani ukiingia mtandaoni basi unahama mtaani. Kwa kukusaidia tu, mtandaoni ni mtaa mkubwa.
 
Mama hakuwa na haja ya kuzungumzia kuhusu uvumi unaohusisha kifo cha Hayati JPM, vitu vingine awe anaviacha vipite kama vumi nyingine tu.
Alikuwa anamjibu na yule alisema -- amekufa kwa COVID19
 
Wee nae famba! Babako amaefanya nini la maana zaidi ya kukuzaa!?
Siku zote nimekuwa nikiwausia ninyi vijana, usiamue Jambo ukiwa bado uko kwenye hasira, au ukiwa kwenye Furaha inayopitiliza, sasa mkuu, Baba yake huyo kijana anahusikaje kwenye Uzi huu??

Tuliza hasira, agiza mkeka uchukue na kitabu kitakatifu, jisomee angalau aya moja huku ukisubilia futari ya jioni
 
Umeongea vizuri sana.
Naunga mkono hoja!

Hii ya kujiita yeye na Magu ni kitu kimoja naamini ni political stunt tu ya kuwapoza wafuasi wa mwendazake, lakini ukweli ni kuwa Samia na Magufuli ni watu wawili tofauti!, hata baadhi ya maamuzi anayochukua unaona wazi ni opposite kabisa na Magufuli.

Cha Msingi Samia:

1.Awe fair, mfariji mkuu, mtu wa haki, aondoe sheria kandamizi, aheshimu katiba, alinde demokrasia

2. Apige vita ufisadi
3. Akamilishe miradi ya kimkakati ya mwendazake
4. Alete maendeleo ya kiuchumi, na hali ya maisha ya watu iboreke
 
Magufuli huwezi kusema kuwa alifeli kiuchumi kwani aliamua kwa makusudi kujenga misingi ya uchumi kuja kuwa endelevu,

Unapojenga reli ya kisasa unatumia pesa nyingi leo lakini ndani ya miaka kadhaa mbeleni reli hiyo ni muhimu sana kwa kurahisisha uchumi huo huo.

Unapohangaikia umeme leo hii mpaka pesa nyingi zikatumika, unakuwa ukitengeneza mazingira ya upatikanaji wa umeme mwingi utakaoondoa kabisa tatizo la mgao wa mara kwa mara, ni nishati ikiwa ya bei ndogo moja kwa moja umesaidia ukuzaji wa uchumi.

JPM alijikuta analazimika kutengeneza ile hali itakayoukuza uchumi mbeleni. Hakuyafanya aliyoyafanya kwa nia ya kuukomoa uchumi kwa nia ya kuwakomoa watu fulani wachache, alijikuta analazimika kufanya maamuzi magumu yenye tija itakayokuja kuonekana siku za mbeleni.

Alilazimika kufufua shirika la ndege kwa kuzingatia umuhimu wake kiuchumi. Corona ikishakuwa imedhibitiwa na safari za ndege zikaanza tena duniani pote, shirika litasimama na faida zake tutaziona.

JPM alikuwa na matatizo yake kama vile kutotabirika, ni hasira zisizo na sababu wakati mwingine zikifanana na visasi lakini kwa ujumla alikuwa na lengo linalotazama miaka kadhaa mbele.
 
Kweli maana mitandao inahusisha kundi dogo sana la wananchi,ndo hiihii mitandao ilimudanganya Lissu anapendwa sana na watanzania atashinda kwa kishindo,kumbe wananchi wakawaida vijijini ambao ndo wengi hawakuwa wanamjua kabisaaa,alichokumbana nacho kwenye sanduku la kura amakijua.
Akajidai maandamano akijua hapa ni sawa na Misri nako yakabuma.
wananchi wa kawaida ndo kwanza wanasikia mambo ya sumu.
 
Back
Top Bottom